TANZANIA (taifa stars) vs CAMEROON !!!

TANZANIA (taifa stars) vs CAMEROON !!!

kwanza nawapongeza taifa stars kwa kutukwepesha aibu ya kufungwa magoli kibao uwanja wa nyumbani. hawa cameroun japokuwa naona kiwango chao cha soka kimeteremka hasa ukizingatia ushiriki wao wa kombe la afrika lakini si timu ya kuibeza hata kidogo. tena naona wamekuja full squad yaani sis wa longi tulikuwa tunasema "full masinonda".

sare hii natumaini itawapa wachezaji wetu uimara wa kisaikolojia na huenda wakafanya vizuri katika mechi zinazofuata.

jamani ukizingatia huzuni tunazoletewa na wanasiasa wetu kila siku angalau wikiendi hii hatujapata kipigo maanake ingekuwa taaaabu kweli.
 
Indomitable Lions held in Dar

Cameroon were held to a nil-nil draw in Tanzania on Saturday, in the latest round of World and Nations Cup qualifying.

The Indomitable Lions still lead group 1 with seven points from three games and Tanzania remain in third place.

But the much-touted Cameroonian strike force, including Barcelona's Samuel Eto'o, failed to register.

The team was said to be furious with the result after the match and refused to speak to waiting journalists.

The result was a riposte from Tanzania coach Marcio Maximo, who has been under strong pressure from fans and the media.

The full house in Dar-es-Salaam ended the game by chanting the coach's name.

Mauritius host Cape Verde in the other game in this group on Sunday.

bbc sports.
 
Sikia KKN pale hata akina Etoo wakilala Jolly club wakaamkia uwanjani hata draw hatupati.Kesho kichapo tu tusijipe hope za kinamna au mpaka tutoke damu ndio itajulikana Stars mahututi?
?????????????????????????????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Vijana wamecheza vizuri kusema ukweli lazima tuwapongeze,maana ingekua enzi zile basi tungefunwa 5 bila majibu lakini vijana wamezuia vizuri kiufundi,viungo nao wameunganisha timu vizuri ila tatizo bado lipo kwenye forward line kwani kuna nafasi 2 za wazi sana ilikua tufunge lakini tukashindwa,sasa tunahitaji watu wenye kimo kirefu na misuli ya nguvu/fiziki nzuri ndiyo tunaweza kufika mbali
 
Cape Verde wameshinda ugenini 1-0 dhidi ya Mauritius jioni hii na kujifikishia points 6, moja tu nyuma ya Cameroon, kibarua bado ni kizito kwetu, we need to start wining games especially at home.
 
inferiority complex ni mbaya sana!yaani droo tena ya ziro ni kama tumeshinda???????

Ni kama tumeshinda cus kwa kijitimu chetu kinavyochechemea na lile squad la cameroun ni "ushindi" tosha
 
Tunashangilia sare ya jana kisha tutajisahau kufanya maadalizi ya wiki ijayo kule yaunde.

Ukweli ni kwamba tusipoangalia tutarudi na aibu la sivyo vijana wacheze 'ngangari' kama tulivyowaona jana.

Nikiwanukuu zE kOMEDI walivyokuwa wakichambua mchezo wa jana kupitia TBC1; 'mgonjwa alishakataa kunywa uji na bahati iziraeli hakupita hiyo jana'
 
Mi nakubaliana na wazo moja kuwa camerron walicheza kwa ku relax zaidi...hawakutaka kuumia...wala kutuumiza sisi.maana nasikia wamefarijika sana na ukarimu wa ajabu walioupata...wakaonaa hakuna haja kuumizanaa...walitaka draw wameipata na wanatafuta point 3 tuu waweze kufuzu raundi ya pili...mpo?sasa subirini kwao muone msala itakavyokula kwetu...nawakilisha
 
sema sasa!

ahhh kwa hiyo draw wanawane naona tumejipa moooooyo bora hata tungewafunga ingekua raha zaidi..hebu angalia our position in de group...with jus 2 points next game ndo mwasema twaenda younde ehh???sasa tusikilizie huko tuone mambo yatakuaje!!atleast its high time tuanze kushambulia n kufunga magoli as so far tuna ka goli kamooja tuu!!
 
It is a pity,nadhani Watanzania tupunguze maneno na tucheze mpira. Kwa sasa tumebakisha mechi moja tu nyumbani na hata tukishinda hiyo moja na kuifunga Mauritius kwao, hatutaenda popote as we will have only 8 points ambazo Cameruni anaweza kuzifikia kwa kutoa sare moja tu na kwa Cape Verde kutoa sare mbili. Wote hao wana uwwezo wa kupata zaidi. The only miracle for us is to win all the remaining matches ili tufikishe point 11 na tuombe Cameruni katika mechi mbili asishinde zote. Maximo ameshindwa kabisa kupata wafungaji kwani kufunga goli moja tu katika mechi tatu ni uchuro!
 
