Tanzania Tena! Waisrael waja kufanya uwekezaji Mkubwa wa Mahoteli Zanzibar

Tanzania Tena! Waisrael waja kufanya uwekezaji Mkubwa wa Mahoteli Zanzibar

Wawekezaji mnakaribishwa, tulisheleweshwa sana ktk miaka sita iliyopita kwa sera ambazo zinasema masikini ambaye hajawahi kula mnofu wa nyama akipata nyama itamuozea mkononi kwa kuishangaa na kutoamini anayo.

Tanzania tuna fukwe za mchanga mweupe ulio safi bila uchafuzi wa mazingira, bahari na maziwa yenye maji ya buluu, mbuga za wanyama, viwanja vya ndege vya kimataifa AAK Zanzibar, JNIA Dar es Salaam, KIA Kilimanjaro, Songwe Mbeya, watu wakarimu, pia kunafikika kwa kutumia masaa machache ni nini tunataka tupewe zaidi ?
Chato International Airport umeisahau.
 
Haya ndo matokeo ya kufanya kazi kwa akili na sio maguvu!

Jarida maarufu nchini Israel la The Times of Israel limeripoti kuhusu Waisrael kuja kufanya uwekezaji mkubwa Zanzivar ikiwemo kujenga Hoteli kubwa za kisasa katika kukuza soko la utalii

Jarida hili halijaishia hapo bali limekwenda mbali na kuelezea kwa namna gani Tanzania kwa ujumla ina vivutio vizuri kuzidi hadi South Africa ila havijapewa kibaumbele. Limetaja mlima K8limanjaro na mbuga ya Serengeti.

Hii ndo Tanzania tunayoitaka. Hongera Rais Samia kwa maono yako katika kukuza Utalii. Kweli tunaanza kuona Matokeo
View attachment 2342822
View attachment 2342840

Lord Denning
Tel Aviv, Israel
Nzuri sana
 
Kina Mr Tozo From Singa-poo!!
Umejuaje bana hahaha...
drakekidding.png
 
Tatizo lenu Waafrica wa Bongo Mna roho za kiswahili mnoo!! sasa wakisha jikita hamkawii kuwaita Majina ya hovyo! utasikia Mara Mkoloni,

Mara minyonyaji, Bwanyeye!

Mara gabachori wamerudi! wezi tu Hao!

Mara Mibepari hii inatunyonya tu na ukoloni Mambo leo! kwa akili zenu za njaa hizo! mnadhani hawajui??

Si walikuwa wamejaa humu?? kwa nini mliwafukuza nyie??! tena kwa Masimango wakaacha Mali au mmesha sahau mara hii tu!! mpaka wakaacha mali zao tele humu,...

angalia Mijengo ya maana Ikulu tamu ile! UDSM wao, K/koo wao! Hotel 77 wao nk! huyo Mama amesema atawarudishia au!!

Yaani mnataka waje wawainueeee! halafu Muwageuke? Mnadhani wao wajinga?? miafrica hamuaminiki pambaneni na hali yenu tu! hamtaki mtashikwa nyaaa!! wale hawaji ng'ooo! mtasubiri sana!

wakijitahidi saana, watakaa Nairobi asubuhi kazini zanzibar! mchana wanarudi na hela kulala Narobi /MOMBASA!!...mara ngapi Balozi zetu zimeshushuliwa huko Israel??

Mazayoni wanapenda Uganda tuuu hapa EA!..kwa sababu zao za kihitoria baaasi!...Hitoria gani hiyo?? hilo ni somo jingine kwa wakt mwingine!...usikose threads zangu...........
 
Wakenya mkuu nao hawapo mbali,na wamejazana huko fukwe za zenji balaa
Wakenya wanatuzidi kwenye Customer service sisi hatuko serious unamkuta Mhudumu wa Kitanzania anachati kwenye simu yake unakaa anakuangalia kama vile amelazimishwa kufanya kazi.

Tupanbane ndugu zangu Watanzania soko la ajira linataka tupambane kwelikweli.

Nakumbuka ile Migodi ya Barrick Watu walikuwa wakifukuzwa kwa wizi wa Dizeli lita 20.
 
Back
Top Bottom