Tanzania(Taifa Stars) yanyolewa bila wembe na Algeria goli 4 kwa 1

Tanzania(Taifa Stars) yanyolewa bila wembe na Algeria goli 4 kwa 1

Ushauri wa Zitto ufuate, pesa yote ya michezo ya kubahatisha ipelekwe kwenye michezo. Huwezi kufanikiwa bila kuwekeza. Jk alianzisha uwanja bora kabisa lakini umekua wakupigia selfie. Tatizo bajet hakuna.

Lakini pia watanzania tunapenda mawaziri wa chache wenye majukumu mengi bila kujua athari zake, utasikia mtu anaitwa waziri wa Habari, sanaa, utamaduni na michezo. Kwa bajeti gani na kichwa gani abebe hayo mambo yote? Ona sasa week hii TFF walikua bize kufungiana wizara nayo ilikua bize kupambana na wasanii matokeo yake tumepigwa tobo.
Kama wewe, ambaye tunadhani ndiye msomi,hujui uwanja wa kisasa wa mpira ulijengwa na Mkapa na si JK,unadhani Taifa stars kuifunga Algeria ni rahisi hivyo?Hatupo serious!

Sote tumekubaliana vyerehani vinne ni kiwanda bado una matumaini ya kuifunga Algeria?!!
 
Maswali mengine bhana kirahisi hivyo ulitegemea kuwafunga Algeria kwa wachezaji gani labda Kichuya, Himid mgonjwa kabs au Mudathiri mwenye kiwango kama homa kupanda na kushuka la muhimu kuandaa wachezaji wadogo wapate exposure nje ndo tuje kushindana
 
Mkuu inawezekana wewe sio mtu wa mpira, Brazil wenyewe walishawahi kufungwa goli 7 pamoja na mastaa walionao. Taifa stars imecheza vizuri by the way
Acha unafiki imecheza vizuri
wakati imetobolewa 4-1 hiyo timu
ni ya kuifuta kabisa
 
Waungwana na swali kidogo nimeona niwashilikishe hivi taifa stars kuna timu inayoweza kuifunga hapa Africa
 
bongo tangu lini tukajua kucheza Mpira ...watanzania niwatu wamaneno mengi kuliko mikakati"
ukitizama magazeti ya kibongo yanavyo upamba Moira wa tz ..unaweza kusema yeeeess team sindio hii''"
kumbe magilini tu hamna kitu ...
 
Mkuu inawezekana wewe sio mtu wa mpira, Brazil wenyewe walishawahi kufungwa goli 7 pamoja na mastaa walionao. Taifa stars imecheza vizuri by the way
baada ya kufungwa goli 7 unajua kilichoktokea"" kocha akajiudhulu...taifa zima lilikuwa linapiga makelele mwanzo mwisho "" na nidhani sasa hivi wajionea kuwa team yao ipo ktika muelekeo Upi"" haya rejea tz ...baada ya kizazi cha kina tenga kuisha katika soccer ..'' kuna lipi lamaana ambalo limeshawahi kufnya na hiyo team "" kazi kutumia pesa za walipa kodi kiboya boya tu pasipo uwepo wa manufaa
 
Bora kucheza kombolela kuliko kocheza mpira hapa bongo land
 
Siku Nikiwa Rais Nchi Hii Timu Ya Taifa Naifuta Viwanja Vyote Naviuza Kwa Timu Binafsi Pesa Naenda Kuwekeza Maji Na Kilimo Kwa Wananchi Vijijini Huko Hii Timu Ndiyo Maana Mwinyi Alisema Ni KICHWA CHA MWENDAWAZIMU Kila Mtu Anajifunzia Kunyoa
 
KAMA UZALENDO NI KUSHANGLIA STARZ, MIMI SYO MZALENDO. TUSIDANGANYANE HAPA, HATA MAGU HAIPEND STARS
 
Hatuna wachezaji, club haziandai wachezaji kuwa na uwezo wakimataifa.
Mchezaji anandaliwa kwenye club kuanzia akiwa mdogo, sasa uku kwetu club hazina academy zitakazo kuza wachezaji kuwa na uwezo mzuri.
Wachezaji wa Tanzania hawana:-
Agility
Match fitness
Technic
Tactical awareness
Sharpness
Passing
Positioning

Hauwezi ukawa na wachezaji wa namna hiyo halafu unategemea watakua na uwezo wa kupambana na wachezaji wenye levo za kimataifa.

Tunatakiwa kuandaa wachezaji kuanzia kwenye grassroot ndio tutaweza kuipeleka Taifa stars afcon.

naona hta wachezaji wa ngorongoro heroes wana matatizo uliyataja hpo juu na hawa ndyo future ya taifa stars

tutegemee maumivu zaidi siku za mbeleni....kwa staili hii mchezahi yupo peke yake anashindwa hta kuwa na utulivu wa kuposses na kutoa pass accuracy ni janga kubwa
 
Hatuna wachezaji, club haziandai wachezaji kuwa na uwezo wakimataifa.
Mchezaji anandaliwa kwenye club kuanzia akiwa mdogo, sasa uku kwetu club hazina academy zitakazo kuza wachezaji kuwa na uwezo mzuri.
Wachezaji wa Tanzania hawana:-
Agility
Match fitness
Technic
Tactical awareness
Sharpness
Passing
Positioning

Hauwezi ukawa na wachezaji wa namna hiyo halafu unategemea watakua na uwezo wa kupambana na wachezaji wenye levo za kimataifa.

Tunatakiwa kuandaa wachezaji kuanzia kwenye grassroot ndio tutaweza kuipeleka Taifa stars afcon.

nadhani pia tuangalie na suala la walimu kwa mfano pale azam wana academy nzuri tu lkn angalia product zao wachezaji wakishafuzu kutoka hpo kwenye academy yao unakuta bdo ana mapungufu kbao hebu mwangalie mchezaji km yahya zaid hyu kakulia kwenye academy ya azam na alikuwa top player kutoka kwebye hyo academy lkn ona madudu anayofanyaga uwanjani km amekulia kwenye soka la mitaani ana mapungufu kbao
 
Watanzania watu wa ajabu hivi hata ukichukua viwango vya wachezaji mmojammoja wa Algeria yupi unaweza kumlinganisha na wa Tanzania kwa kifupi wengi wameharibiwa na premiur League ya Uingereza ambao kila siku wanaonyesha wao ni bora lakini hawana mafanikio, sisi tunatakiwa tujenge timu kuanzia ngazi ya vilabu ndio tuweze kujilinganisha na nchi hizo
 
MANULA alijua akidaka angepigwa nyingi na ingemharibia UTANZANIA ONE FEKI wake.... pole Aisha
 
Back
Top Bottom