SoC04 Tanzania tuitakakayo tutaipata kwa kuweka msingi bora wa malezi kwa vijana

SoC04 Tanzania tuitakakayo tutaipata kwa kuweka msingi bora wa malezi kwa vijana

Tanzania Tuitakayo competition threads

PRISCAR MWAKA

New Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
3
Reaction score
0
Malezi
Malezi ndio Msingi bora wa kutengeneza watu bora na watu wa maana katika nchi ,malezi yasipokuwa mazuri kwa watu hakika tutatengeneza Tanzania ambayo itakosa kuwa na viongozi wazuri na wanaowajibika katika kuhakikisha kwamba tunasonga mbele.

Malezi sizingumzii kwa watoto tu hata kwa watu wazima nikiwa. na maana kwamba hata Vijana ambao wana ndoto siku moja ya kuwa viongozi wakubwa ni lazima wapate mafunzo kutoka kwa wakubwa wao waliowatangulia either katika kazi au siasa ili waweze kujifunza vema ili kuwa na Tanzania yenye mafanikio mbeleni ni vema tutengeneze mambo yafuatayo;

1. TUTENGENEZE VIONGOZI BORA KUPITIA MALEZI
Watu wakipewa malezi bora ya uongozi wakafundishwa ni kwa namna gani kiongozi awe bora afanyaje ili kuleta mabadiliko hakika miaka hiyo ya mbeleni Tanzania itakuwa bora sana.

2. TUTENGENEZE UCHUMI IMARA
Uchumi utakuwa imara katika nchi kwasababu watu wamepewa elimu ya fedha kuanzia Nyumbani kwetu kuwafundisha watoto mpaka kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa na hili litawezekana sana kama serikali itaweka budget kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na wakubwa wawe wanaweka mikakati ya kukutana pamoja na kubadilishana mawazo ya namna gani kama nchi tuinuke na kufika mbali lever nyingine ya uchumi.

3. TUTENGENEZE FAMILIA BORA MAJUMBUNI KWETU
Kuwa na familia bora na yenye Amani itafanya tuwe watu wenye mafanikio makubwa sana nikiwa na maana kwamba migogoro ya kuachana mama na baba ipungue kasi kwani mtu hawezi kuwa kiongozi bora au akafanya mambo bora na mazuri katika nchi kama katika lever ya familia hakuna amani na ameshindwa kuiongoza.

TUTENGENEZE VIJANA AMBAO WATAKUWA NA UJASIRI WA KUANZA KUFANYA MAMBO MAKUBWA BILA KUOGOPA
Vijana wengi ni waoga kwenye kuanza kufanya jambo wapo vijana wengi sana mtaani wana mawazo mazuri sana lakini wanashindwa kuchukua hatua ya kuanza kufanyia kazi mawazo yao ili kufikia ndoto kubwa walizonazo na kufanya nchi iinuke kiuchumi lakini pia kwa innovation za watu walizonazo iinueke katika technolojia.

HITIMISHO
Tanzania inavijana wengi sana na wana mawazo mazuri sana Serikali ingejaribu kuweka mpango mkakati ni kwa namna gani inawafikia vijana na kusikia mawazo walionayo kuhusu nchi lakini kukutana nao tu haitoshi pia kuwashika mkono Vijana ili wakatimize ndoto zao na kujenga nchi yenye mafanikio makubwa sana.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom