Tanzania sasa tuwe na siku tatu za kupumzika katika wiki moja

Tanzania sasa tuwe na siku tatu za kupumzika katika wiki moja

Minaunga mkono wanaosama mzigo upigwe wiki nzima hakuna mapumziko ila iwe huru kuwa mtu atakapoona mda wa ibada kwa dini yake umeingia basi rukhsa akaabudu kuliko ilivyo sasa ni dini moja2 enye kupewa siku mbil kwenda kuabudu hakika huo ni upendeleo, ndio maana waelevu tuna pinga hoja kua serkali haina dini
 
Well, kama biblia inasema "siku sita fanya kazi siku ya saba pumzika..." ni kwa nini Wakristo wanaanza kupumzika siku ya sita (Jumamosi)??

Usipotoshe maandiko. Siku ya saba ni Jumamosi peke yake, Jumapili ni siku ya kwanza ya juma, soma Luka 23:54-56 na Luka 24:1 utagundua kuwa Yesu alisulubiwa Ijumaa siku ya maandalio na alifufuka Jumapili siku ya kwanza ya juma. Biblia na Quran vyote vinaitambua Sabato hebu soma Kut. 20:8-11 na Quran 2:65 uone maagizo ya Mungu. Fanyeni vyovyote vile sisi tutaendelea kuitunza Sabato hata kufa. Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.
 
Mkuu labda ungeziita siku za kuabudu lol.. Kama huwa lengo lake kubwa ni kuabudu na si kupumzika.

But its sound so awkward!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mkuu, it is siku sita kufanya kazi ili kwa hiyo siku moja upumzike...Emphasis being on the day of rest not the day of work!

Pili, it tells more about rest(Rest in the Lord) si kupumzika eti kustarehe, bali being more closer to your CREATOR.

Usipotoshe maandiko. Siku ya saba ni Jumamosi peke yake, Jumapili ni siku ya kwanza ya juma, soma Luka 23:54-56 na Luka 24:1 utagundua kuwa Yesu alisulubiwa Ijumaa siku ya maandalio na alifufuka Jumapili siku ya kwanza ya juma. Biblia na Quran vyote vinaitambua Sabato hebu soma Kut. 20:8-11 na Quran 2:65 uone maagizo ya Mungu. Fanyeni vyovyote vile sisi tutaendelea kuitunza Sabato hata kufa. Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu.
Kwa nini Wakristo wanapata siku mbili kwa wiki za kupumzika na kuabudu, Jumamosi na Jumapili, wakati Waislamu hawapati hata siku moja?
 
Kwa utawala wa Sultani yote yanawezekana!!
 
Kwa nini Wakristo wanapata siku mbili kwa wiki za kupumzika na kuabudu, Jumamosi na Jumapili, wakati Waislamu hawapati hata siku moja?

Mkuu Anheuser, nadhani bado hatujaelewana vyema.. point yako hasa ni ipi?

Unataka kusema siku ya Jumamosi naJumapili "weekend" ni mapumziko kwa wakristo na siku za kazi kwa waislamu?

Pili kusema, "waislamu hawapati hata siku moja ya kupumzika" hebu thibitisha wapi katika ofisi ya Serikali au Taasisi/Shirika/Kampuni binafsi ambapo waislamu wanakwenda siku saba za wiki kazini na wakristo wakipumzika(while waislamu) wakiwa kazini.

Kuna tofauti kati ya siku ya kuabudu na siku za mapumziko za wiki!
 
Last edited by a moderator:
sisi kwetu alhamisi

tunaenda kutambika hatufanyi kazi..hivyo napendekeza mapumuziko yaanze alhamis haki sawa.!
 
Mkuu Anheuser, nadhani bado hatujaelewana vyema.. point yako hasa ni ipi?

Unataka kusema siku ya Jumamosi naJumapili "weekend" ni mapumziko kwa wakristo na siku za kazi kwa waislamu?

Pili kusema, "waislamu hawapati hata siku moja ya kupumzika" hebu thibitisha wapi katika ofisi ya Serikali au Taasisi/Shirika/Kampuni binafsi ambapo waislamu wanakwenda siku saba za wiki kazini na wakristo wakipumzika(while waislamu) wakiwa kazini.

Kuna tofauti kati ya siku ya kuabudu na siku za mapumziko za wiki!
Natafuta jinsi ya kurekebisha ama kurahisisha swali langu sipati, hakuna jinsi ya ku rephrase swali langu tofauti sana.

