Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili kati ya 1981-82 [Kaimu] na 1982-85 Madaraka Kamili kwa kuteuliwa na Mkuu wa Chuo, Wakati Huo Rais Julius K Nyerere. Mojawapo ya kazi yangu ilikuwa kuandaa mambo kama haya. Nimefurahia kuwa matayarisho sasa yanaanza kuzaa matunda. Nitatayarisha makal maalum na kuyaleta katika Jukwaa la Jamii. Kama kuna msomaji anayetaka kuniuliza maswali mahsusu kuhusu jambo hi;li, anakaribishwa. Niwezalo kusema sasa hivi ni kuwa Kenya imeshaipiku Tanganyika katika swala la kukufaidi Kiswahili kama ajira nje! Sisi tumekifaidi zaidi kama kiungo cha makabila kiasi kuwa sasa hata wahaya wanaanza kuzungumza Kiswahili wao kwa wao. Kiswahili sasa hakina tena "shombo". Ninajivuna kuwa nilikuwa mmojawapo wa wale walioisafisha hii shombo kwa kushirikiana na UNESCO na kwa msaada wa Finland. Ukiona vinaelea, vimeundwa!
Canute W TEMU, 0754282101, cwtemu@gmail.com. Mshiriki wa Maendeleo, Mwalimu wa Kiswahili Helsinki, Uingereza York, Ujerumani Hamburg na Bayreuth ;pia Mfasiri na Mkalimani. pia mkulima wa Iliki, Vanila na Tangawizi kijijini Masaera, Kilema Kusini, Moshi Kilimanjaro.
Ajira hizo changamkeni!