SoC04 Tanzania Tuitakayo yenye Mfumo wa Serikali na si Chama

SoC04 Tanzania Tuitakayo yenye Mfumo wa Serikali na si Chama

Tanzania Tuitakayo competition threads

De Greate

New Member
Joined
Aug 27, 2022
Posts
2
Reaction score
0
Tanzania tuitakayo imebakia katika taswira ya vichwa vyetu. Hii ndio Tanzania tuliyonayo. Demokrasia katika nchi yangu sasa imekuwa ya kusadikika imebakia kuwa picha tu katika fikra zetu. Mifumo imekuwa na nguvu kuliko Maamuzi yetu.

Uongozi katika dhana ya demokrasia ni lazima uwe mfumo unaogeme watu wote na kutekeleza maslahi mapana ya Taifa. Uwazi na uwajibikani ni nguzo ya demokrasia kama itajwavyo katika vitabu lakini sina uwakika sana katika nchi yangu.

Hatuwezi kusema mfumo wa serekali ni wakidemokrasia kama maamuzi na machaguzi ya watu hayatapewa vipaumbele. Mchakato wa uchaguzi huru na wakidemokrasia unatakiwa kuegemea maslahi mapana ya raia na si itikadi na mifumo ya upande fulani wenye nguvu. Zaidi sana uwazi na uwajibikaji ndio nguzo za demokrasi yenye kuleta maendelo.

Tumekuwa na sifa ya demokrasi ya vyama vingi tangu 1992 na imepelekea kuwepo na uchaguzi na uhuru wa wananchi kuamua nani awe kiongozi hapa nchini. Ni shauku ya kila Mtanzania kuona kuwa mawazo yake yanaheshimika na mfumo wa uongozi wanao unataka unatendeka. Mungu akijalia mwakani tunaelekea uchaguzi mkuu ni matamanio ya kila Mtanzania kuona changamoto ya vyama vingi na kupata viongozi bora na si viongozi wa mfumo.

Mifumo imeathiri sana serekali kiasi cha kusikia mtu anasema serekali ya chama fulani au ilani ya chama fulani ndio mwongozo wa mifumo mingi ya maamuzi ndani ya Taifa. Nazani si jambo baya lakini, Je maslahi mapana ya Watanzania wenye vyama vingi na demokrasia ya maamuzi yanalindwajwe na mfumo wa maamuzi ya chama chenye nguvu ya kuadhiri mfumo mzima wa maamuzi ya serekali?. Je Demokrasi yetu hairuhusu changamoto ya kuunda serekali isiyo na uchama?

Si lengi kusisitiza maswala ya chama na ubaguzi ila nawasilisha matamanio ya kuwa na serekali ya wananchi yenye viongozi wawakilishi wa wananchi wenye nia ya kulinda maslahi ya Taifa na watu na si chama au itikadi. Je hatuwezi kuvua viatu vya chama na kuvaa viatu vya serekali yaani kuwatumikia wananchi? Nazani tunalemewa sana na viongozi wano vaa viatu vya chama pamoja na serekali kwa wakati mmoja.

Je, hatuwezi kupeperusha bendera ya Taifa katika magari ambayo yamenunuliwa kwa pesa za wananchi nakuacha kupeperusha bendera ya chama? Natanguliza kusema naipenda Tanzania naipenda nchi yangu. Picha ya nchi tuitamaniyo imebakia kwenye fikra tu. Nawaza na kutamani uchaguzi wa 2025 ukatusaidie kufumbua fumbo hili.

Ni miaka kadhaa sasa tuna chombo cha kujadili sera na kuwakilisha wananchi katika maamuzi ya Serikali. Lakini kutokana na mfumo unaogemea upande mmoja wenye nguvu ya kuathiri maamuzi ya serekali. Basi maslahi mapana ya Watanzania wenye kuamini katika uwakilishi na mifumo ya vyama vingi yamebakia kuwa shauku tu. Nadhani simulizi hii inaelezea jinamizi tulilo nalo kwenye nchi hii. Chombo hicho sasa kimebakia kutekeleza ilani na maslahi ya upande fulani. Je mipango mikakati ya Taifa kwa miaka mitano ( Five Years Development Plan) haitoshi au haikidhi kutoa dira ya maendeleo Mpaka tutumie ilani ya chama?

Sasa imekuwa kawaida kusikia ikitajwa serekali ya chama fulani. Ni mifumo imetufanya kuegemea upande mmoja. Si dhambi ila maslahi ya watu wote yanalindwa. Jinamizi la upigaji kutokana na report ya mkaguzi wetu je Watuhumiwa wameshughulikiwa?. Naipenda nchi yangu naipenda amani tuliyo nayo ni maombi yangu Mungu atupe amani na kuzidi tunapo elekea uchaguzi ujao.

