Hivi unajua, at times I strongly feel...Hii westphalian democracy tuliyoiga magharibi haitufai kabisa. Labda tutafute mkondo mwingine. Maana kama baada ya nusu karne we have failed to implement what we copied, sasa tufanyeje? Jiulize siku hizi viongozi wanaitisha uchaguzi kwa mbwembwe nyingi, incumbent wanaiba kura...kwa nguvu na baraka za vyombo vya dola...then wanakwambia njoo tuzungumzie power sharing! Kifupi ukaongee na kujadiliana na mbaya wako. Alianza Kibaki, kaja Mugabe who is next? Definetely hii trend itaendelea na hii aina ya "demokrasia" Inapata support sana kwa viongozi wa kiafrika "kwa ajili ya kuepusha maafa". sasa Mkuu wangu..where are we going kweli? MIMI NADHANI AFRICA INABIDI TURUDI KWENYE DRAWING BOARD.
We are neither democrats after six decades nor completely outcasts. Though we are heading in the hole.
Hapana mimi nadhani hii aina ya democrasia ya wenzetu inatupoteza. Masharti yake hatuyawezi! Kweli kabisa.
Mkuu Masanja,
Maneno yako mazito sana, na sina hata cha kuongeza maana hapo tupo ukurasa mmoja, mimi nguvu ziliiniisha sana kwenye mfano wa Chiluba, kwa sababu huyu alipokuwa kiongozi wa Unions za wachimba madini kule Zambia, he was so tough kwa Kaunda kwamba binafsi nilikuwa ninamuaminia sana kwamba atakuja kufanya maajabu, lakini baada ya aliyoyafanya ya hata kujaribu kujiongezea muda wa utawala uwe vipindi vitatu, basi nikakata tamaa na Africa kuhusu Demokrasia,
Demokrasia ya West sio ile original ya The Greeks, meaning kwamba hata The West nao waliipokea ile Greek's raw democracy na kui-modify ili ikidhi mahitaji yao ndio wakaweza kuwa na hii waliyonayo sasa, ambayo briefly ni a learned art yenye utamaduni wa kubadilika na set of qualities ambazo zina permeate na kujitengenezea njia za kujizawadia katika uhai wake. Na pia its values of inclusion, fairness and mutual accountability naturally infuse not only political life, but economic and cultural life as well. Halafu wananchi wana-set the rules ili ku-keep wealth continually circulating huku wakiukinga sana ili influence zake zisiwemo kwenye siasa, ingawa sio rahisi lakini wanajaribu hasa kwa kuwa on top katika kusimamia sheria zao, na ni hapa kwenye uzembe wa kusimamia sheria zao ndipo yamewakuta matatizo makubwa ya kiuchumi hivi karibuni, matatizo ambayo sisi Africa ni ya kawaida kwa sababu hatuzingatii sheria hata siku moja,
- Sasa kama The West wamezembea kidogo tu ku-regulate sheria zao za uchumi, yamewakuta makubwa namna hiyo imagine sisi ambao hatujawahi hata siku moja kusimamia sheria zetu kwa 100% tumekutwa na matatizo ya aina gani since our independence? Sasa nimeona wananchi wengi hapa wakilaani financial system hizo za West kutokana na matatizo yaliyowakumba sasa hivi, which I find to be out of touch with reality kwa sababu nilifkiri kwamba tunahitaji ku-celebrate capitalism kwa vile kwenye haya matatizo ya sasa imeonyesha ni kwa nini inatawala dunia nzima na itatawala kwa muda mrefu sana to come ni kwa kuwa ina a strong built in emergency system (ES) ambayo wakati wa good times ina-pump kodi isiyokuwa na mfano kwa serikali, ambayo wakati kama huu ndio inatakiwa kui-bail out kama vile US ambako serikali imetumia kodi karibu Dola Billioni 700, na UK karibu Dola Billioni 70 sasa kwa nini tusiheshimu kwamba hiyo system ya utawala inaweza kutoa hela zote hizo kuuuokoa uchumi wake yenyewe bila ku-collapse au kujipelekea to the ground!
Tizama Switzerland, wao pia walii-modify Demokrasia ili ikidhi mahitaji na matakwa yao as a nation, wao wakaamua kutokuwa na permanent president, kuna baraza la wawakilishi ambalo wajumbe hupokezana urais, ambao literally ni ceremonial position tu kwa ajili hasa ya ku-deal na international issues, lakini otherwise maamuzi yote ya taifa hufanywa collectivelly na baraza hilo la wawakilishi ambao huridhia only matakwa ya wananchi through referendums ambazo huko kwao ni kitu cha kawaida almost kila siku. It is good na it is working kwa mahitaji yao tu na unaweza kuiita anything lakini at heart ni modification ya demokrasia ambayo sisi Africa imetushinda kabisaa!
Africa, hata pa kuanzia na kuishia sijui ni wapi, ukiangalia kina Mugabe, Mbeki hawa ni viongozi walioingia wakakuta kila kitu in place kama inavyotakiwa, binadam mstaarabu siku zote huacha mahali alipoingia pakiwa pema kuliko alivyopakuta, sasa niambie utawaitaje hawa waa-Afrca wenzetu? Hawa ndio waliopaswa kuwa mfano wa kuigwa na Africa nzima lakini look what they did! Africa tumeruhusu ukabila, udini na utamaduni wa kizamani kuwa ndio our source of strength and wisdom katika kuongozana, mimi nawajua viongozi wengi katika taifa letu wanaoamini kuwa uongozi wao ni wa kupewa na Mungu, infact wengi wao wanaamini kuwa wao ni sometype of wafalme, kwa hiyo hata tabia zao ni za kifalme falme, I mean rais Nixon alipojiuzulu urais wa US kwa kuwa corrupted na a crook, aliliomba msamaha taifa lake tena sincererily, sio kama kina Lowassa, ambao ndio kwanza wanaenda "kujipokea wenyewe" kwenye majimbo yao ya ubunge, na mpaka leo hajatuomba radhi wananchi kwa kutulaza giza bila umeme, huku akichota Dola laki moja na nusu kila siku ya Mungu, ndio kwanza bado anadai ana haki zake kisheria kuwa eti hazikuheshimiwa,
Huko US kuna scientific studies zimewahi kufanywa ili kujua kwa nini among marais wengi wa huko in history, Nixon was the most corrupted kuliko wengine wote? Guess what? One study ingawa matokeo yake ni debatable, waligundua kua Nixon alikuwa anatokea kwenye background ya kimasikini sana kulinganisha na marais wengine wa taifa hilo kwa hiyo wakadai kuwa huenda hapo kuna relativism between umasikini na political corruption, sasa as much ninataka ku-argue against the finding ya hii study, mazingara ya uongozi wa Africa licha ya taifa langu Tanzania yananisuta sana kwenye hilo!
Ahsante Wakuu! na Mungu Aibariki Africa!