'Titicomb', uko sahihi kabisa, kwamba ile 4% ya IMF ulikuwa ni utabiri, na pia tarakimu walizokuwa wametoa serikali kwa wakati ule, pia ilikuwa ni utabiri; lakini tabiri zote mbili zilikuwa ni kwa mwaka mzima. Hii 7.2% ya sasa inayoripotiwa sio ya mwaka, ni ya kipindi (nadhani nusu mwaka, au robo?). Kwa hiyo tofauti ya kwanza ndio hiyo. Bado hatujui uchumi utakuwa kwa kiasi gani baada ya kuchakata namba zote za mwaka.
Huu ukuaji wa 7.2%, ni dalili nzuri, kama pasipojitokeza tatizo kubwa katika kipindi kilichosalia na kuiporomosha namba hiyo.
Lakini tofauti kubwa kati ya 4% ya IMF na hii 7.2% ya serikali, ambayo pengine ndiyo iliyosababisha mtafaruku kati ya pande hizo mbili ni njia iliyotumika kuikokotoa hiyo 7.2%. Inasemekana (mimi sijui), kwamba serikali iliamua kutumia njia tofauti na ile iliyotumika miaka yote katika kuipata asilimia ya ukuaji wa uchumi wetu. Kwa hiyo, hizi tarakimu mbili (kwa uelewa wangu) zimepatikana kwa kutumia njia tofauti zilizotoa namba mbili tofauti. IMF wameshikilia ile njia iliyotumika siku zote, Tanzania ikaamua kutumia njia mpya.
Hili si jambo geni. Rwanda na wao wamefanya hivyo hivyo.
Huu ndio uelewa wa jambo hili. Nipo tayari kusahihishwa kama sivyo hivyo.