Maswala ya uwazi na uwajibikaji tumefikia wapi nazani imetufanya kufa ganzi na kuacha kufuatilia tena taarifa za utekelezaji na uwajibikaji wa wawakilishi wetu. Ningepata muda wa kuzungumza na viongozi ninge wakumbusha kuwa wao ni Watanzania na ni wawakilishi wa Watanzania wasisahau ilo. Sina uwakika kama wanakumbuka tena tunasubiria kuwaona majimboni na ahadi hewa ifikapo wakati wa uchaguzi.

Nawaza kama tutaweza kupata bahati katiks uchaguzi ujao kuwa na Tanzania tuitakayo ambayo imebakia katika vichwa na fikra zetu. Naomba sauti zetu zipae kufikia ngazi walizoko wakumbusheni kuhusu Tanzania tuitakayo:

1. Tanzania itakayo heshimu uchaguzi na kutupa viongozi tunaowachagua.

2.Tanzania yenye chombo cha uwakilishi na si mfumo wa kujadili na kutekeleza ilani za upande mmoja ili kulinda maslahi mapana ya upande mmoja na kukita mizizi ya utawala badala ya Uongozi. Labda nikumbushie utawala na uongozi ni tofauti.

Nimekumbuka si ngonjera naandika ila ni maudhui ya Tanzania niitamaniyo.

3. Tanzania yenye kuteuwa viongozi (wakati wa uteuzi) kwa kuangazia matwaka ya wananchi na sifa za kiongozi na si itikadi na maamuzi ya upande mmoja.

4.Tanzania yenye kuwajibisha kila atakayekosea bila kujali cheo, hadhi, nafasi au itikadi ya upande mmoja. Nawaza kwanini mtu aboronge badala ya kuwajibishwa anahamishwa. Nazani kuna Tanzania nyingine tunaitaka na siyo hii.

5.Tanzania yenye serekali ya watu na si serekali ya chama. Tanzania itakayothamini uzalendo na maslahi ya wananchi zaidi ya siasa na itikadi za chama.

6. Tanzania inayo pambana na rushwa na kuwajibisha kila mtu bila kujali chochote. Maana mkaguzi wetu huweka bayana waovu lakini kelele nyingi watapelekewa wadogo kama matrafiki, n.k kuhusu rushwa ile hali kuna Mabilioni yamebadhirishwa na kila mwaka wimbo wa mkaguzi wetu umekuwa "unanswered cries"

7. Nazani tunataka Tanzania yenye uzalishaji wa ndani, uwekezaji na uwajibikaji katika matumizi ya fedha ili kupunguza deni la Taifa na kuongeza kipato cha ndani

Nazani sipo ndotoni ila mawazo yangu yananionyesha Tanzania ya kusadikika ambayo kama kweli tutaweka uzalendo mbele na kuheshimu Demokrasia ya kweli tutakuwa na Tanzania niliyoitaja awali. Usawa, uwazi na uwajibikaji ukitumika kujenga uongozi wa mwaka 2025 nazani tutakuwa na Tanzania hii

1.Tutakuwa na kasi ya maendeleo na ustawi

2.Tutapunguza deni la Taifa na kutokomeza jinamizi la kodi linalowakandamiza wananchi.

3. Kilio cha umaskini kitakuwa historia pia maisha ya wananchi yataboreka na usawa utakuwepo

4. Kuongeza uzalishaji wa ndani na kupunguza utegemezi

5. Demokrasia itakuwa si maono tena bali maisha halisi ndani ya Taifa.

Ndugu msomaji, Nisisitize tuendelee kuilinda amani tuliyo nayo, tuyatunze mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi, tuheshimu usawa na haki kwani kila mmoja ni Mtanzania na mwisho Tusiache kujiandaa na uchaguzi wa 2025 tuweke chuki pembeni tushiriki kampeni na kupiga kura ili kujenga Tanzania ya maono yetu.
thinking-emoticon-vector-225909.jpg
 
Upvote 2
Mifumo imeathiri sana serekali kiasi cha kusikia mtu anasema serekali ya chama fulani au ilani ya chama fulani ndio mwongozo wa mifumo mingi ya maamuzi ndani ya Taifa. Nazani si jambo baya lakini, Je maslahi mapana ya Watanzania wenye vyama vingi na demokrasia ya maamuzi yanalindwajwe na mfumo wa maamuzi ya chama chenye nguvu ya kuadhiri mfumo mzima wa maamuzi ya serekali?. Je Demokrasi yetu hairuhusu changamoto ya kuunda serekali isiyo na uchama?
Swali, gumu hili. Gumu sana.


Ndugu msomaji, Nisisitize tuendelee kuilinda amani tuliyo nayo, tuyatunze mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi, tuheshimu usawa na haki kwani kila mmoja ni Mtanzania na mwisho Tusiache kujiandaa na uchaguzi wa 2025 tuweke chuki pembeni tushiriki kampeni na kupiga kura ili kujenga Tanzania ya maono yetu.
Tanzania yenye vyama vingi vinavyojenga Taifa moja. Demokrasia👊
 
Back
Top Bottom