Tanzania siku moja itakuwa kama South Africa, au waarabu?

Nomadiq

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2025
Posts
8,572
Reaction score
22,926
Kwa timu za soka letu la Tanzania, ni nadra sana kukuta timu mbili zote zimefuzu kwenda hatua kubwa za mashindano ya vilabu Afrika.

Kwa waarabu(Morocco,Algeria na Egypt) ni kawaida sana, unakuta USM Alger na MC Alger wapo hatua za robo fainali wote, au nusu fainali.

Egypt unakuta Zamalek, Al Ahly wote wapo hatua za robo au nusu. Tunisia ukuta Berkane na Esperance wamefika robo fainali.

South Africa wamefanya kweli mwaka huu Mamelodi Sundowns, Stellenbosch, na Orlando wote wametinga hatua ya nusu fainali kwenye mashindano wanayoshiriki.

Natamani kuona Young Africans, Azam FC, Singida BS, na Simba wakitinga angalau hatua ya robo fainali kwa pamoja ndani ya msimu mmoja. Mwaka jana walijitahidi ningependa kuona ikitokea tena.
 
Timu zinategemea maombi na uchawi wee uliona wapi bwana
20240904_122706.jpg
 
Haiwezi kua siku moja bali ni mchakato... Mchakato wenyewe unatuhitaji sisi wenyewe na wala sio mwingine
 
Ah wapi uliona mchungaji kaenda kuisalia pirates au mamelodi mzeya
Huwa na wao wanapiga Dua au maombi ya kutosha wakitaka kuja hawaji kizembe ila approx. 75% wanamikakati mizuri uwanjani sio kama sisi 75% ni mikakati ya nje ya uwanja.
 
Haiwezi kua siku moja bali ni mchakato... Mchakato wenyewe unatuhitaji sisi wenyewe na wala sio mwingine
Ni kweli kabisa mkuu kuna kanuni nasikia inazitaka klabu zote zinazoshiriki ligi kuu kuwa na timu za Academy na U-15, U-17, U-23 hivi inatekelezwa ?
 
Kwa timu za soka letu la Tanzania, ni nadra sana kukuta timu mbili zote zimefuzu kwenda hatua kubwa za mashindano ya vilabu Afrika.

Kwa waarabu(Morocco,Algeria na Egypt) ni kawaida sana, unakuta USM Alger na MC Alger wapo hatua za robo fainali wote, au nusu fainali.

Egypt unakuta Zamalek, Al Ahly wote wapo hatua za robo au nusu. Tunisia ukuta Berkane na Esperance wamefika robo fainali.

South Africa wamefanya kweli mwaka huu Mamelodi Sundowns, Stellenbosch, na Orlando wote wametinga hatua ya nusu fainali kwenye mashindano wanayoshiriki.

Natamani kuona Young Africans, Azam FC, Singida BS, na Simba wakitinga angalau hatua ya robo fainali kwa pamoja ndani ya msimu mmoja. Mwaka jana walijitahidi ningependa kuona ikitokea tena.
Kwenye Yanga hapo bora ungeiweka Kengold!
 
Back
Top Bottom