Tanzania: Taifa ambalo lina amani ila limekosa haki

JET SALLI

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Posts
2,995
Reaction score
2,047
Taifa letu linasifika kote duniani kwa kuwa taifa lenye amani. Watu wanasema ukiuliza popote africa na nje ya Africa kuhusu tanzania utaambiwa ni taifa lililojipatia na kujizolea heshima kubwa duniani kupitia Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kuwa taifa lenye amani na haki kwa watu wote kwa wakati ule wa uongozi wa Baba wa Taifa. Haki ilisisitizwa na kupewa kipau mbele kwa sababu wakati wa ukoloni wa wazungu mambo hayo msingi yalikosekana.

Waafrika wa Tanzania hawakuruhusiwa kukutanika, ilikuwa ni marufuku, haki ya elimu ilikosekana, na uhuru wa watu kujiamulia mambo yao wenyewe. Leo hii watawala wetu chini ya CCM wanafanya juhudi kuturudisha kule ambako baba wa taifa na wenzie wapigania uhuru walitung'oa, leo hii hatuwezi kusema kwamba watu walimie meno au wamenyooka kupitia uongozi wa awamu ya tano, tukumbuke kwa tumelimia meno wakati wa utumwa, tumenyimwa haki wakati wa ukoloni, sasa ni vema watu wasipewe nchi tu pasipo kujua nn vipaumbele vya taifa, wakati huu baada ya kuwa taifa hili ni huru lengo si kuendelea kutesa watu katika nchi huru bali kufanya maisha ya watanzania kuwa mepesi na mazuri zaidi.

Hatuwezi kuwadanganya Watanzania kwa vitu vinavyoonekana huwezi leo wewe kama viongozi ukasema unawajali wanyonge na maskini huku vitu unavyotumia ni vya kifahari huko ni kuwafanyia unafiki wa wazi watanzania. Ndio maana tunasema haki ndio tunda la amani. Leo hii gharama za kampeni zinazotumiwa na CCM kwa mtu mwenye akili huwezi sema hiki ni chama makini. Angalia wagombea watu walivyopitisha rushwa wakati wa kura za kutafuta wagombea ubunge hiki ni chama kinachotia aibu.

Watu wengi wakiwemo wana CCM wengi walidhani Magufuli ataweza kudhibiti rushwa kwa kuanza na chama chake cha CCM hasa kwa kuwaondoa wagombea waliotumia rushwa kupata kura kwenye kinyang'anyiro cha kutafuta nafasi za ubunge.

Nadhani wote tumeona kilichotokea asilimia 80% ya waliotumia rushwa ndio waliorudishwa na wale ambao wapiga kura waliona wanawafaa na watawasaidia kuleta maendeleo wote majina yao yalikatwa sasa tunajiuliza haki ya watu kuchagua viongozi wanaowataka iko wapi na imepotelea wapi na itarudi lini. Kwa sababu watu walidhani Magufuli anaweza kutuvusha na kumbe ndio ameshindwa kabisa hivyo basi huu mwaka tunapaswa kuipumzisha CCM maana hakuna jipya tena tunaloweza kulitarajia au kulisubiri.
 
Hakuna amani. Utawala wa kikandamizi uliogopesha watu. Hakuna mani bila haki. Watu wanateswa, wanauawa, wanafungwa, halafu amani itatoka wapi?
 
Tanzania haki za mashoga na ndoa za jinsia moja sio siri hizo hazipo mwambie Lisu na Amsterdam wake
.
JamiiForums-1748853399.jpg
 
Miaka 42 unalilia haki, haki inatafutwa, haki sio wajibu. Simama itafute haki lakini sisi haki tunayo na Magufuli ana tulindia haki zetu.
 
Tunayoyasikia kusini yana ukweli wowote? Nani atatoka kututoa hofu? Sisi kaskazini je tuko salama? Au ndo mpaka uchaguzi upite?
 
Usilete ya kangi lugola ndio maana alipigwa chini uwaziri na ubunge na Lisu tunamsubiri tumpige chini October ,28 akaungane na Lugola
... saa hizi unamkana mzalendo Kangi na mabendera yake yaliyojaa kila kona ya mwili? Usitake kutuaminisha kwamba wewe ni mzalendo kuliko yeye tena kauli ile ya "mashoga kuwa salama Tanzania" aliitoa in his capacity kama waziri wa mambo ya ndani - msimamo rasmi wa serikali - kauli ambayo hadi leo haijawahi kutenguliwa iwe na Rais au kiongozi mwingine yeyote.

