ram
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 9,326
- 8,505
Aisee [emoji38][emoji38][emoji38]Kocha kama.unampenda sana Boko mpelekee mabinti zako
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aisee [emoji38][emoji38][emoji38]Kocha kama.unampenda sana Boko mpelekee mabinti zako
Ni kazi sana kushabikia timu isiyo na malengo.....Sisi na ukata wetu tunalisongesha tu, Kaitaba kwetu[emoji1666][emoji1666][emoji111]Bado,mpira unaenda DK 120
[emoji23][emoji23][emoji23]Simba leo walikuwa ugenini?
Nashaanga mabingwa wanacheza nyumbani kwao wanatoa droo na timu isiyofamika, yaonyesha asilimia zaidi ya 100 matokeo yao huko nje yatakuwa mabovu zaidi ya taifa stars[emoji23][emoji23][emoji23]
Walikua wanacheza mechi ya mkoani kwao
Jana keyboard zao ziligoma kuandika kelele za aina hiyo wapo kutafuta kelele zingine za kujifariji nazoHivi zile kelele za "bado hamjaenda kucheza mechi za mikoni" huko kwenu bado zipo?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Jana keyboard zao ziligoma kuandika kelele za aina hiyo wapo kutafuta kelele zingine za kujifariji nazo
Wapo kupekua kamusi kujua maana halisi ya kikosi kipana[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kama nawaona walivyopoa kama kiporo cha ugali
Vanya paluhengo vapigite sawe ukoUnoge be mwagito
Simba wanajifanya wanakikosi kipaana ila hawajui kuwa wanawachezaji wa type moja wa kiungo hawana plan B,leo Lipuli walijaa sana kati wangekuwa na mawinga na kupiga kross wangeshinda game hii, ndo maana kuna dogo aliingia na kupiga kross kadhaa za hatari sana,ila kwa team yetu hamna plan B hata mbambane watawatoa asubuhi tuPatashika la mtifuano wa ligi kuu ya Tanzania bara TPL, linatarajia kutimua vumbi leo Ijumaa Novemba 23, 2018 na kesho kutwa ambapo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam mabingwa wa nchi wana Lunyasi, Pasi mia, Simba SC watawakaribisha wana Paluhengo Lipuli FC.
Kwa mchezo wa leo Simba inahitaji ushindi ili kujiweka vizuri kwenye msimamo wa ligi kuu TPL, kabla ya kuwakabili Mbabane Swallows ya Swaziland katika ligi ya Klabu bingwa Afrika utakaovurumishwa Novemba 27/28 kwenye uwanja wa Taifa. Kumbuka mchezo huu utashuhudia mubashara kupitia Azam Sports 2 kuanzia saa 10:00 jioni.
Vikosi vya timu kwa pande zote mbili kwenye mchezo wa leo hadharaniView attachment 943891View attachment 943892View attachment 943893
Uwanja wa Taifa..Mpira umeanza ni mchezo wa TPL
Simba SC 0-0 Lipuli FC
Timu zimeanza kwa mashambulizi kwa pande zote kwa zamu.
04' John Bocco anakosa bao baada ya shuti lake kupanguliwa na golikipa wa Lipuli FC...ilikuwa hatari sana
07' Simba wanapoteza nafasi nzuri ya kuandika bao..Shuti kali John Bocco kudakwa na golikipa wa Lipuli
10' Matokeo bado bila bila uwanja wa Taifa
Timu zishambuliana kwa zamu..Lipuli wanakwenda kwenye lango la Simba
20' Simba SC 0-0 Lipuli FC
28' Lipuli FC wanakosa nafasi ya wazi kuandika bao baada ya Beki Bukaba kupokonywa mpira na mchezaji wa Lipuli na kupiga shuti lililookolewa na Aishi Manula.
Wawa na Bukaba wanashindwa kukaa sawa huenda Kocha wa Simba akafanya mabadilko kidogo.
30' Kwa mara nyingine tena Lipuli wanakosa bao..Ni kazi nzuri ya golikipa Aishi Manula kupangua shuti na kumkuta mchezaji wa Lipuli na kupiga nje nakuwa goal kick
35' Simba SC 0-0 Lipuli FC
Anakwenda kwenye Benchi Paul Bukaba anaingia James Kotei upande wa Simba SC
40' Faulo kuelekea lango la Lipuli baada ya golikipa kuucheza mpira nje ya 18 wakati Bocco akienda kumsalimia..
Inapigwa faulo lakini haikuzaa matunda
Lipuli wanajaribu kupanga mashambulizi lakini mabeki wa Simba akiongozwa Wawa wanaokoa hatari zote..!
45+3' Ni Mapumziko uwanja wa Taifa mchezo wa Simba na Lipuli ambapo wanatoka bila kwa bila
Simba SC 0-0 Lipuli FC
Kipindi cha pili kimeanza kwa mchezo wa TPL
Lipuli wanatengezea nafasi kwa kujaribu kulifikia lango la Simba..Lakini Simba nao wanazidi kuliandama lango la Lipuli kuona kama wanaweza kupata bao
60' Simba SC 0-0 Lipuli FC
72' John Bocco leo anazidiki kukosa bahati ya kuiandikia timu yake bao..nafasi nyingine tena anapoteza
74' Kichuya anatoka nafasi yake anaingia Haruna Niyonzima upande wa Simba SC
Lipuli wakwenda kumjaribu Manula..lakini Wawa anahakikisha kuwa hakuna kumfikia
77' Goo la la, Ilikuwa hatari lango la Lipuli ni Kapteni John Bocco anapoteza nafasi kwa mara nyingine tena..Leo si yeye tena
80' Simba 0-0 Lipuli FC uwanja wa Taifa.
Rashid anakwenda na kupiga shuti lakini golikipa wa Lipuli anakaa sawa..ilikuwa nafasi murua kwa Simba
90+5 kuelekea kumalizika mchezo huu wa TPL
Naaaaaaaam Mpira umekwisha ambapo timu zinatoka suluhu ya bila kufungana, pamoja na kuwa na mashambulizi makali kwa pande zote lakini Simba walionekana kuwa bora zaidi kutafuta mabao lakini bahati haikiwa yao.
Simba SC 0-0 Lipuli FC
Pamoja na wote hapa JF walioshiriki kuleta mchezo huu shukrani kwenu
Asanteni...Ghazwat
Anaongea sana huyu,angeenda kuwa msemaji wa Taarabu tu
HahahaaaKama kawaida mnyama ananyonya damu mtu bila huruma. Karata ya leo inaonesha tunamzima lipuli kwa bao 4 bila kitu cha 4G
Wacha weeeMnyama mkali tafuna hao wanapaluhengo