Baada ya kutafuna rasilimali za watanzania kwa ufisadi uliotukuka chini ya mbawa za Rais kikwete na familia yake, Ghalib S Mohamed Mwenyekiti wa kampuni ya Alosco inayomiliki makampuni mengine zaidi ya kumi ikiwemo Supermarket za Home Shopping Centre, sasa ndio ataongoza kamati ya ufundi ya wizi wa kura kuanzia tar 24 oktoba.
Ghalib akiwa pamoja na Faroukh Bagonza wa kampuni za mafuta ya TSN na Supermarket za TSN wame ratibu wizi wa kura kwa kuagiza masanduku yaliyo jaa makaratasi ya kupigia kura kutoka Msumbiji na vifaa vingine haramu vya kupigia kura ambavyo vimehifadhiwa kwenye Godauni (maghala) ya Faroukh Mtaa wa Gerezani, Mnazi moja.
Ghalib na Faroukh wakishirikiana na jangili mwenzao Abdulrahman Kinana wiki iliyopita wamenunua magari manne kutoka kampuni ya Toyota Tanzania Ltd iliyopo barabara ya Pugu. Magari hayo yatatumika kusafirisha makaratasi ya kura batili na kutumika kama magari feki ya wasimamizi wa kimataifa wa SADC. Mpango ni kupeleka gari mbili Zanzibar na mbili zitakuwa Tanzania Bara. Gari hizo aina ya Toyota Landcruiser Hardtop (2) zenye namba za usajili T 471 DFC na T 469 DFC zenye chasis namba TEEB71 90 - 7026583 na TEEB71 00 7026617. Pia wamenunua Toyota Hilux Double Cabin (2) zenye namba za usajili T 468 DFC na T 470 DFC zenye chasis namba AHTFR22G10 6105538 na AHTDR22G00 6105546.
Ghalib S Mohamed, fisadi na jangili ambae tangu rais Jakaya Kikwete aliposhika hatamu mwaka 2005, alipewa fursa za kufanya biashara bila kulipia ushuru bidhaa alizokuwa akiingiza nchini kwa ubia na familia ya Rais Jakaya Kikwete. Leo hii kupitia mianya hii ya kifisadi na unyonyaji wa jasho la watanzania, Ghalib ni moja kati ya matajiri wa kubwa Tanzania anae miliki Mali nyingi za kifahari, Majengo, Magari na biashara nyingi za nyuma ya pazia.
Ghalib ana miliki jumba lenye gharama ya bilioni 13 za kitanzania iliyo jengwa kwenye eneo la heka 11 huko Kinyerezi. Eneo hilo ambalo lilimefanya familia zaidi 33 kuhamishwa bila kibali maalum kwa ajili ya ujenzi wa jumba moja la mtu mmoja.
Ghalib huyu huyu ana miliki nyumba 4 Masaki na sasa ana malizia jumba lingine la kifahari mtaa wa Lincoln Masaki ambalo lina jengwa na wakandarasi kutoka china.
Ghalib ana miliki magari tofauti ya kifahari ikiwemo Rolls Royce, Bentley, Ferrari magari kadhaa aina ya Range Rover yenye thamani zaidi ya billioni 3 za kitanzania.
Kazi kubwa ya kifisadi ni ile ya usafirishaji bidhaa bila kulipa ushuru kupitia kampuni yake ya usafirishaji ya Silent Ocean inayosimamiwa na mdogo wake anaye itwa Salaah ambayo makao makuu yake yapo China. Salaah ambae kwa sasa amefanywa balozi mdogo wa Tanzania nchini China bila kuzingatia hiztoria yake ya uhalifu wa kutumia silaha na kutishia kuuwa watu kwenye kumbi tofauti za starehe, zaidi ya hapo salaah hana elimu wala historia ya kidiplomasia lakini uswahiba wa familia yao na JK umempa nafasi hii kubwa kabisa katika Taifa letu.
Leo hii Ghalib ndio nguzo kuu ya ufadhili wa CCM na familia za viongozi wa CCM. Kwa Lugha nyepesi, ghalib ndio anafanya mipango yote na mikakati ya CCM na Serikali iliyopo madarakani. Mkakati mkubwa alionao sasa ni huu wa kuartibu wizi wa kura ambao Ghalib na maswahiba wake wamemwaga pesa nyingi sana ili kufanikisha wizi mkubwa wa kura katika historia ya Taif hili wakijua dhahiri Magufuli hana asilimia 30 ya kura za Watanzania.