Tanzania Tulikuwa salama zaidi Mikononi mwa Ujamaa kuliko Tulivyo sasa Mikononi mwa Ubepari/Ubeberu

Serikali ina mambo mengi so haiwezi handle kila kitu. Hata timu za mpira tu hazifanyi kila kitu zenyewe jezi zinatengenezwa na Adidas, marketing inafanywa na digital companies, management inafanywa na Elliot companies sijui merchandise inafanywa na Spotify huko. Maana yake ni kwamba kila mtu aki specialise on what he does better ndio maendeleo yataonekana.

Otherwise serikali iendeshwe kwa mfumo wa Bodi yaani Rais anapewa KPI na kila mwaka inakua reviewed aki underperform shareholders wanamuondoa!! Hili haliwezekani hivyo basi hakuna haja ya serikali kuhodhi uchumi maana hakuna uwajibikaji kama uliopo private sector. Vodacom iliposhuka tu faida walipunguza wafanyakazi maelfu hakuna utani ila NIDA ina underperform ndio kwanza wanaongezewa mishahara na posho.
 
Nadhani sasa naelewa tofauti yetu hasa ipo wapi.
Wewe bado ukpo 'trapped' kwenye mifumo, kijamaa/socialist, communist versus capitalism. Mimi nilishaondoka huko siku nyingi sana.
Sijali sana nani analeta mapadiliko katika maisha ya wananchi wetu, ili mradi anafanya hivyo kwa haki na maslahi ya kila upande.

Serikali huwezi kusema ina 'limitations' za kufanya mambo, kwani serikali ni ya wananchi wenyewe.

Wewe bado unang'ang'ania nadharia za vitabuni, kama unavyo zieleza hapa, kuamini kwamba serikali haiwezi kufanya mambo kwa niaba ya wananchi na ikayafanya kwa ufanisi; kwa sababu tu ya nadharia unazosoma vitabuni, na kutoa mifano ambayo ni dhahiri kabisa ni utendaji mbovu na siyo kwa sababu za kukosa uwezo wa kufanya vizuri.
Wewe kila suluhisho la matatizo unaliona kwenye sekta binafsi, na huku ukisahau kabisa kwamba ufanisi kwenye sekta binafsi unatokana na yanayofanywa serikalini kwenyewe. Kama serikali inaamua kuharibu mashirika yake yenyewe au ishirikiane na sekta binasfi hiyo hiyo kuharibu mashirika yake, hilo linakuwa ni sababu ya kusema serikali haina uwezo wa kuendesha mashirika kwa ufanisi!

Hizi ni kasumba tu.

Hiyo mifano ya mashirika ya kimarekani yanayofanya biashara au kutengeneza silaha uliyoyatolea mfano hapo, utayatofautisha vipi na serikali za nchi hiyo? hawa ni sawasawa tu na kuwa waajiriwa wa serikali yenyewe, pamoja na kuwa na muundo wa kampuni.

Ninachosisitiza hapa, achana na ushabiki wa mifumo kinadharia. Tanzama mazingira ya nchi yako na amua kufanya yanayohitajika kwa manufaa ya nchi bila kujali hiyo mifumo unayojifunza vitabuni.
 
Sasa hivi hii nchi si ya Nyerere tena bali ni ya mimi, wewe na watanzania wengine wanaoipenda nchi yao...wanaotaka Tanzania iwe urithi mwema kwa vizazi vijavyo kama Mwalimu alivyotamani.
 
Nilichokiona hapa ni kwamba watu wengi hawafahamu kuhusu hii mifumo ya kiuchumi kati ya ujamaa na Ubepari, watu wanasema ila wanaogonzwa na Taarifa finyu juu ya mifumo hii ya kiuchumi.

Unasema Ujamaa ulishindwa na Ubepari au Ubeberu ni njia sahihi ya kiuchumi na hasa kwa watu maskini kama hapa Afrika?

