Tanzania Q2 GDP growth rises to 7.2 pct v 6.1 pct

Ongelea na deni la Taifa wacha mapambio. Stability ya Currency in isolation siyo measure ya uchumi nzuri au unaokua lazima kuwa na interplay na macro economic factors zingine.
 
That is the crux of the matter.

Government's credibility on anything disappeared from that point, and they hardly disguise anything ever since, because they know only the gullible deadheads still believe anything coming from them. And, therefore, you see now, whatever they promise, people know it's a mirage!

For example who still believes there is going to be a fair and free election, 2019 and 2020!
 
Shukrani mkuu.
Nilitaka ufafanuzi tu na nimeupata mzuri sana toka kwako.
Mimi sijui chochote kuhusu uchumi, ni mweupe kabisa.
 
Kuhusu domestic consumption sichangii sina takwimu, kuhusu madeni ya ndani inabidi utufafanulie mfano yapi?

Kuhusu korosho hapo umepotea kidogo, serikali imeuza korosho nyingi kwenda nje(Vietnam kama sikosei) hivi karibuni na ndio maana umeonamkuu kafanya ziara kusini na ile mikwala ya wasio lipwa mawaziri na manaibu watoe ahadi kwenye mikutano ya hadharani lini watalipa.
huenda hizi nazo ndio zimepaisha uchumi Q2.

Kwenye sekta ya madini unakosea sana kuangalia sehemu moja tu ya mgogoro wa Acacia tena madini ya aina moja dhahabu.
Ukweli ni kuwa migodi ya dhahabu mingine kama GG ilikuwa operational, migodi ya almasi ilikuwa inaendelea, madini ya vito kama tanzanite makusanyo yalikuwa mazuri sana.
Kudhibitiwa kwa utoroshaji madini na kulazimishwa kuuzia ktk masoko maalum kumesaidi sana hata wachimbaji wadogo kuongeza pato loa taifa kwa kiasi kikubwa.

Yaliyo bakia nakuunga mkono kiasi kikubwa ingawa hujaweka takwimu hata moja umeongea hisia au mtazamo, namimi nimeiga kufanya hivyo hivyo kwa kiasi kikubwa.,
 
Shukrani mkuu.
Nilitaka ufafanuzi tu na nimeupata mzuri sana toka kwako.
Mimi sijui chochote kuhusu uchumi, ni mweupe kabisa.
Haaa! Umenichekesha sana. Huwezi kunishinda mimi!
Lakini subiri. Fani hii ya uchumi, kila mtu mwenye akili za kuvukia barabara ni 'mchumi.'

Kila siku tunashughulika na uchumi wetu binafsi majumbani mwetu, au sio?
 
Is just a nightmare, this dude won't leave the state house by a ballot box.
 
Kuhusu kutumia kikokotoo kipya serikali iko sahihi kwa 100%, hivi vikokotoo tunanvyoletewa haviendani na uhalisia wa nchi zetu za Afrika. Kwa mfano tuu, kwenye ujenzi, watu kila siku wanajenga nyumba lakini thamani ya soko la ujenzi halifahamiki na hivyo halijumuishwi kwenye GDP.

Wavuvi na wachimba madini wetu wadogo wadogo uzalishaji wao nao ulikuwa haujumuishwi kwenye vikokotoo. Sasa leo serikali imeweka mfumo mpya wa masoko ya kuuza madini ili kuweza kupata rekodi ya mauzo, na tunapata mpaka Tsh 2000m kutoka 160m kwa mwezi, sasa utaendeleaje kutumia kikokotoo cha zamani?

Kwenye nchi zao zilizoendelea teyari wanamifumo inayoangalia maendeleo ya ujenzi, kwa mfano, kwa kuangalia zip code tuu. Sisi mfumo huo hatuna, na kwa kutumia kikokotoo cha zamani, itaonesha Tanzania hatujengi nyumba (hamna real estate market), huoni hapo kuna tatizo?
 
Chamoto, hii ni hoja nzuri kabisa. Ninakubaliana nayo..., lakini...si kuna taratibu za kuyafanya mambo haya?

Na ninaelewa kwamba hiki kipimo cha ukuaji wa uchumi kwa kuangalia GDP ni swala lililokwishapigiwa kelele sana kila mahali duniani, na ndio sababu kukazuka vipimo mbalimbali katika kuangalia maendeleo ya wananchi. Sasa sijui kuna "Indexe(s)" na "indicators" ngapi duniani siku hizi.
Na katika yote hayo, ni katika kutafuta kipimo halisi zaidi kinachoonyesha maendeleo wanayoyapata wananchi wa kawaida.

GDP bado ni kipimo kinachotumika duniani kote, ikiwa ni pamoja na vipimo vingine vilivyobuniwa na vitakavyoendelea kubuniwa.
Vyote hivi vina taratibu na njia zake zilizokubaliwa zitumike kuzipata. Tatizo linajitokeza nchi moja ikaona taratibu hizo hazifai na ikaamua kufanya kwa kutumia njia zake, na matokeo ya ubunifu huo nchi hiyo ikaendelea kuyapa jina halali la GDP. Kwa maoni yangu, hapo hilo ni tatizo, pamoja na uzuri wa ubunifu huo.

Sasa sijui kama nimejieleza vizuri hapa ili kieleweke ninachojaribu kukiwasilisha.
 
