"Tanzania pulls out" ndio headlines ambazo huwapa raha Wabongo, pulling out, pulling out, pulling out, siku zote uwoga na kutokujiamini kwa lolote na popote.
Muwekeze kwenye elimu ili umma wa Tanzania uwe na uwezo wa kushindana na kuongoza, sio haya maisha ya mkisikia jina la Kenya mnababaika na kutetereka.
Wakenya tumewekeza kwenye nguvu kazi. Juzi kuna sehemu niliwaskia dada wa Kitanzania wakiongea wenyewe ofisini sehemu, halafu mmoja akasema "Hiyo ripoti imeandaliwa na Mkenya, chezea Wakenya wewe, wanajituma kweli".... Hawakujua mimi Mkenya, aisei nilihisi mzuka, nilihisi nipae kwa mabawa...yaani hadi raha....
Nafikiri hii picha hapa inaelezea kitu cha kujifunza kuhusu Kenya....