Patashika ya Ligi Kuu Tanzania
'TPL' kuendelea kupigwa leo Mei 19, 2019 kunako uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ambapo Mabingwa watetezi
Simba SC, Mnyama Mkali Mwituni, wakiwakaribisha
Ndanda FC Wanakuchele kutoka Mtwara.
Ni mechi inayotarajiwa kuwa ngumu ya vuta nikuvute kwa muda wote wa dakika tisini, kwani katika mchezo wa mzunguko wa kwanza timu hizi zilitoka sare ya kutofungana.
Leo wanapambana tena
Ndanda FC watawasimamisha Simba SC? Au
Simba SC watapata matokeo chanya yatakayowasogeza kushikilia kombe kwa mkono mmoja?
Usikose Ukaambiwa.
Kumbuka mchezo kuanzia saa 10:00 jioni na itakuwa mubashara na Azam Sports 2.
View attachment 1102213View attachment 1102214
Wakati wowote Kabumbu litaanza uwanja wa Uhuru
Naaaaam mpira umeanza uwanja wa uhuru
00' Simba SC 0-0 Ndanda FC
05' Gooooooooooooaaaal goooooaal
Maddie Kagere anahesabu bao la kwanza upande wa Simba akipokea pasi ya Bocco
Simba SC 1-0 Ndanda FC
Simba wanatawala mchezo wa kwa pasi za hapa na pale.
10' Goooooooooooooooooooaaal Maddie Kagere anahesabu bao la pili upande wa Simba
Simba SC 2-0 Ndanda FC
15' Mpira unacheza upande wa Ndanda FC pamoja na kushambuliwa langoni mwao!
Bocco anakwenda, lakini anakosea wanachukua Ndanda wanakwenda mbele kujaribu kushambulia lakini Niyonzima anaharibu mipango
20' Simba SC 2-0 Ndanda FC
Ndanda wanapata faulo..Nahodha Makasi anapaisha na kuwa goal kick
25' bado matokeo Simba wako mbele kwa goli mbili bila majibu...
Zana anaonywa na mwamuzi baada ya kumfanyia madhambi
30' Simba SC 2-0 Ndanda FC,
Wachukua Simba kwake Mo Hussein anatokea golikipa anakuokoa
Kagere anakwenda na mpira mashariki ya uwanja, Ndanda wanajaribu kuondosha hatari ile...
Haya Ndanda wanaonana sasa kujaribu kulisogelea lango mchezaji anapiga ndefu lakini unatoka nje ya lango upande wa Simba
35' Simba SC 2-0 Ndanda FC
Kigi Makasi anaonyeshwa kadi ya Njano baada ya kumchezea faulo Zana Coulibaly
Mkopi anapiga ndefu..Lakini Aishi Manula anatokea na kudaka bila wasiwasi.
Mpaka sasa mpira umepungua ile kasi ya mwanzo
40' kuelekea kuwa mapumziko ambapo Simba wanaongoza kwa bao mbili
Hassan Dilunga anapiga shuti kali kwa umbali mrefu..Lakini unatoka nje kuwa goal kick
V. Manyanga anakwenda na anapiga chenga hata hivyo anaukosea..!