Jamani ni ushauri tena tumeshaona kwa muda mfupi tu ni viongozi wangapi wamepoteza maisha mwaka huu tu kwa miezi mitatu. Lakini hatujui ni Watanzania wangapi hasa wenye umri mkubwa na wale wenye matatizo mengine ni wangapi wamepotea. Mimi binafsi nimechanjwa na nilikuwa tayari kupigwa chanjo yeyote kati ya hizi wataalamu wa kitaifa wamezipitisha kuwa salama.
Huu ni wakati wa kuokoa maisha ya Watanzania. Baada ya maziko ya shujaa wetu Magufuli maambukizi yataongezeka kwasababu ya mikusanyiko na kutokufuata masharti. Tuliambiwa wizara inafanya uchunguzi ni wakati wakutupa msimamo wa wizara kwasababu hizi chanjo zinagombaniwa na nchi nyingi sana. Lakini nawashukuru maraisi wastaafu kwa kuonyesha kuvaa barakoa sio kitu kibaya kwa kuokoa maisha na maambukizi.
Wengi wanasema watu hata viongozi wamekufa na sababu nyingine lakini Corona ndivyo inavyo ua ni kwamba inafanya tatizo lingine ndilo likuondoe kama ni moyo, kisukari, pumu, na magojwa mengine. Vilevile bila kujua sababu wenye damu type A wanazidiwa zaidi hata wale vijana!. Ukisikia kijana kalazwa kwa Corona kamuulize aina yake ya damu wengi ni type A.
Raisi Samia chukua hatua mapema. Tukiongea na familia hata za hawa waliofariki na madaktari ambao wengine tumesoma nao wanasema neno moja tu Covid19! maana yake wamekufa kwa Corona.