Tanzania "Shamba la bibi" hadi lini? Hii Ruby ni yetu. Iweje iko sokoni Dubai na serikali yetu haijui? Nasaidia, mchimbaji huyu, anzieni hapa!

Maadam wewe ni mtetezi wa CCM na watawala wake,huna haki ya kulalamikia wala kuhoji mambo haya.

Insanity is doing the same thing over and over again and expecting different results-Albert Einstein.
Huyu jamaa huwa anatetea sana serikali na Chama chake Cha CCM, leo amewageuka!
 
Mahenge Matombo udongo tofauti!
 
Dunia ina umafia mwingi saaana..

Biashara ya madini inamilikiwa na cartels fulani ambazo zina matawi kila mahala na zipo kuhakikisha maslahi ya mabwanyenye yanastawi.. Kudeal na huu umafia kunahitaji akili kubwa zaidi ya hizi akili za kina Joti na Mpoki...

DRC ni nchi kubwa sana yenye madini kila mahala lakini ukiwa pale Lubumbashi aka Katanga province utakuta raia wana njaa na umasikini japo huko polini mamafia wa dunia wanakamua watakavyo midege ikitua na kuruka
Kifupi nchi imetekwa na wahuni ndio wanaimiliki.

Tanzania iko mikononi mwa wahuni toka enzi za uhuru, madalali wa hao wahuni tuko nao tunaishi nao na wengine tunaamini kama ndugu zetu but they are here purposely, Kupitia hao madalali ndio hata uongozi wa juu na maeneo nyeti wanapatikana watu.... Kuvuka hiki kikwazo na kuukata mnyororo wa wahuni huhitaji demokrasia bali unahitaji kiburi, unyama, kutojali na ukatili mwingi, ukiwavuruga ndipo utapata nafasi ya kuset na kuokoa maslahi ya Taifa...

Watanzania kwa kupenda maisha mazuri mepesi wamegeuka maagent wa cartels na kusaidia ustawi wao pale penye ugumu, Cartels hizi zimejipenyeza Kanisani, misikitini, Kwenye vyama vya siasa na kila penye influence ili kulinda maslahi yao kila yanapoingiliwa..
 
Magufuli alijitoa sana kulinda raslimali za nchi, kulikuwa na ulinzi na utaratibu Kwa wachimbaji, wachimbaji walichimba , kulikuwa na maafisa wa madini na TRA katika sehemu mpya au za zamani ambapo wachimbaji wanafanya shughuli zao, mali ikipatikana itajulikana Kwa maafisa wote wa madini , TRA , itapimwa na mchimbaji kupewa kibali Cha kwenda kuuza Mali yake katika masoko ya ndani yaliyopo, hivyo mchimbaji ataandamana na hao maafisa wa pande mbili.

Akifika sokoni wanunuzi wengi hutaka kununua mali hiyo kulingana na soko au bei iliyopo kwenye soko la dunia Kwa siku hiyo, mnunuzi akipatikana Mali itapimwa kuji ridhisha na kuona kiwango tajwa kutoka maafisa wa madini ni sahihi? Kama ni sahihi basi ana mlipa muuzaji na muamala wa serikali ana kusanya pesa hiyo ana ilipa TRA, utaratibu ambao ulikuwa mzuri sana, uliondoa usumbufu na kutoa soko huru Kwa wachimbaji, hivyo wachimbaji wali hamasika.

Hata kama ikitokea hakuna wanunuzi kulingana na kiwango kikubwa Cha pesa, serikali iikuwa na utaratibu wa kununua, mfano ni zile kilo za tanzanite zilizopatikana Kwa yule mmasai (Laizer), hivyo wanunuzi wa nje walikuja nchini na kujisali kama wanunuzi na kupewa license ya kununua na kuuza popote duniani.

Baada ya Mama kuingia akasema hatua hizo sio sahihi , Zina kimbiza wafanya biashara, aka ruhusu wanunuzi waje kiholela wanunue popote na mahali kokote, tuna fungua nchi, ndio maana madini hyafiki tena katika masoko yaliyowekwa, wanunuzi wanaenda kule kule shimoni/porini/ machimboni na kusubili mali huko na kufanya biashara kule kule na kutorosha mali, hakuna tena TRA, maafisa madini au usalama wa taifa kule, wote wako maofsini maana agenda ni kufungua nchi, tulambe hasari.

Hii nchi binafsi nafikiri siasa Ina zipeleka pabaya, Magufuli alijitahidi sana ila baada ya kumtia moyo tukimwita majina yote mabaya, ana kimbiza wawekezaji, muuaji, hapendi mataraji, Leo tuna pigwa jiwe la bil zaidi ya 250 lakini utasikia time kimbilia world bank, EU, USAID au china kuomba misaada, ni taifa ambalo mindset zetu ni kuomba omba, kiongozi wa nchi lazima uwe extraordinary na kuachana na tabia za kufanya basic things, hatuwezi kuwa taifa Imara Kwa viongozi kufanya vitu vya kawaida ambavyo mtu yeyote anaweza fanya.
 

Waziri husika ajihuzuru
 
Tulipaswa kuelezwa lilichimbwa lini na kuuzwa lini?

Yote kwa yote, CCM ni ile ile, hakuna kipya. Karibu wote ni wezi na hawana mpango wa kuacha wizi.
 
alikuwa mwizi kama wanasiasa wenzie walivyo wezi ila bado haiondoi ukweli ni mmoja wa ma Rais wachapakazi kuwahi kutokea nchini

kama huamini report ya Ukaguzi wa Mkaguzi mkuu wa Serikali alieteuliwa na yeye mwenyewe unataka nikiwekee ushahidi wa picha wakati anaiba ? gharama ya kutokujua kwako na mahaba yako kwake haihusu watu wenye akili


Julius Nyerere ndio Rais pekee ninaeweza kuamini kuwa hakuwahi kuliibia hili Taifa…waliofuata na watakaokuja watatofautiana viwango vya wizi na kuficha taarifa za wizi wao tu


 
Nahisi hiyo ni kama yale marubi ya longido. Yani dude kuuuubwa ila halina thamani yoyote ya maana. Mpaka yawe tani za kutosha. Halafu madini ya vito huwa yana vigezo vyake vya kitaalam wanaita C's.

Halafu mbona jiwe ni chafu sana. Nilidhani ni safi kwelikweli na lina rangi ya kutosha. Yaani mawe machafu kama hayo yapo mengi sana moro, Longido, mahenge yanauzwa bei ya nyanya 🤣
 
Kwahiyo Kwa akili yako, limetolewa wakati wa JPM ,ila Leo hivi Sasa ndo imejulikana?.




Sent using Jamii Forums mobile app
ungekuwa mfuatiliaji mzuri wa hii sekta ungejua kuwa kuna kipindi around 2yrs back mgodi huo wa Longido ndio ulitema mawe zaidi,rekodi ya kutoka mawe karibuni Mundarara hazipo,kikawaida njia za mawe ni nadra kutoka jiwe 1 tu pekee kama hilo,ukishashika mkondo(njia) yanatoka mfululizo kwa muda fulani mpaka njia ifunge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…