nikipewa hii nchi nafuta dini zote za kigeni nyambaf...
Kupumzika baada ya kufanya nini?
waislam mungu wetu ametutaka tuwe wachapa kazi,ndio sababu hatujawekewa siku yoyote kupumzika bali tumeambiwa=inaponadiwa kwa ajili ya sala nendeni upesi ktk ibada na mnapomaliza sala tawanyikeni ktk kutafuta riziki,kwa hiyo hakuna ajenda ya kupumzika kwa waislam,kwa hiyo kama kuna mwislam anataka kuwe na siku maalum ya kupumzika kama ilivyo kwa dini nyingine huyo haendi sawa na mwongozo wa dini yetu tukufu,tusiige kila kitu nduguzanguni.
waislam mungu wetu ametutaka tuwe wachapa kazi,ndio sababu hatujawekewa siku yoyote kupumzika bali tumeambiwa=inaponadiwa kwa ajili ya sala nendeni upesi ktk ibada na mnapomaliza sala tawanyikeni ktk kutafuta riziki,kwa hiyo hakuna ajenda ya kupumzika kwa waislam,kwa hiyo kama kuna mwislam anataka kuwe na siku maalum ya kupumzika kama ilivyo kwa dini nyingine huyo haendi sawa na mwongozo wa dini yetu tukufu,tusiige kila kitu nduguzanguni.
Jehova witness huwa tunsasali Jumatatu na Jumatano na zenyewe zifikiriwe kuwa za mapumziko
Mkuu Kakende,
Nadhani hakuna kitu kinachokera kama watu kufikiri kupumzika bila kuwa na sababu ya 'kupumzika', yaani watu wanafurahia hali ya kutowajibika (idle) kuliko kupumzika (rest) kiuhalisia.
Iwapo watu wanachelewa katika ofisi, then wanapokuta baadhi ya watu wakiwasubiri..wanaeaambia 'ofisi bado haijasafishwa'..wakimaliza "kusafisha" ofisi bado anakwambia wameenda 'kunywa chai'..then ndio aanze utaratibu wa kuwasikiliza wateja/wahudumiwa, tena huku akichat kutumia simu!
Bado muda si muda utaambiwa 'lunch time', mfano ukienda mchana katika ofisi nyingi(kutokana na uzembe na msongamano wa watu asubuhi) utaambiwa bado 'wanakula' kana kwamba wanakula mawe as their lunch.
Kurudi ofisini muda umeenda na bado watu wanachat ...muda si muda, ofisi hufungwa na watu huambiwa "kesho".
Hiyo ndiyo routine ya watenda kazi wengi hapa TZ, kuchelewa kazini, kuwahi kutoka kazini na kutotenda kazi kwa wajibu.
Maoni yangu, tuendelee na mfumo uliopo HIVI HIVI isiongezwe wala kupunguzwa kwa siku yeyote, hadi pale tutapojifunza uwajibikaji. Mfano mzuri kwa sisi WaKristo ni kuwa Biblia inasema, "siku sita fanya kazi, lakini siku ya Saba upumzike"..Sasa tutakuwa watu wa ajabu kutofanya kazi halafu "tupumzike".
What if kuwe na dini za kuanza kusali na kupumzika kuanzia jumapili hadi jumatatu(Yaani WIKI NZIMA), unataka kusema watu wasifanye kazi kwa kuwa watu wanasali na kupumzika?!..Kusali na kupumzika gani huko wakati watu wanatumia muda huo huo kufanya uovu?.
Tuache kutumia dini zetu kama visingizio(excuse).. Tuwajibike kwanza, So until then acha system iwe hivi hivi!
Huo utakuwa ni upuuzi, dini zote zikidai siku ya mapumziko bado tuwe na siku za kufanyakazi siku 7 zitakuwa hazitoshi, sijui hapo tutasema katiba mpya iseme wiki iwe na siku kumi?
Tangu mchakato wa kutoa maoni uanze, baadhi ya watanzania kwa kupitia Radio fulani pia makongamano mbalimbali ya katiba wanapenda sasa nchi iwe na siku tatu za kupumzika hili pia waislam nao wapate nafasi ya ibada ili iwe haki sawa. Siku ya Ijumaa (Waislam), Jumamosi (Wasabato), Jumapili( Madhehebu mengine ya Kikristu) Nchi kama Saudi arabia mapumziko yao ni Alhamis na Ijumaa, Nchi za Ulaya Mapumziko yao ni Jumamosi na Jumapili. Hapa kwetu ni Jumamosi na Jumapili. Sina uhakika kama Jumapili na Jumamosi zipo kwenye Katiba ya sasa au ni mfumo tulio urithi kwa wakoloni. Mimi binafsi naona kama siku ya mapumziko itaanzia Ijumaa basi tutakuwa tumeweka rekodi ya dunia kwe kurest. We unasemaje?
maskini unatamani vipi kupumzika....khaa
Well, kama biblia inasema "siku sita fanya kazi siku ya saba pumzika..." ni kwa nini Wakristo wanaanza kupumzika siku ya sita (Jumamosi)??Maoni yangu, tuendelee na mfumo uliopo HIVI HIVI isiongezwe wala kupunguzwa kwa siku yeyote, hadi pale tutapojifunza uwajibikaji. Mfano mzuri kwa sisi WaKristo ni kuwa Biblia inasema, "siku sita fanya kazi, lakini siku ya Saba upumzike"..Sasa tutakuwa watu wa ajabu kutofanya kazi halafu "tupumzike".
Well, kama biblia inasema "siku sita fanya kazi siku ya saba pumzika..." ni kwa nini Wakristo wanaanza kupumzika siku ya sita (Jumamosi)??