Ujamaa ulishindwa wapi na Ubepari umeshinda wapi?

Tangu tulipoamua kuzivaa sera za Kiuchumi za Ki-liberali au Ki-bepari tumenufaika nini kama Nchi?
Umaskini imepotea?

Tupo wapi kama Nchi baada ya kuachana na sera za Kijamaa?
Je CCM imeachana na sera hizo za ujamaa na kujitegemea?

Ni kwamba tumekuwa makasuku wa mifumo kandamizi na katili ya Magharibi na sasa tunataka kufikiri kama watu wa Magharibi na mifumo yao hovu na kandamizi dhidi ya maskini waliyo wengi!

Tunaongoza na kufikiri kama Wazungu tukiwaona wao ndiyo ALFA na OMEGA wa kila kitu hapa Duniani huku sisi tukisahua uwezo wetu wa kiasili katika mambo mengi!!

Hiko hivi, ujamaa ni njia bora ya kuunganisha watu, kujikomboa kiuchumi na kuunda Taifa lisilo migawanyiko ya kimagharibi. Ujamaa unaosemwa ulishindwa ni kwa sababu ya propaganda za Magharibi zikiongozwa na Marekani na rafiki yake Uingereza. Tangu tuachane na sseraza kiuchumi za Kijamaa Taifa limekuwa maskini na watu wamekuwa fukara kwa sababu mfumo wa kibeberu una tabia nyingi za kuunda na kupendelea wachache kumiliki na kutumia rasilimali za wengi ili kujinufaisha.

Tuseme Ubepari umetusaidia, kivipi? kipi kimekuwa bora kwenye mfumo wa kibeberu?

Wakati wa Magufuli tulishuhudia Mapinduzi makubwa ya kiuchumi ni wachache walafi na wezi wanaona kuwa kipindi hiki tulikuwa vibaya kama Nchi, wachache hasa mawakala wa Ubeberu walichukia kwa sababu Magufuli aliileta Nchi katika mfumo halisi wa Ujamaa na kujitegemea.
 
Ujamaa ni sera ya kipumbavu ndiyo maana hata Nyerere alishindwa akangatuka madarakani
 
Ni vizuri tukaangalia Mazingira yetu kama Nchi baadala ya kushabikia mifumo kandamizi dhidi ya waliyo wengi. Kuendelea kuwa makasuku wa Magharibi haiwezi kutusaidia chochote.
 
Ujamaa ndio umeifikisha nchi kwenye umasikini , uvivu na uoga wa kipuuzi.

Angalia top 10 ya mega economies uniambie wapi socialists wapo.

Utasema uchina ila kimsingi uchina wana ubepari sio ujamaa.
 
Ujamaa au Ubepari hauna ubaya kwa ujumla wake. Tatizo ni umasikini wa fikra wa wananchi.
Matokeo ya fikra hizo za kimasikini, viongozi ambao ni sehemu ya wananchi hutunga husimamia sera na sheria kwa umasikini huo huo wa fikra na matokeo yake ni wageni kufaidi nchi zao.
Kinachotakiwa ni mapinduzi ya fikra, wananchi wajue kwamba wanaweza kuwashughulikia viongozi wajinga ambao ni vibaraka wa wageni, pamoja na wageni wenyewe ili wananchi wamiliki uchumi na kuendeleza nchi yao. Kwa sababu ya utandawazi, hakuna sababu ya nchi za Africa kuwa masikini tena, yatakaiwa miaka ijayo ziwe tajiri kuliko ulaya kwa sababu ya raslimali tulizo nazo.
 
Ujamaa ndio umeifikisha nchi kwenye umasikini , uvivu na uoga wa kipuuzi.

Angalia top 10 ya mega economies uniambie wapi socialists wapo.

Utasema uchina ila kimsingi uchina wana ubepari sio ujamaa.
kasome historia vzr.
kinachougharimu ujamaa mara zote huwa ni hujuma toka kwa mabepari/mabeberu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…