Afu ukutaka kuamini siasa zimeutawala embu cheki na local media zinazosifia..!!, Eto'o ana andikwa kuwa ''alipotea'' hadi gazeti za leo as if hatuna mechi next weekend!!

Inauma lakini ukweli unabakia sioni future katika soka la kibongo as far as Taifa Stars is concerned!!
 
Hivi tunashangilia kutoa droo na Cameroon wakati MALAWI kamfunga MISRI ambaye hata huyo Camerron alipewa dozi ya kutosha na MISRI
Wenzetu Kenya wamewafunga Zimbabwe,Uganda kamfunga Angola,Rwanda kamfunga Moroco,Sudan kamfunga Mali
 
Sis ni wale wa kusema kufungwa tumefungwa lakini chenga tumewala. Kenya wameshinda mechi mbili mfululizo zote za nyumbani. Hiyo imewapa moyo wakenya hadi Raila kuahidi donge nono kwenye mechi ya marudiano na Zimbabwe. Sisi tukitoka nje ya Tanzania ni visingizio tele, tukija nyumbani hatushindi tunang'ang'ania droo na kujisifu.!!!!!!! Kweli hii nchi yetu ni vichwa vya wendawazimu, Ruksa hakukosea.
 
nadhani kitu kingine wa tanzania wanasahau huko na kuzidi jazana ujinga wa kushangilia draw na cameroon ni kuwa haya ni mashindano ya kugombania nafasi za both world cup 2010 na african cup of nations 2010....kwa mpigo...
so tusipojitahidi kupata walau nafasi ya pili ambayo naona yaenda kwa nchi kama cape verde we are goin to be out kwa mashindano ya kimataifa mpaka 2011 atleast tutakapoanza gombani kwa ajili ya world cup ya 2014 na afcon 2012!!!!
so de maximo guy wil stay over here kwa miaka mitatu without any proper objective maana timu ya taifa maximum labda ishiriki mambo ya chalenji dats all!!

so tuachane na ujinga wa kushabikia draw ya cameroon na kujisahau!!if we managed to draw na cameroon kwanin tukafungwa na cape verde??iweje tukatoa draw na mauritius sasa??

mbona kenya wanashinda,uganda wanafunga hadi waliotutoa sie???
 
nmekutana na ahadi za maximo mpya mwananchi kule

Maximo: Hukumu ni kwa Mauritius *Stars imeimarika, Cape Verde wajiandae

KOCHA wa Taifa Stars, Marcio Maximo amesema pointi sita atakazozipata atakapocheza na Mauritius na Cape Verde zitaiwezesha timu yake kufuzu kwa raundi ya pili ya mchakato wa kuwania kucheza Fainali za 2010.


Maximo aliyasema hayo baada ya mchezo wa juzi na Cameroon huku akisema kuwa, mchezo wa marudiano mjini Yaounde utakuwa mgumu, lakini lazima kushinda mechi ya Mauritius na Cape Verde.


?Unajua ule ulikuwa mchezo wa kwanza na ndiyo maana nikasema tunaanza. Tumetoka sare mbili, tumepoteza moja, lakini michezo ijayo ukiondoa ule wa Jumamosi dhidi ya Cameroon, nasema pointi sita zipo kwani timu imeimarika.


Stars yenye pointi mbili baada ya kucheza michezo mitatu imebakiza mechi tatu dhidi ya Cape Verde Mauritius na mmoja dhidi ya Cameroon itakayochezwa Juni 21.


Maximo, ameuondoa katika hesabu zake mchezo huu dhidi ya Cameroon na kuiangalia zaidi michezo miwili dhidi ya Cape Verde na Mauritius.


Maximo alisema endapo timu yake itashinda michezo hiyo miwili, itafikisha pointi nane ambazo itaisaidia timu hiyo kufuzu.


"Nakubali ya kwamba tulipoteza pointi mbili hapa dhidi ya Mauritius, inaniuma sana, lakini bado timu ina nafasi ya kufuzu ikijipa matumaini ya kufikisha pointi nane baada ya kushinda michezo miwili dhidi ya Cape Verde na Mauritius.


Ninasema hapa lazima kushinda, tutajitahidi na nataka kusema Cape Verde hawatoki hapa, lazima tutawafunga, najivunia timu yangu imeimarika sana.
 
wajimini nina swali,nikiangalia taifa stars kila mchezaji alikua na kitambaa cheusi mkono wa kulia,je tulikua twaomboleza au ndo mambo ya chenge hayo walikua wakitafuta siti uwanjani??!!?
maan anishasikiaga african teams hufanyaga mambo hayo
 
Back
Top Bottom