Tanzania sasa tuwe na siku tatu za kupumzika katika wiki moja

Mimi nina ushauri huu mapumziko yafutwe tufanye kazi siku zote, ushauri wa pili mapumziko yawe siku moja tu kila mmoja atachagua siku yake kutokana na imani ya dini yake
 
Mkuu Kakende,

Nadhani hakuna kitu kinachokera kama watu kufikiri kupumzika bila kuwa na sababu ya 'kupumzika', yaani watu wanafurahia hali ya kutowajibika (idle) kuliko kupumzika (rest) kiuhalisia.

Iwapo watu wanachelewa katika ofisi, then wanapokuta baadhi ya watu wakiwasubiri..wanaeaambia 'ofisi bado haijasafishwa'..wakimaliza "kusafisha" ofisi bado anakwambia wameenda 'kunywa chai'..then ndio aanze utaratibu wa kuwasikiliza wateja/wahudumiwa, tena huku akichat kutumia simu!

Bado muda si muda utaambiwa 'lunch time', mfano ukienda mchana katika ofisi nyingi(kutokana na uzembe na msongamano wa watu asubuhi) utaambiwa bado 'wanakula' kana kwamba wanakula mawe as their lunch.
Kurudi ofisini muda umeenda na bado watu wanachat ...muda si muda, ofisi hufungwa na watu huambiwa "kesho".

Hiyo ndiyo routine ya watenda kazi wengi hapa TZ, kuchelewa kazini, kuwahi kutoka kazini na kutotenda kazi kwa wajibu.

Maoni yangu, tuendelee na mfumo uliopo HIVI HIVI isiongezwe wala kupunguzwa kwa siku yeyote, hadi pale tutapojifunza uwajibikaji. Mfano mzuri kwa sisi WaKristo ni kuwa Biblia inasema, "siku sita fanya kazi, lakini siku ya Saba upumzike"..Sasa tutakuwa watu wa ajabu kutofanya kazi halafu "tupumzike".

What if kuwe na dini za kuanza kusali na kupumzika kuanzia jumapili hadi jumatatu(Yaani WIKI NZIMA), unataka kusema watu wasifanye kazi kwa kuwa watu wanasali na kupumzika?!..Kusali na kupumzika gani huko wakati watu wanatumia muda huo huo kufanya uovu?.

Tuache kutumia dini zetu kama visingizio(excuse).. Tuwajibike kwanza, So until then acha system iwe hivi hivi!
 
Last edited by a moderator:
Huo utakuwa ni upuuzi, dini zote zikidai siku ya mapumziko bado tuwe na siku za kufanyakazi siku 7 zitakuwa hazitoshi, sijui hapo tutasema katiba mpya iseme wiki iwe na siku kumi?
 
waislam mungu wetu ametutaka tuwe wachapa kazi,ndio sababu hatujawekewa siku yoyote kupumzika bali tumeambiwa=inaponadiwa kwa ajili ya sala nendeni upesi ktk ibada na mnapomaliza sala tawanyikeni ktk kutafuta riziki,kwa hiyo hakuna ajenda ya kupumzika kwa waislam,kwa hiyo kama kuna mwislam anataka kuwe na siku maalum ya kupumzika kama ilivyo kwa dini nyingine huyo haendi sawa na mwongozo wa dini yetu tukufu,tusiige kila kitu nduguzanguni.

wenye masikio watakuwa wamesikia!
 
hebu chukua tano kwanza,una akili sana!
 
Mkuu Kakende,

Nadhani hakuna kitu kinachokera kama watu kufikiri kupumzika bila kuwa na sababu ya 'kupumzika', yaani watu wanafurahia hali ya kutowajibika (idle) kuliko kupumzika (rest) kiuhalisia.

Iwapo watu wanachelewa katika ofisi, then wanapokuta baadhi ya watu wakiwasubiri..wanaeaambia 'ofisi bado haijasafishwa'..wakimaliza "kusafisha" ofisi bado anakwambia wameenda 'kunywa chai'..then ndio aanze utaratibu wa kuwasikiliza wateja/wahudumiwa, tena huku akichat kutumia simu!

Bado muda si muda utaambiwa 'lunch time', mfano ukienda mchana katika ofisi nyingi(kutokana na uzembe na msongamano wa watu asubuhi) utaambiwa bado 'wanakula' kana kwamba wanakula mawe as their lunch.
Kurudi ofisini muda umeenda na bado watu wanachat ...muda si muda, ofisi hufungwa na watu huambiwa "kesho".

Hiyo ndiyo routine ya watenda kazi wengi hapa TZ, kuchelewa kazini, kuwahi kutoka kazini na kutotenda kazi kwa wajibu.

Maoni yangu, tuendelee na mfumo uliopo HIVI HIVI isiongezwe wala kupunguzwa kwa siku yeyote, hadi pale tutapojifunza uwajibikaji. Mfano mzuri kwa sisi WaKristo ni kuwa Biblia inasema, "siku sita fanya kazi, lakini siku ya Saba upumzike"..Sasa tutakuwa watu wa ajabu kutofanya kazi halafu "tupumzike".

What if kuwe na dini za kuanza kusali na kupumzika kuanzia jumapili hadi jumatatu(Yaani WIKI NZIMA), unataka kusema watu wasifanye kazi kwa kuwa watu wanasali na kupumzika?!..Kusali na kupumzika gani huko wakati watu wanatumia muda huo huo kufanya uovu?.

Tuache kutumia dini zetu kama visingizio(excuse).. Tuwajibike kwanza, So until then acha system iwe hivi hivi!