By the way kilichompiga chini uwaziri sio kauli ile usitake kuleta porojo hapa.
 
Taifa letu linasifika kote duniani kwa kuwa taifa lenye amani. Watu wanasema ukiuliza popote africa na nje ya Africa kuhusu tanzania utaambiwa ni taifa lililojipatia na kujizolea heshima kubwa duniani kupitia Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kuwa taifa lenye amani na haki kwa watu wote kwa wakati ule wa uongozi wa Baba wa Taifa. Haki ilisisitizwa na kupewa kipau mbele kwa sababu wakati wa ukoloni wa wazungu mambo hayo msingi yalikosekana.

Waafrika wa Tanzania hawakuruhusiwa kukutanika, ilikuwa ni marufuku, haki ya elimu ilikosekana, na uhuru wa watu kujiamulia mambo yao wenyewe. Leo hii watawala wetu chini ya CCM wanafanya juhudi kuturudisha kule ambako baba wa taifa na wenzie wapigania uhuru walitung'oa, leo hii hatuwezi kusema kwamba watu walimie meno au wamenyooka kupitia uongozi wa awamu ya tano, tukumbuke kwa tumelimia meno wakati wa utumwa, tumenyimwa haki wakati wa ukoloni, sasa ni vema watu wasipewe nchi tu pasipo kujua nn vipaumbele vya taifa, wakati huu baada ya kuwa taifa hili ni huru lengo si kuendelea kutesa watu katika nchi huru bali kufanya maisha ya watanzania kuwa mepesi na mazuri zaidi.

Hatuwezi kuwadanganya Watanzania kwa vitu vinavyoonekana huwezi leo wewe kama viongozi ukasema unawajali wanyonge na maskini huku vitu unavyotumia ni vya kifahari huko ni kuwafanyia unafiki wa wazi watanzania. Ndio maana tunasema haki ndio tunda la amani. Leo hii gharama za kampeni zinazotumiwa na CCM kwa mtu mwenye akili huwezi sema hiki ni chama makini. Angalia wagombea watu walivyopitisha rushwa wakati wa kura za kutafuta wagombea ubunge hiki ni chama kinachotia aibu.

Watu wengi wakiwemo wana CCM wengi walidhani Magufuli ataweza kudhibiti rushwa kwa kuanza na chama chake cha CCM hasa kwa kuwaondoa wagombea waliotumia rushwa kupata kura kwenye kinyang'anyiro cha kutafuta nafasi za ubunge.

Nadhani wote tumeona kilichotokea asilimia 80% ya waliotumia rushwa ndio waliorudishwa na wale ambao wapiga kura waliona wanawafaa na watawasaidia kuleta maendeleo wote majina yao yalikatwa sasa tunajiuliza haki ya watu kuchagua viongozi wanaowataka iko wapi na imepotelea wapi na itarudi lini. Kwa sababu watu walidhani Magufuli anaweza kutuvusha na kumbe ndio ameshindwa kabisa hivyo basi huu mwaka tunapaswa kuipumzisha CCM maana hakuna jipya tena tunaloweza kulitarajia au kulisubiri.
Ila mimi nipo tayari kupoteza haki lakini sio amani.

Bora iondoke haki lakini amani iwepo.

Na bora iwepo amani na haki.

Kuwepo kwa amani pia ni haki hiyo manake una haki ya kuishi kwa amani.
 
TANZANIA NI NCHI YENYE UTULIVU HAINA AMANI WALA HAKI MSIPOTOSHE.

Na huu utulivu tuliokuwa nao JIWE ANAUWEKA REHANI.
 
Ila mimi nipo tayari kupoteza haki lakini sio amani.

Bora iondoke haki lakini amani iwepo.

Na bora iwepo amani na haki.

Kuwepo kwa amani pia ni haki hiyo manake una haki ya kuishi kwa amani.

Tunataka amani ya haki na sio amani ya ncha ya upanga.
 
Back
Top Bottom