Naipongeza serikali kwa ujenzi wa reli ya kisasa,pia kwa kuona kuwa hatuwezi kuendesha reli ya kisasa bila kuwa na umeme wa uhakika na wakaona wajenge Bwawa kubwa la maji la Mwl.Nyerere kwa ajili ya kuzalishia umeme sababu umeme tuliokuwa nao usingetosha kwa matumizi na kwa ajili ya kuendeshea treni ya umeme.
Iwapo gharama za nauli zitazingatia vipato vya wananchi na kusimamiwa ipasavyo reli hii itakuwa kivutio kikubwa kwa wananchi kama njia mbadala ya kusafiria badala ya mabasi/magari hasa kutokana na wakati huu tukikabiliwa na ongezeko la mafuta ambalo hupelekea gharama za nauli kupanda, kutokana na reli hii kutumia muda mchache na usalama wa safari, hivyo serikali kupata mapato hivyo shirika la reli kujiendesha kwa faida .Hii itapelekea wasafiri wa barabara hasa abiria kupungua kwenye maeneo ambapo reli hii inapita hivyo kupunguza ajali za barabarani.

Upvote
2