Tanzania "Shamba la bibi" hadi lini? Hii Ruby ni yetu. Iweje iko sokoni Dubai na serikali yetu haijui? Nasaidia, mchimbaji huyu, anzieni hapa!

Magufuli alipojaribu kuwabinya hawa wahuni mkamuita dikteta.

Haya, faidini matunda ya DEMOKRASIA!

Hii ndio DEMOKRASIA NA UTAWALA BORA Chini ya Jemedari Chui Jike.
Kuwadhibiti ni kuweka uhuru wa soko huku serikali ikikusanya Kodi kwa uwazi.
Kujenga ukuta, kuweka urasimu kunaongeza utoroshaji kupitia wachache wenye nafasi.
Uwazi na elimu kwa raia ili wapambane sokoni ndiyo demokrasia na utawala Bora.
 
Nimesema once na ninasema tena, kama hii kitu ni fake na overvalued tungepiga kimya tu..., sababu inatutangaza zaidi hata ya Royal Tour..., Hapa tungepiga mwendo tu wa no comment....

Kwahio naweza kusema shukrani zimuendekee jamaa aliyegushi bei ya hio Ruby
 
Lazima lilipiwe Kodi, je limelipiwa Kodi? Sheria ya madini hairuhusu madini kusafirishwa nje isipokua Kwa Kibali maalum kutoka kwenye Mamlaka husika je lilikatiwa Kibali?
 
Kumevunjwa sheria ipi, si anaruhusiwa kuuza jiwe ? Nadhani tukianzia hapo tutaweza kupata wapi kuelekeza nguvu. Unajua wenzetu kwa mfano wale walio na mafuta, hufanywa kama ni mali ya taifa. Labda concept kama ile ya ardhi mali ya serekali, sababu zake hazitofautiani sana na hizi za madini.
 
Anapaswa Kulipia Kodi, lakini pia Sheria za madini haziruhusu jiwe kutoka nchini bila Kibali maalum Cha Mamlaka
 
Paschal hii si level ya mijadala yetu! Mijadala yetu ni Mama anaupiga mwingi,Vijana wanakosa pesa za kununulia mapenzi,Wanaume wa Rukwa wameshindwa kukata viuno sababu ya bumps, Sukuma Gang vs Msoga Gang!
Hiyo ndo mijadala yetu!
Mawe ya ruby mbona tunayo mengi tu! Yaani Waziri au Serikali yetu ikae kufuatilia Jiwe la kilo 2!?
Hao ni Matapeli wanataka kupiga watu huko ndo maana wanasubiri mwezi mtukufu (Ramadan) upite. Kama ni halali kwa nini wasifanye mnada leo au kesho?
Dola milioni 120 ($ 120 million) si mchezo, kuna harufu ya utapeli hapo!
 
Kuwadhibiti ni kuweka uhuru wa soko huku serikali ikikusanya Kodi kwa uwazi.
Kujenga ukuta, kuweka urasimu kunaongeza utoroshaji kupitia wachache wenye nafasi.
Uwazi na elimu kwa raia ili wapambane sokoni ndiyo demokrasia na utawala Bora.
Ona jizi lingine hili!

Ptuuuuu! Mukundi wambwaa!
 
Uhuni tu hapo hamna jiwe LA thamani hiyo,dhahabu tu 1Kg ni $ 50,000 sasa ruby ndio itauzwa bill hizo 240 kwa 2.8Kg??

ruby iko juu kuliko Gold na upatikanaji wake ni sio kiviile...gold ina promo sana duniani lakini yapo madini yana thamani kuliko gold...

ila kuipata hiyo 1kg ya ruby ni mziki..
 
Naamini kwamba zipo nyingine nyingi sana zinazofanana, kama serikali kweli inayo nia basi ifanyie utafiti kufahamu madini yote yaliyotoroshwa nchini. Kuna wakati India ilikuwa inauza Tanzanite nyingi kuliko Tz including nchi jirani, je wameshayafanyie kazi hayo? Huyu mtu aliyelitangaza hilo jiwe la Ruby waziwazi nadhani ana kusudi la wazi kabisa. Kwani alilazimishwa kuelezea madini yalikotokea?
 
kyee kyeee kyeee huu Ndio ukweli mchungu ambayo hao wazalendo uchwara wanauimba yaani uteseke wewe Halafu mjinga Mmoja aje akupangie matumizi,yaani hapa nawaza Siku nipate jiwe Halafu kenge Mmoja wa kijani aje
Nyee! nyeee! Nyeee!
Nalichekea na kulichangamkia likiingia kingi nalipa kinywaji chenye slow killer tunagonga grass na cheer nalipa mgao wake then baada ya mwezi tunazika jitu
Pumbafu kabisa hii nchi Ina wachumia tumbo wanaojali mavitambi Yao Kwa deals haramu huku yakiwafukarisha wavuja jasho'.
Kiama chaja!
 
ruby iko juu kuliko Gold na upatikanaji wake ni sio kiviile...gold ina promo sana duniani lakini yapo madini yana thamani kuliko gold...

ila kuipata hiyo 1kg ya ruby ni mziki..
Hajui kitu gold gram haizidi laki moja na nusu ruby kiwango kwa gram haipungui milion 5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…