Huyo anayesema wamejenga 67 hakuna hata moja imekamilika,ushahidi tunao kwanza hakuna sehemu tumeshuhudia uzinduzi wa hospitali mpya ukiacha vi heath centres vya mln 400,pili huku niliko kuna hospitali 3 ziko kwenye hatua mbalimbali za ujenzi na hazijulikani zitakamilika lini hapo ni toka 2015 sasa hizo 67 ziko wapi si bora wangesema tumeanza ujenzi wa hospitali 67 za wilaya
By the way nchi ina wilaya zaidi ya 135 afu kuna hospital 5+67 na kuna mikoa haina hospitali hapo sijataja kata,jeuri ya kujipiga kifua inatoka wapi wakati kuna upungufu wa 70% kwenye huduma za afya? Sielewi kujenga daraja la kuvuka ziwa kwa hali kama hiyo hapo juu,akili kama hizi zinapatikana kwa watu wa ccm tu na yale mazuzu yanashangilia.Nilimsikia rais anasema wagonjwa na wamama wanakufa kusubili pantoni waende hospital sasa kwa nini kusijengwe hospital huko wanakotoka?
Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo amesema Rais John Magufuli ametoa Sh284.5 bilioni kwa ajili ya kuboresha na kujenga vituo vipya vya afya nchini.
Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Aprili 30 katika viwanja vya Mwakangale wilayani Kyela katika ziara ya Rais Magufuli mkoani Mbeya.
“Tukizungumzia sekta ya afya juzi tu kule Mbonde Mtwara Rais umezindua kituo cha afya kikiwa ni miongoni mwa vituo vya afya vilivyoboreshwa 352, vituo vya afya vipya 67 ambavyo vimetumia Sh284.5 bilioni.”
“Tunakushukuru ndiyo maana watu wa Ipinga wanafahamu kituo chao cha afya ni bora kuliko hospitali ya wilaya, tumeshaleta dawa, vifaa tiba na vifaa vya kisasa mpaka pasi pale ipo,” amesema Jafo.
Aidha, Jafo amesema Rais ameidhinisha Sh52.6 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa shule, madarasa, nyumba za walimu na vyoo.
ATLEAST TOA UJINGA KAKA.
AU HUJUI KWANINI BUDGET INATENGWA??
KWAHIYO ULITAKA RAIS AJIKITE KTK AFYA TU ILHALI MIUNDOMBINU MIBOVU?
KIGAMBONI VITUO VYA AFYA VIPO.
ISIPOKUWA KUNA CHOICE YA MTU.
KUMBUKA DAR NI JIJI.
KUNA WALIOTAKA KUWAHI KAZINI WENGINE KUWAHI MASHULE NDIO MAANA DARAJA KUJENGWA LIMEWAPA WATU UNAFUU KUWAHI WAENDAPO.
VITUO VYA AFYA VINAJENGWA IT MEANS RAIS ANASTAHIL PONGEZI KWASABABU ANATEKELEZA KINACHOSTAHILI.
KAONA VITUO VYA AFYA VIDOGO AKATOA HELA VIONGEZWE NA KUBORESHWA.
KUMBUKA AKATI MAGU ANAINGIA MADARAKAN HATA X-RAY MACHINES ZILIKUA TABU HADI HUKU MJINI.
AKAONGEZA VIFAA TIBA IKIWEMO VITANDA,VIFAA VYA MAABARA NA MADAWA.
HUYO BADO HASTAHILI PONGEZI??
INGEKUWA AMEAHIDI HALAFU HAKUNA KINACHOENDELEA KWELI.
LAKINI KUMBE KESHAANZA KUJENGA TATIZO LIKO WAPI??
KTK AFYA KASHAANZA UTEKELEZAJI WACHA ABORESHE MIUNDOMBINU.
WE HAUJUI TULIKUA TUNASUMBUKAJE KTK KUWAHI SHUGHULI ZETU KIPIND DARAJA HALIPO.
MUDA MWINGINE FICHA UJINGA.