MURUSI
JF-Expert Member
- Jun 25, 2013
- 4,537
- 8,824
Kuwe na 50 kwa 50 kati ya miradi ya maendeleo ya watu na miradi ya maendeleo ya vitu ili kupunguza umaskini wa vipato.
Tanzania ni moja ya nchi zinazo kuja juu sana kwa swala zima la ukuaji wa uchumi, na hii inachochoewa na kasi ya maendeleo hasa hasa miundo mbinu, Tuna miradi mingi sana ya miundo mbinu sehemu mbalimbali za nchi, kama Vile reli ya SGR, Madaraja, Meli, Vijwanja vya ndege na kadhalika.
Ila ukwel ni kwamba takwimu za ukuaji wa Uchumi hazijawahi kwenda sawa sawa na maisha ya watu, takwimu za ukuaji wa uchumi au hata ukuaji wa pato la Taifa hazi akisi maisha ya watu. Bado kuna umaikin mkubwa sana Tanzania hii.
Umasikini ni nini? Umasikini ni hali ya ukosefu wa mahitaji ya msingi kama vla Chakula, maji salama na safi, huduma ya afya,mavazi hivi vyote vinasbabishwa na mtu kuto kuwa na uwezo wa kuvipata au kuvinunua kutokana na kuto kuwa na kipato.
Maendeleo ya vitu ni yapi? Kwangu mimi maendeleo ya vitu ni maendeleo yanayo fanywa na Serikali ambayo sana yanalenga katika miundo mbinu, ujenzi wa Madaraja, Barabara,Reli, Meli, ununuaji wa Ndege, Magari ya kifahari na kadhalika hii yote ni maendeleo ya vitu. Haya hufaidi wachache sana, na kundi kubwa hubakia kuwa watazamaji tu.
Maendeleo ya watu ni yapi? Haya kwangu mimi ni maendeleo ya mtu mmoja mmoja hasa katika Nyanja ya kipato, Kipato ndio kila kitu, Mtu akisha kuwa na kipato hakuna kitakacho mshinda kufanya, ataweza kununua chakula, atapata maji afi na salama, atanunua mavazi, atalala sehemu nzuri.
Kwanini tuna maendeleo ya vitu na hayo maeneo bado kuna umasikini mkubwa?
Ukitembea sehemu nyingi za Tanzania, utakuta kweli kuna miradi mikubwa mikubwa inaendelea pale ila pembeni yake utaona kabisa hali za maisha ya watu ni mbaya sana, miradi mikubwa inaendelea ila unakutana na umaiskini mkubwa sana, unakutana na watu walio kata tama nahii ni kwa sababu hakuna miradi ya maendeleo ya watu bali kuna miradi tu ya maendeleo ya vitu.
Mfano, Ujenzi wa SGR, huu ni mradi mkubwa sana, unajengwa unapita maeneo tofauti tofauti, ila ukweli ni kwamba SGR haiwezi ondoa umasikini wa wa watu kama wale watu hawajawezeshwa kuwa na miradi ya kuwaondeleo umasikini, kuna sehemu nyingi za nchi hii kuna Barabara nzuri, Madaraja, umeme lakini kuna umsakini mkubwa sana tena umasikini wa kutisha, sababu kuu ni kwamba jamii ile bado haijawezeshwa.
Maendeleo ya watu yanafananaje? Maendeleo ya watu ni maendeleo yanayo gusa moja kwa moja mtu mmoja mmoja, hasa kwenye nyanja ya kipato, Mfano wa maendeleo ya watu ni kama vile Miradi ya Kilimo kwenye jamiii, inayo gusa watu mmoja kwa mmoja, miradi ya ufugaji kuku, Samaki, Ng’ombe na mifugo mingine, hii inawagusa watu moja kwa mmoja, Miradi ya viwanda vidogo vidogo kulingana na kile wanacho zalisha ile jamii, Mfano Kigoma wanalima Mawese ila hakujawahi kuwepo na kiwanda cha maana cha kuchakata mafuta ya mawese,Kuna maeneo ni wasusi wa vikapu, hakujawahi kuwepo na kiwanda cha kuwawezesha kususa kwa ubora na kuuza hata nje ya nchi.
