Tanzania(Taifa Stars) yanyolewa bila wembe na Algeria goli 4 kwa 1

Tanzania(Taifa Stars) yanyolewa bila wembe na Algeria goli 4 kwa 1

Kunyolewa bila wembe kupoje? Au ulitaka kusema wamenyolewa kwa chupa?
 
Bado tunaelekea kwenye mziki wa congo DR hatuwezi toka ata kwa dawa
 
Kwa viwango wale Algeria wapi vizuri Na wamesha shiriki world cup...ni kiwango jingine,tumejitahidi kwa kiwango chetu
Linalotakiwa ni Tanzania kuwekeza katika michezo yote ikiwamo soka,tuwe Na misingi,academy za kutosha shule Na vyuo vya michezo,viwanja vya kutosha baadae tutafurahi,hawa wenzetu waliwekeza Na walianza harakati kitambo
Hebu serikali tuanze Na watoto wadogo.
 
Kuna mambo nadhani hatuko sawa. Sijui kama timu zetu za taifa tuna walimu wa Saikolojia. Kuna wachezaji wanajituma sana lakini wengi wao hawana confidence, ndiyo maana wanapoteza pasi nyingi sana kwa wapinzani. Mf ni Himid Mao. Leo hakuwa kwenye form nzuri kimchezo.

Vile vile timu haikuwa na muunganiko mzuri kuanzia nyuma mpaka mbele. Yondani, Banda na Kapombe hawakuwa na maelewano. Pia Mudathir, Ndemla na Mao hawakuunganisha vizuri walinzi na washambuliaji. Mie siyo shabiki wa timu yoyote Tz, lakini nadhani Mkude na Mzamiru wangefanya vizuri zaidi.

Pongezi kwa Msuva na Samatta. Wamecheza vizuri sana, hasa Msuva. Goal keeper siyo mbaya, lakini angejitahidi kupunguza weight maana ana kitambi kabisa!
 
Timu ya Taifa(Taifa Stars) imeambulia kipigo cha mabao 4 kwa 1 kutoka kwa timu ya Taifa ya Algeria katika mchezo wa kirafiki

> Goli pekee la kufutia machozi la Taifa Stars limefungwa na Simon Msuva anayekipiga katika Klabu ya Difaa El Jadid ya nchini Morocco

View attachment 722670
International Friendly Match‬
‪Algeria 4-1 Tanzania ‬
‪[emoji460]️Baghdad‬
‪[emoji460]️Msuva‬
‪[emoji460]️Kapombe (og)‬
‪[emoji460]️Carl‬
[emoji460]️Baghdad
‪84'‬
Piga mbwa hao
 
Kiufundi Mimi nimefurahi hata kama tumefungwa hizo goli kwani kuna Kitu kikubwa mno tumejifunza kwa Kucheza na Watu ambao wametuzidi kwa kila kitu. Tena leo tumejitahidi kwani katika ile mechi ya Kimashindano tulifugwa Wiki / Goli Saba ( 7 ) nzuri tu lakini leo tumezipunguza na kufikia hizo Nne ( 4 ) hali ambayo inaonyesha kuwa tumejitahidi na taratibu Timu yetu ikiwa inapata mechi za Kirafiki na Mataifa makubwa na yaliyotuzidi basi huko mbeleni tutakuja kuwa wazuri mno.
Kila siku mnajifunza
 
Inasikitisha sana Taifa stars haiwezi kumiliki mpira wala kugawa pasi za uhakika kadhaa za kupanga kuishambulia timu ya Algeria.

Ni kama vile Taifa Stars walikwenda kuvuia mvua ya magoli isiwapate. Jina Mahrez wa Leicester City liliwafanya kukosa kujiamini wakati pia wa Algeria wanajua makali ya Mbwana Samatta na Simon Msuva lakini Algeria walikuwa na game plan isiyo angalia ''majina'' makubwa ya Taifa Stars.

Timu yoyote ili ishinde inatakiwa kuwa na wachezaji wa ulinzi na viungo wenye uwezo wa kumiliki na kutoa pasi za mpira baina yao kwa uhakika kabla ya kuwatupia kina Samata na Simon Msuva.
 
Tena hzo 4 wamejtahd. Tz mpra bado. Tuanzie kwenye accademy kwanza.
 
Yule mzee alilazimishwa kuifuta ile kauli ya kichwa cha mwenda wazimu. Ila kiuhalisia hakukua na ulazima wa kuharakisha kuifuta.
 
Timu ya Taifa(Taifa Stars) imeambulia kipigo cha mabao 4 kwa 1 kutoka kwa timu ya Taifa ya Algeria katika mchezo wa kirafiki

> Goli pekee la kufutia machozi la Taifa Stars limefungwa na Simon Msuva anayekipiga katika Klabu ya Difaa El Jadid ya nchini Morocco

View attachment 722670
International Friendly Match‬
‪Algeria 4-1 Tanzania ‬
‪⚽️Baghdad‬
‪⚽️Msuva‬
‪⚽️Kapombe (og)‬
‪⚽️Carl‬
⚽️Baghdad
‪84'‬
mfungaji wa goal la Tanzania ni msuva au kichuya?
 
Kuna msemo maarufu sana uliosemwa na wahenga na wengi wetu tukafundishwa mashuleni kwamba SIKIO LA KUFA HALISIKI DAWA, kuliko kuendelea kuwekeza Kwenye mchezo wa mpira wa miguu kama Taifa, ni bora hayo mapesa mengi tunayopoteza tukawekeza Kwenye mpango wa nuclear, miaka thelathini toka sasa tuwe na uwezo angarau wa kuzalisha Makombora ya masafa mafupi yatakayo tusaidia kujikinga na maadui ukizingatia kwamba tuna madini ya uranium ya kutosha.
images%20(3).jpg
 
Kabisa mkuu.
Maana si kwa kugeuzwa gunia la mazoez ya ngumi huku asee
 
Back
Top Bottom