SoC04 TANZANIA TUITAKAYO: Serikali ya Uthubutu, Uwajibikaji mzuri kwa maendeleo bora katika Sekta ya Elimu

Tanzania Tuitakayo competition threads

My beginning

Member
Joined
May 31, 2023
Posts
11
Reaction score
8
Tofauti na awamu nyingine za maraisi waliopita , serikali ya sasa chini ya awamu ya sita ikiongozwa na Raisi wa jamuhuri wa muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan inaonesha kujenga shule nyingi Kwa ajili ya kutataua changamoto ya ukosefu wa madarasa. Zaidi kuwepo wa Elimu ya bure mashuleni bila ada imepelekea ongezeko kubwa la wanafunzi kuanzia shule za msingi mpaka sekondari.

Takwimu za Tamisemi zinaonyesha kuwa katika Mwaka 2023 wanafunzi wa darasa la kwanza walioandikishwa hadi Februari walikuwa ni milioni 1.78 ambapo kati yao, wasichana walikuwa 917,211. Undikishaji huo ni sawa na asilimia 109.07 ya lengo la kuandikisha wanafunzi milioni 1.63 na pia ni ongezeko la wanafunzi 60,320 ikilinganishwa na wanafunzi walioandikishwa kwa kipindi kama hicho mwaka 2022.

Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake Kwa mwaka 2023/2024Waziri wa Tamisemi, Angellah Kairuki anasema Ongezeko limetokana na uhamasishaji wa jamii, ujenzi wa vituo shikizi na kuendelea kutoa elimu msingi bila ada. Lakini licha ya taarifa hizo zinazoonesha kuwa Kuna Maendeleo makubwa kiuhalisia bado Kuna huduma na mifumo ya elimu isiyo Bora Katika Maendeleo mazuri katika Sekta ya Elimu.

Moja ya sababu kubwa inayopelekea Uwajibikaji dhaifu ni kutokana na ukosefu wa walimu kuanzia ngazi ya msingi mpaka sekondari hasa maeneo ya vijijini. Mfano mwezi tarehe 7 mwezi wa nne mwaka huu gazeti la mwananchi liliripoti ukosefu wa walimu kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera ikifungua shule 33 mpya, wadau wa maendeleo wilayani humo wameitaka serikali kuajili walimu wa kutosha ili kuinua taaluma kwa wanafunzi ukilinganisha na hali ilivyo sasa.

Haitoshi mwaka 2023, shule ya sekondari mji mpya iliyopo manisipaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro iliiomba serikali kuwapatia walimu wa masomo ya sayansi pamoja na shule ya sekondari Shisyete iliyopo mbeya inakabiliwa na ukosefu wa walimu na vifaa shuleni na shule nyingine nyingi zaidi hasa maeneo ya vijijini unaeza kukuta shule inawalimu Tisa tu wanafunzi kibao Hali inayopelekea Uwajibikaji mbovu wa Elimu.

Nini kifanyike kuwa na serikali ya Uthubutu, Uwajibikaji Mzuri Kwa Maendeleo Bora Katika Sekta Ya Elimu;

1. Elimu ya Vitendo Kwa njia ya teknolojia ya habari na mawasiliano
Elimu ya Vitendo Kwa njia ya teknolojia ya habari na mawasiliano itasaidia kupunguza uhaba wa walimu. Kupitia vifaa vya sauti na video mashuleni itasaidia wanafunzi kupata uelewa zaidi Kwa sababu watakuwa wanajifunza kupitia picha, video na sauti Hali inayopelekea uelewa wa haraka. Pia itasaidia mwalimu kufundisha wanafunzi wengi kwenye maeneo yenye uhaba wa walimu hata pale ambapo Kuna mikondo mingi na madarasa mengi atatumia video Kwa ajili ya wanafunzi wote na kuokoa muda.

2. Elimu ya masuala ya kijamii mashuleni
Serikali inapaswa kuzingatia elimu ya kijamii mashuleni kwani itasaidia kuwa na Uwajibikaji Mzuri Kwa Maendeleo Bora. Mfano wa Elimu hii ni pamoja na ukatili wa kijinsia, ndoa za utotoni na mimba katika umri mdogo. Elimu hii itasaidia wanafunzi wengi kuelewa mfumo mzima wa kijamii. Mfano jinsi Gani ndoa za utotoni na mimba katika umri mdogo utaleta madhara na fikira potovu juu ya safari Yao ya ndoto za baadae katika maisha Yao, kwani Kwa kufanya Vitendo ivo katika umri mdogo huathiri tabia zao na madhara mengine kama kifo lakini zaidi itawapa hamasa katika Elimu Yao na kuepuka athari mbalimbali mpaka watahakikisha wanafikia malengo Yao ambayo ni muhimu kama vijana na kuwekeza nguvu katika taifa Kwa ujumla.

