Tanzania Programmers ni kweli tunafeli ni kweli hatuna uwezo wapi tunapokwama, nini kifanyike?

Kuna ule usemi usemao ''chema chajiuza, kibaya chajitembeza''. Tanzania ni nchi ya watu wa maneno mengi. Kazi nyingi tunazifanya kwa maneno. Hii culture imejengeka sana kwa sababu chimbuko la uongozi wetu na makao makuu ya nchi ni Pwani. Na unajua tena watu wa Pwani ni watu wanaopenda kuongea zaidi kuliko kutenda. Hili limeenea mpaka kwenye uongozi wa nchi. Nchi yetu inajengwa kwa maneno na kujisifia. Lakini kwa bahati nzuri (na mbaya kwetu) ni kuwa kuna kazi zinahitaji utendaji. Kama hujui, huwezi kufanya chochote au ukifanya matokeo yake yanakuwa hayana mvuto. Hapo ndipo programming inapoingia. Hata wewe unayejiita ni mwalimu sidhani kama una ujuzi wowote wa maana. Kama unao basi weka samples za kazi yako watu waone.
 
Nitaweka mkuu
 
Thread hii kila wiki mtu anakuja na remix yake, wabongo kwa kupenda kupondana na kushushana hatujambo, labda tengeneza App ya kuponda watu.
 
Wazo ni zuri.Swali ni Je nani atalipia Gharama za kuutengeneza?Je Ukishatengeneza Mfumo huo utaingizaje Pesa?Je umiliki na usimamizi wa mfumo husika pamoja na taarifa utakuwa chini ya nani?
 
Wazo ni zuri.Swali ni Je nani atalipia Gharama za kuutengeneza?Je Ukishatengeneza Mfumo huo utaingizaje Pesa?Je umiliki na usimamizi wa mfumo husika pamoja na taarifa utakuwa chini ya nani?
hapa mfumo huu mnunuzi ni serikali kwa maoni yangu
 
Nazani ni muhimu developer wa bongo kuwa na forum au team watano watano wanafanya kazi vijana wengi ukiwapa kazi wanakimbia kazi inakuwa inatia mashaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…