Kuna maeneo wanalima matunda, Ila hakujawahi kuwa na kiwanda au viwanda vidogo vidogo vya wao kuchakata yale matunda yao kuliko kuyaacha yanaoza, mfano msimu wa Maembe. Hii ifano na mingine mingi inaweza saidia kuondoa umasikini wa vipato.
Kuondoa Umasikini wa Vipato kwa China, China pamoja na kuwa na idadi kubwa ya watu ila iko kwenye top 5 ya nchi zeney kasi kubwa ya kuondoa umasikini wa watu, China pamoja na kuwa na miradi ya vitu kule kwao ila wana miradi ya watu pia, China inaondoa umasikini kwa sababu inakuwa na miradi ya aina mbili, miradi ya vitu na miradi ya watu. China hadi sasa ina kadiriwa kuondoa umasikini wa vipato kwa wachina Milion 770, hii I tangu mipango ya Mao hadi sasa hivi.
Kilicho itesa Ethiopia muda mrefu sana ni kuwa na miradi mingi sana ya vitu bila kuwa na miradi ya kuwainua watu, ila sasa wameanza kuja na miradi ya watu ili kupunguza hata wimbi la kutorokea Africa kusini la Raia wao.
Tunaweza vipi kuondoa umasikini wa vipato kwa Tanzania au kuwa na miradi ya 50 kwa 50?
Tanzania tunaweza kuondoa umasikini wa watu kwa kuwa na miradi sambamba na miradi mikubwa inavyo tengewa pesa.

- Tuwe na Miradi ya watu ndani ya miradi ya vitu; Ujenzi wa SGR ulipaswa kwenye bajeti yake kuwemo pia na bajeti ya maendeleo ya waty kule inako pita, SGR ilipaswa kuwa yale maeneo inayo pita kuwe kuna maendeleo ya watu sio vitu tena, hii pia ingeweza kuisadia SGR yenyee kwa baadae katika swala zima la mizigo, hii sio kwa SGR pekee bali hata ujenzi wa Barabara za Lami, Madaraja makubwa na kadhalika,Bila hii tutashuhudia umasikini miaka na mika pamoja na kuwa na miundo mbinu mikubwa sana.
- Bajeti inayo somwa Dodoma iwe ina ainisha Pesa za miradi ya watu, miradi ya kuondoa umasikini, Mara zote Pale Dodoma, inasomwa bajeti za miradi ya vitu, utasikia ujenzi wa Daraja, umeme, karavati, Barabara na kadhalika, ila hakuna anaye kumbuka kuuliza kuna pesa ngapi imetengwa ya kwenda kwenye miradi ya watu mmoja kwa moja.Miradi ya watu inaachwa nyuma tukiamini kwamba tukisha maliza miradi ya vitu basi umasikini utapotea automatically kitu ambacho sio sahihi kabisa.
- Bunge lisipitishe mradi mkubwa wowote kama ndani yake hakuna bajeti ya miradi ya maendelo ya watu, hii iwe ni shariti namba moja la kupitisha mradi wowote mkubwa, hii itasaidia sana kuondoa kundi kubwa la watu au jamii kutok kwenye umasikini mkubwa sana, umasikini wa kutupwa.
- Miradi ya maendelo ya watu, izingatie kile ambacho watu wanakifanya maeneo yao na sio kuwapekekea miradi ambayo haihusiani na wanacho kifanya, hii pia imekuwa inafanyika sana Tanzania, kupelekea wananchi mradi amabo unakuwa hauna tija kwao. Mfano Jmaii inazalisha mafuta ya alzeti nyie mnawapelekea mradi wa Ssamaki, inawachanganya.
- Kila halimashauri ionyeshe ina bajeti kiasi gani inatenga kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya watu na kweli ionekene kwa macho ikitumika.
Upvote
1