3. Ongezeko la walimu na vitendea kazi mashuleni
 japokuwa serikali inapambana kuleta Maendeleo Kwa umma kama vile kujenga shule nyingi za msingi mpaka sekondari ila bado Kuna changamoto katika suala zima la walimu Kwa shule za msingi mpaka sekondari hii imekuwa kero na shida sana Kwa wanafunzi na walimu Hali inayopelekea Uwajibikaji mbovu katika Elimu. April 12, mwaka huu Raisi Samia Suluhu Hassan aliridhia kibali Cha kuajiri watumishin21, 200 Kwa kada za ualimu na Afya ambapo watumishi 13,130 ni ualimu wa sekondari na msingi lakini bado changamoto hii imekuwa kero, Hali inayopelekea mfumo mbovu mfano matokeo ya shule kuwa mabovu na yakutoridhisha ni Moja ya sababu ya kutokuwa na walimu na vitendea kazi duni, hii tunaona katika shule zote vijijini na mijini ila hasa vijijini . Tunaona wanafunzi wakiwakilisha kero kama hii mara nyingi muda wa risala kwenye mahafali Yao, Kwa kweli serikali izingatie sana jambo hili. Tazama hapa;

4. Uboreshwaji Mzuri wa vituo vya ufundi
KUtokana na mfumo wa Elimu tuliorithi kutoka Kwa wakoloni umeathiri sana mfumo mzima wa Elimu iliyopo Kwa sasa. Mfano kuanzia chekechea, msingi, sekondari mpaka chuo hii yote tumerithi Kwa wakoloni. Ifikie hatua serikali iangalie upande wa pili mfano wanafunzi wakimakiza Elimu ya msingi itabidi waendelee katika vyuo vya ufundi Kwa muda kama miezi mitatu Kwa ajili ya mafunzo yatayosaidia wao kupata ujuzi na maarifa mbalimbali kuhusiana na maisha kiujumla. Itawafumbua macho kupitia Elimu hii na kuanzia kutazamia fursa nyingine katika jamii na sio kutegemea tu ajira za serikali. Hata ikitokea mwanafunzi kashindwa kuendelea na Elimu ya sekondari tayari anakuwa na ujuzi wa ujasiliamali katika Sekta mbalimbali mfano ufundi mwashi, bomba, ushonaji wa nguo. Hii itasaidia kupunguza kero na shida ya ukosefu wa ajira Kwa vijana wengi na kuwafanya vijana wengi kuwa wabunifu.

5. Kuanzishwa Kwa Elimu inayoendana na uhalisia wa maisha.
Elimu kama vile Sanaa ya maisha, Elimu ya fedha na mendeleo binafsi maishani itakuwa nyenzo kuu wa Tanzania kufanikiwa sana katika uchumi binafsi na taifa Kwa ujumla. Mfano kuanzishwa Kwa mitaala ya Sanaa na jinsi ya kutumia vipaji vyao katika kuajiri badala ya kutegemea serikali tu, Elimu ya fedha jinsi ya kutunza fedha kuzalisha fedha na kujua fedha ilipojificha itasaidia sana wanafunzi kuwa na ujuzi na maarifa mbalimbali Hali inayopelekea kuepuka baadhi ya makosa yatayowafanya wajute baadae. Lakini kubwa zaidi itawasogeza katika nidhamu binafsi ya maisha na malengo Yao Kwa ujumla Kwa maana Kwa taifa jema tunapaswa kuwa na Uwajibikaji Mzuri sisi na Kwa wengine na sio kusoma na kujifunza mambo yasiyohusiana na maisha halisi Kwa asilia kubwa.

Hivyo basi, kama Sekta ya Elimu inapaswa kuwajibika vema Kwa Maendeleo ya Elimu Bora. Pia kama Sekta ya Elimu inapaswa kuwajibika vilivyo Kwa Elimu ya uwezeshwaji Kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kama vile kuwapatia vifaa maalumu kulingana na mahitaji Yao kama vile baisikeli, miwani na kofia Kwa albino pamoja na vifaa vya kusomea kama tablet. Ni kweli usiopingika, wanafunzi wenye mahitaji maalumu wanapata shida sana kwenye suala ya Elimu ivo kama serikali inapaswa kuwakumbuka na kuwa na utekelezaji Mzuri juu Yao. Pia kuwezeshwa Kwa mahitaji maalumu mashuleni kama vile chakula Cha mchana shuleni, taulo za kike na uboreshwaji wa miundombinu hasa sehemu za vijijini itasaidia wanafunzi wengi kuwa shuleni Kwa muda husika na kutowafanya wengi wao kukosa vipindi Hali itayopelekea ufaulu mkubwa Kwa Maendeleo Bora ya Elimu.
 
Upvote 4

Sawa kiasi, sema nn mwananguu: hii labda kama ni hatua ya mwisho kabisa maana bado video sio sawa na kuwepo kifizikia. Na pia elimu ya vitendo kuitazama kwa video, inabakia kuwa elimu ya nadharia - nadharia yenye rangi zaidi lakini bado ni nadharia tu

Elimu ya sekondari tayari anakuwa na ujuzi wa ujasiliamali katika Sekta mbalimbali mfano ufundi mwashi, bomba, ushonaji wa nguo
Elimu ya kujitegemea ili aweze kutegemewa na kutegemeka pia, saafi
Elimu kama vile Sanaa ya maisha, Elimu ya fedha na mendeleo binafsi maishani itakuwa nyenzo kuu wa Tanzania kufanikiwa sana katika uchumi binafsi na taifa Kwa ujumla.
Mada yako nzuri, pointi nzuri kwa kweli. Asante
.
 
Mkuu serikali hii ina tofauti gani na serikali zilizopita?
 
Back
Top Bottom