UTANGULIZI
Nchini Ta nzania, tangu tupate Uhuru Mambo ya ukatili kwa watoto yamekuwa yakiripotiwa siku Hadi siku na vyombo mbailimbali vya habari. Ukatili umekuwa ukitokea kwa njia mbalimbali ikiwemo kimwili Kama vile ukatili wa kingono. Licha ya serikali kuweka Mambo mbalimbali kukabiliana na janga hili ikiwemo Sheria kali, Sera nzuri na uhamasishaji kupitia vyombo vya habari, bado tatizo ni kubwa na ukatili unaendelea kutendeka katika jamii.
Nini tatizo kwa nchi yetu?
Vitendo vingi vya ukatili vinatokea ndani ya jamii lakini taarifa zinazofika kwa serikali au vyombo husika ni chache kuliko idadi ya vitendo vinavyotokea ndani ya jamii.
Na Mara nyingi serikali imekuwa ikipata taarifa za ukatili pale ambapo mtoto ameshapata athari kubwa Kama vile:
✓mauaji yatokanayo na ukatili.
✓Madhara makubwa ya mtoto yasiweza kufichika Kama vile majereha na changamoto kubwa za kiafya.
Lakini vipo vitendo vingi vinavyofanyika ndani ya jamii havifiki kwa mamlaka husika na bado vinaendelea kutesa watoto.
TATATIZO KUU
Nchi yetu haijawa na mfumo mzuri wa jamii kuripoti ukatili kwa watoto.
Kwa Sasa jamii hairipoti ukatili ipasavyo kutokana na sababu kuu 4;
1. Vitendo vingi vya ukatili ni sehemu ya tamaduni ya jamii. Mfano ndoa za utotoni, hivyo ni ngumu kuletwa kwa vyombo husika na jamii yenyewe mpaka pale yatakapotokea matatuzo makubwa Kama vifo.
2. Rushwa.
Wapo watu wema waliowahi kuripoti lakini Cha kushangaza hakuna hatua yoyote inayochukuliwa kwa mhusika. Watendaji wa vyombo husika pamoja na baadhi ya watendaji wa jeshi la polisi wameifanya rushwa kuwa ni sehemu ya maisha, hivyo hata jamii inavunjika moyo na kuona hakuna faida yoyote ya kuripoti Kama wahusika hawachukuliwi hatua.
3. Hofu au kuogopa kuingia hatiani au kuogopa madhara baada ya kuripoti kwani watendaji wengi hawana uelewa wa Sheria za faragha na usiri wa mteja hasa ngazi za chini Kama serikali za mitaa. Hivyo unaweza kuripoti ukaangukia kwenye ugomvi.
4. Vyombo husika Kama polisi vinapungukiwa na lugha rafiki kwa wateja wao.
Mwananchi anaogopa kwenda polisi kuripoti kutokana na taarifa kuwa ukifika polisi kuanzia getini mpaka ofisini ukijichanganya kidogo tu unachukuliwa hatua. Hivyo mtu yuko radhi abaki na taarifa lakini sio kwenda polisi( no good customer care language).
SULUHISHO
SERIKALI IJENGE MFUMO WA KUPAMBANA NA UKATILI UKAOFANYA KAZI NDANI YA SEKTA YA ELIMU TANZANIA.
Ili kuweza kufikia angalau nusu ya ukatili unaotokea katika jamii serikali itanye yafuatayo kwenye sekta ya elimu:
WALIMU NA VIONGOZI WOTE NDANI YA SHULE ZOTE TANZANIA NGAZI ZOTE KUANZIA SHULE ZA CHEKECHEA HADI SEKONDARI WAFUNDISHWE JINSI YA KUTAMBUA NA KURIPOTI UKATILI.
Hii iende sambamba na mafunzo ya walimu waingiapo kazini pamoja na wawapo kazi( in-service training).
SABABU ZA KUTUMIA SEKTA YA ELIMU.
✓Watoto wengi walio kwenye hatari na wanaopata ukatili ni wale wa umri wa shule. Watoto miaka 4 hadi 17 asilimia kubwa wapo mashuleni. Hivyo ni rahisi kuwpata waliokwenye hatari ya ukatili na wanaokatiliwa Licha ya jamii kuwaficha.
✓walimu ndio kundi lililo karibu na watoto hawa kwa mda mrefu, takribani masaa 8 kila siku na miezi 9 kwa mwaka. Hivyo wakipewa maarifa juu ya ukatili mengi tutayapata.
✓Jamii inaficha ukatili kwa sababu baadhi yake ni sehemu ya tamaduni zake za kawaida, hivyo ni ngumu kupata tukitegemea jamii watokako watoto.
KWANINI WALIMU WA SASA HAWARIPOTI KWA UFANISI LICHA YA KUWEPO KAMPENI ZA KUKOMESHA UKATILI?
1. Walimu wote wa Sasa na wa zamani hawana maarifa ya kutosha Kuhusu viashiria vya mtoto anayepata ukatili na aliyekwenye hatari ya ukatili hivyo ndio sababu ya ukimya was.
2. Hakuna utaratibu bayana wa kuripoti ukatili mbali na namba za mamlaka husika ambazo hazijaleta ufanisi miaka mingi.
3. Hofu ya kutoa taarifa isiyo sahihi. " What if I'm wrong"? Kuogopa kuwa hatiani.
PENDEKEZO JUU MAFUNZO YA WALIMU
Walimu wapewe mafunzo kabla na wakati wakiwa kazini ( pre and in-service training).
1. Namna bora ya kutambua viashiria vya ukatili kwa watoto. Hii itasaidia kupata kupata taarifa nyingi kwa sababu watoto wote walipo shuleni, kwa sababu walimu wapo nao karibu mda wote itakuwa rahisi kumtambua mtoto aliyepo kwenye ukatili.
2. Wafundishwe na wapewe njia rafiki na rahisi ya kuripoti ukatili hasa njia kidigitali.
SERIKALI ITENGENEZE MFUMO WA KIDIGITALI UTAOWEZESHA WALIMU KURIPOTI UKATILI KWA TAARIFA TOSHELEZI NA KAMILIFU.
Mfumo wa Sasa ni wa kizamani, unatakiwa upige au uende ofisini kuelezea tukio ni njia ngumu na si rafiki
Kuwepo na mfumo mzuri wa kimtandao(MULTI-SECTORAL ONLINE APPLICATION SOFTWARE).
✓Mfumo huu uwe umeunganishwa na taasisi mbalimbali zinazohusika na watoto kama vile Polisi, wizara ya elimu na mahakama ili kuweka uwazi na kuepuka rushwa.
Walimu waweze kusajili vitendo vya ukatili na maelezo yake bila kuhitaji kuongea kwa mdomo.
Faragha ya taarifa za watoto na watoa taarifa zikuzwe kwenye mfumo huo.
HITIMISHO
Bila kuwa na mfumo mzuri wa kupata na kuripoti taarifa za ukatili hatuwezi kumaliza ukatili wa watoto. Tukianza na sekta ya elimu tutafanikiwa kwa kiwango fulani kwenda mbele kutoka hapa tulipo.

Upvote
4