Nimekuelewa vizuri sana kuhusu hoja yako ya kuona tatizo la kila nchi kujifanyia mambo kivyake. Hata hivyo kwa kikokotoo hicho hicho cha GDP bado kuna tatizo la ukusanyaji mzuri taarifa kwa nchi nyingi za Afrika.

Kwa Tanzania naona awamu ya tano imeanza kunakili aina mbalimbali za mapato (mf. vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo wadogo) ili ya jumuishwe kwenye pato zima la taifa. Tukiendelea kunakili hivi kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na kwenye ujenzi tutaweza kuipandisha GDP (hata kama ni kwenye karatasi) ambapo itavutia wawekezaji wa nje kuja kufanya FDI.
 
Mkuu ulizaliwa kupinga na utaendelea kupinga. Over!!
 
Na kwenye utalii Tanzania imekuwa ya 4 barani Afrika. Mapato ya serikali kutokana na biashara ya utalii yalifika karibu TShs trillion 6 mwaka 2018, kiasi kinachotosha kujenga SGR au lile bwawa la umeme la Stiglers gouge kule mto Rufiji.

Mkuu wapo watakaokuja kupinga na hili kwa singizio kibovu kabisa Cha kupika data.
Watu hatari sana hao kuwapatia Nafasi ya kuliongoza Taifa hili lenye uchumi unaokua kwa kasi nzuri.
 
Reactions: Dua
Tukifanikiwa kufanya hivi, tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana, na maendeleo yetu yataanza kuonekana kwa haraka. Kwa juhudi hizi nami nawapongeza wahusika.
 
Mkuu Kuna kundi kubwa Sana la vijana pale ufipani Ambao hawakumaliza hata kidato Cha nne,Wao wanajua kukua kwa uchumi wa Taifa Mpaka nyumbani kwao Wapate uhakika wa kula wali nyama kwa wiki nzima.
They can't distinguish between per capital income and National's GDP. What they know On economic rise up, is about Eating fresh and good foods. thus why they blame daily about these true datas concern with Economics.

Kwa Msaada tu kwa nyie vichwa maji mnaosema Ni data za kupikwa; China Ni Taifa Tajiri Namba Mbili Duniani lenye GDP ya kiwango Cha SGR lakini mpaka leo Kuna wachina wanaishi maisha duni Sana hasa wale walio maeneo ya Farm belts Richa ya utajiri na Maendeleo ya Taifa lao.
Kwa hiyo mnachotakiwa kuelewa Ni kuwa kuna kukua Uchumi wa mtu binafsi(per capital income) na pia kukua kwa Uchumi wa Taifa(National GDP income). Na Taarifa hii iliyotoka inahusu kukua kwa Uchumi wa Taifa la Tanzania na Wala siyo Uchumi wa Mtu mmoja mmoja(Mtanzania). Kuchanganya hivi vitu viwili kuwa kitu kimoja nikutaka kuibua hoja na ubishi wa kijinga tu usio kuwa na Maana.

Mfano, nchi za Uarabuni(United State Emirates) hazipo kwenye rank za juu Sana wa nchi Tajiri duniani lakini ukija kwa pato la mtu mmoja mmoja yaani per capital income ipo juu zaidi kuliko nchi nyingi hata zilizo top 5.

Kwahiyo wakuu Kama hutujui haya Mambo ya uchumi Ni Bora tuwe tunachangia hoja kwa kuomba msaada Wajuzi watujuze kuliko kuja na hoja zako za kupikapika kuonyesha jinsi gani usivyo jua Mambo.
 
Reactions: Dua
Ongelea na deni la Taifa wacha mapambio. Stability ya Currency in isolation siyo measure ya uchumi nzuri au unaokua lazima kuwa na interplay na macro economic factors zingine.

Mkuu kuna nchi inayodaiwa kama USA? Usiogope deni kukidhi maendeleo ya nchi, kazi ambayo inafanyika hivi sasa na JPM ni kubwa huwezi kuona matokeo leo lakini mwache amalize muda wake mtamkumbuka. FYI niambie nchi moja tu ambayo imeendelea bila kuwa na stability ya curreny yake? UK walimaliza kulipa deni la 1st world war few years ago after 2010. Hilo neno mapambio naona umekariri do your research kabla ya kuja kubwata bwata JF.
 

Maendeleo hayana Chama​
 
Hujui kitu wewe, unachojua ni kuweka bold font and blue colour kwenye sentensi. Nikikujibu nitakupa umaarufu. Nimeshindwa kuelewa hoja zangu unaniambia ninabwata?? Njoo na hoja usilete dharau.
 
Sijawahi kuamini katika GDP,utajiri wa watu wachache unagawanywa kwa umaskini wote then mtu anasema kipato kimekua
 
Hujui kitu wewe, unachojua ni kuweka bold font and blue colour kwenye sentensi. Nikikujibu nitakupa umaarufu. Nimeshindwa kuelewa hoja zangu unaniambia ninabwata?? Njoo na hoja usilete dharau.

Nije kutafuta umaarufu JF? Nicheke mie, kama hoja imekushinda kaa kimya. Narudia tena hakuna nchi yenye deni kubwa kama marekani. Tanzania bado deni letu ni dogo, if you know what I mean.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…