nmekutana na ahadi za maximo mpya mwananchi kule
Maximo: Hukumu ni kwa Mauritius *Stars imeimarika, Cape Verde wajiandae
KOCHA wa Taifa Stars, Marcio Maximo amesema pointi sita atakazozipata atakapocheza na Mauritius na Cape Verde zitaiwezesha timu yake kufuzu kwa raundi ya pili ya mchakato wa kuwania kucheza Fainali za 2010.
Maximo aliyasema hayo baada ya mchezo wa juzi na Cameroon huku akisema kuwa, mchezo wa marudiano mjini Yaounde utakuwa mgumu, lakini lazima kushinda mechi ya Mauritius na Cape Verde.
?Unajua ule ulikuwa mchezo wa kwanza na ndiyo maana nikasema tunaanza. Tumetoka sare mbili, tumepoteza moja, lakini michezo ijayo ukiondoa ule wa Jumamosi dhidi ya Cameroon, nasema pointi sita zipo kwani timu imeimarika.
Stars yenye pointi mbili baada ya kucheza michezo mitatu imebakiza mechi tatu dhidi ya Cape Verde Mauritius na mmoja dhidi ya Cameroon itakayochezwa Juni 21.
Maximo, ameuondoa katika hesabu zake mchezo huu dhidi ya Cameroon na kuiangalia zaidi michezo miwili dhidi ya Cape Verde na Mauritius.
Maximo alisema endapo timu yake itashinda michezo hiyo miwili, itafikisha pointi nane ambazo itaisaidia timu hiyo kufuzu.
"Nakubali ya kwamba tulipoteza pointi mbili hapa dhidi ya Mauritius, inaniuma sana, lakini bado timu ina nafasi ya kufuzu ikijipa matumaini ya kufikisha pointi nane baada ya kushinda michezo miwili dhidi ya Cape Verde na Mauritius.
Ninasema hapa lazima kushinda, tutajitahidi na nataka kusema Cape Verde hawatoki hapa, lazima tutawafunga, najivunia timu yangu imeimarika sana.