Tanzania Premier League 'TPL' Mwadui FC Vs Yanga SC, Uwanja wa Kambarage, Shinyanga

Tanzania Premier League 'TPL' Mwadui FC Vs Yanga SC, Uwanja wa Kambarage, Shinyanga

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania TPL, kuelekea leo Novemba 22, 2018 kwa viwanja viwili kutimua vumbi, ambapo mkoani Shinyanga wenyeji Mwadui FC watawakaribisha Yanga SC kwenye uwanja wa Kambarage.

Kama haitoshi Azam FC vinara wa ligi kuu, watapapatuana na Ruvu Shooting kwenye dimba la Azam Complex.

Vikosi vya mchezo wa Mwadui FC na Yanga SC, kama ifuatavyo. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10:00 jioni.
IMG_20181122_151014_650.jpeg
View attachment 942699

Kuanzia sasa mpira utaanza uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga huku timu zote zikifanya ukaguzi

Naaaaaaaam mpira umeanza kunako dimba la Kambarage


00' Mwadui FC 0-0 Yanga SC

10' Goooal Goooaal Makambo anaandika bao kwa upande wa Yanga baada ya shuti lake la kushoto kwenda moja kwa moja wavuni na kumuacha golikipa akichumpa bila mafanikio

Mwadui FC 0-1 Yanga SC

20' Mwadui wametawala mchezo lakini mashambulizi yao yanashindwa kuzaa matunda.

40' Gooooooooooaaal Salim Aiyee anasawazisha bao upande wa Mwadui FC baada ya shuti la Charles Ilanfya kutemwa na golikipa Kindoki

Mwadui FC 1-1 Yanga SC

Naaaaaaaam mpira ni mapumziko

Awamu ya pili ya mchezo wa TPL inaanza uwanja wa CCM Kambarage

Mwadui FC 1-1 Yanga SC

55' Ngasaaaaaaa gooooal.. Mchezaji wa Mrisho Ngasa anaandika bao la pili baada ya kupiga shuti katikati ya ngome ya Mwadui FC

Mwadui FC 1-2 Yanga SC


Mashambulizi ni kwa pande zote, huku Mwadui FC wakitafuta bao la kusawazisha ili kubaki walau na alama moja

Wakati wowote mpira utakwisha uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga

90' Naaaaaaaam mpira umekwisha ambapo Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Mwadui FC

Mabao ya Yanga yakifungwa na Makambo dakika 10 na Ngasa kunako dakika ya 55 huku bao la Mwadui FC likiwekwa wavuni na Salim Aiyee kunako dakika 40 za mchezo wa TPL

Timu ya JF tumekuletea mtanange huu

Asanteni.. Ghazwat
 
Katika kikosi cha Yanga SC itakosa huduma ya wachezaji wao muhimu Beki kisiki Kelvin Yondani na golikipa Beno Kakolanya ambao hawakusafiri na timu kutokana na matatizo binafsi
IMG_20181122_151425_715.jpeg
IMG_20181122_140249_948.jpeg
 
Du... mbona....wanasawazisha fasta hao....golini kuko salama kweli au limekaa shati ?
 
Back
Top Bottom