Strong point
 
Wakati wa uongozi wa mwalimu Nyerere tulikuwa tunafanya kazi siku ya Jsi mpaka saa 6.30 akajaondoa Mwinyi Jsi ikawa kulala na sikukuu ikiangukia Jsi au J2 inafidiwa. Ieleweke kuwa Jsi haikuwekwa kwa ajili ya wasabato bali mzee Ruksa alitaka wafanyakazi wapate muda wa kujiongezea kipato kwa kwenda mashambani. Sasa tukitaka kupumzika tena Ijumaa itakuwa kasheshe. Mimi nafikiri waislamu waruhusiwe kufanya kazi nusu siku siku ya Ijumaa ili kuondoa utata.
 
Huo utakuwa ni upuuzi, dini zote zikidai siku ya mapumziko bado tuwe na siku za kufanyakazi siku 7 zitakuwa hazitoshi, sijui hapo tutasema katiba mpya iseme wiki iwe na siku kumi?

Kuna sms moja niliisoma weekend hii iliyopita inasema kuwa ''Watanzania ni wavivu. Wevi wawili waliiba pesa benki walipofika ghetto mwenzake kamwambia tuhesabu kwanza tujue tumeiba kiasi gani. Mwizi mwenza mvivu kasema nimechoka tulale kesho asubuhi watatangaza ni kiasi gani kimeibiwa tutapata jibu''.
 
Tangu mchakato wa kutoa maoni uanze, baadhi ya watanzania kwa kupitia Radio fulani pia makongamano mbalimbali ya katiba wanapenda sasa nchi iwe na siku tatu za kupumzika hili pia waislam nao wapate nafasi ya ibada ili iwe haki sawa. Siku ya Ijumaa (Waislam), Jumamosi (Wasabato), Jumapili( Madhehebu mengine ya Kikristu) Nchi kama Saudi arabia mapumziko yao ni Alhamis na Ijumaa, Nchi za Ulaya Mapumziko yao ni Jumamosi na Jumapili. Hapa kwetu ni Jumamosi na Jumapili. Sina uhakika kama Jumapili na Jumamosi zipo kwenye Katiba ya sasa au ni mfumo tulio urithi kwa wakoloni. Mimi binafsi naona kama siku ya mapumziko itaanzia Ijumaa basi tutakuwa tumeweka rekodi ya dunia kwe kurest. We unasemaje?

Mapumziko ni jumamosi na jumapili tu. Tukitaka kumridhisha kila mtu kuna watu watajitokeza na kusema kuwa wao wanasali Jumatatu hivyo tuwe na siku nne za mapumziko.
 
Hebu wasitufanye sote kuwa wavivu.Tujiulize kwanza Haki tunayoidai hapo ni ipi na kwa misingi ipi?Na je itawezekana kweli kumridhisha kila mwananchi iwapo atadai haki yake?Sisi ni masikini,twpaswa kuongeza siku za kufanya kazi badala ya kupunguza.Tutakuwa taifa la watu wavivu za ya tulivyo sasa.
 
Tukumbushane. Tanzania tulikuwa tunafanya kazi Jumatatu hadi Jumamosi. Jumatatu kuanzia saa 1.30 hadi 8.30 na Jumamosi 1.30 hadi 6.30. Mzee Mwinyi akabadili kwamba kazi iwe Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 1.30 hadi 9.30. Masaa yaliongezwa ili kufidia yale ya Jumamosi.

Madhumuni ya kuweka Jumamosi siku ya mapumziko ilikuwa wafanyakazi wapate nafasi ya kufanya kazi ili wajiongezee kipato. Hii, kwa mujibu wa Mzee Mwinyi, ni kwa sababu mishahara ilikuwa hiwatoshi wafanyakazi. Jumamosi haikuwa siku ya mapumziko kwa sababu ya Wasabato Huu ni upotoshaji

Wislam kudai siku ya Ijumaa iwe ya mapumziko sijui wanaitoa wapi katika Qoran. Nijuavyo mimi ni kuwa waislam wanatakiwa kwenda kufanya kazi baada ya kusali. Nitafurahi kuambiwa Aya ambayo inawataka kupumzika. Kusema Uarabuni au Ujerman na siku nzao za kupumzika zinatuhusu nini.
 
Hivi tumejishughulisha kujua ni kwa nini serikali iliamua jmosi na jpili kuwa mapumziko au tunakisia tu kuwa sababu ni za kidini?
 
Hatupaswi kuwa wavivu kiasi hicho wanaoabudu ijm wapewe ruhusa ya kuabudu wengine wachape kazi,hizo siku tano za kazi hazitoshi,chapa kaaazii!
 
Maoni yangu, tuendelee na mfumo uliopo HIVI HIVI isiongezwe wala kupunguzwa kwa siku yeyote, hadi pale tutapojifunza uwajibikaji. Mfano mzuri kwa sisi WaKristo ni kuwa Biblia inasema, "siku sita fanya kazi, lakini siku ya Saba upumzike"..Sasa tutakuwa watu wa ajabu kutofanya kazi halafu "tupumzike".
Well, kama biblia inasema "siku sita fanya kazi siku ya saba pumzika..." ni kwa nini Wakristo wanaanza kupumzika siku ya sita (Jumamosi)??
 
umesahau siku ya wapagani kwani nao husali hata chini ya mti, nayo inatakiwa iwe ya kupumzika.
 
Well, kama biblia inasema "siku sita fanya kazi siku ya saba pumzika..." ni kwa nini Wakristo wanaanza kupumzika siku ya sita (Jumamosi)??

Mkuu, it is siku sita kufanya kazi ili kwa hiyo siku moja upumzike...Emphasis being on the day of rest not the day of work!

Pili, it tells more about rest(Rest in the Lord) si kupumzika eti kustarehe, bali being more closer to your CREATOR.
 
Back
Top Bottom