Jumamosi na Jumapili ni siku za kuabudu kwa Wakristo, milango ya madhabahu imefunguliwa, na ni siku zao za kupumzika, milango ya serikali na makampuni officially imefungwa. Waislam hawana siku hata moja ambayo milango ya maofisi imefungwa, milango ya madhabahu imefunguliwa.

Kwa nini?

Kwa nini unatetea status quo, hali ibaki hivyo hivyo, wakati Wakristo wana siku mbili kwa juma, Waislam hawana hata siku moja ya kupumzika na kuabudu?
 
Mkuu Anheuser,

Nijuavyo mimi siku za mapumziko, kuabudu hutegemeana na utaifa, yaani muundo wa kikatiba, muundo wa kikanuni na utaratibu.

Mf. Nchi za 'kiislam' Jordan kwa mfano, kuanzia siku ya ijumaa ni mapumziko.Tena ijumaa muda wa mchana(ingawa huswali muda wote.) huwa siku ya kuabudu!

Nchi za 'Kikristo'..mf. Italy..siku ya jumapili ni muujiza maduka kuwa wazi!

Kwa nchi zisizo na kuegemea sana udini lakini kwa kutambua umuhimu wa dini mbalimbali kwa faisa ya wananchi wake!Siku ya mwisho wa juma(Jumamosi) na siku ya kwanza ya juma(jumapili) huwa siku za mapumziko!Mf. US(baadhi ya majimbo), Tanzania na nchi nyingi za Afrika kwa ujumla.

Sidhani kama ni sawa kusema kuwa wakristo 'wanapendelewa' ..maana si watu wote walio katika ofisi wasio waislamu kuwa ni wakristo, Mkuu.

Ila kama Quran nayo pia yataka kupumzika siku ya ijumaa kama itakavyo kwa siku ya Saba kwa wakristo ni vizuri tukaweka mawazo haya kikatiba mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Ila kama Quran nayo pia yataka kupumzika siku ya ijumaa kama itakavyo kwa siku ya Saba kwa wakristo ni vizuri tukaweka mawazo haya kikatiba mkuu.
Anhaa, okay, basi yaishe, maana umebadili msimamo wako, mwanzoni ulisema unataka mambo yabakie hivi hivi yalivyo.

Hippocratessocrates: "Maoni yangu, tuendelee na mfumo uliopo HIVI HIVI isiongezwe wala kupunguzwa kwa siku yeyote..."

Kitu ambacho kinaleta utata na misuguano ya kidini. Wakristo wanapata siku mbili za kupumzika na kuabudu, Jumamosi na Jumapili, Waislam hawapati hata siku moja, mfumo umelalia upande mmoja.
 
Kwa nini Wakristo wanapata siku mbili kwa wiki za kupumzika na kuabudu, Jumamosi na Jumapili, wakati Waislamu hawapati hata siku moja?

Mkuu Waislam wanayo siku ya mapumziko ambayo ni Sabato yaani Jumamosi hebu soma Quran 2:65 linganisha na Kut. 20:8-11 na Isa. 66:22-24 neno la Mungu liko wazi, utata unatoka wapi?
 
Mkuu Waislam wanayo siku ya mapumziko ambayo ni Sabato yaani Jumamosi hebu soma Quran 2:65 linganisha na Kut. 20:8-11 na Isa. 66:22-24 neno la Mungu liko wazi, utata unatoka wapi?
Sawa, wanayo siku ya kupumzika, Jumamosi, lakini hawaabudu Jumamosi, hivyo hawana siku ya kupumzika na kuabudu. Wakristo wanazo mbili, Jumamosi na Jumapili, Waislamu hawana hata moja.

Ni haki hiyo?
 
Mkuu, it is siku sita kufanya kazi ili kwa hiyo siku moja upumzike...Emphasis being on the day of rest not the day of work!

Pili, it tells more about rest(Rest in the Lord) si kupumzika eti kustarehe, bali being more closer to your CREATOR.

Kwa muktadha wa neno siku sita kama lilivyotumika katika maandiko ya biblia,haikuwa maana ya siku hizi za kuzama na kuchomoza kwa jua.

Ukitaka kujua soma tena maandiko siku ya kwanza kiliumbwa nini? Alafu jiulize jua ambalo ndio kigezo cha kupata usiku na mchana lilishaumbwa?
 
Ndugu, what's your point?...Ilimaanisha nini kwa kusema siku sita? au bi siku sita zipi hizo unazozifahamu wewe?
 
Back
Top Bottom