Serikali ina mambo mengi so haiwezi handle kila kitu. Hata timu za mpira tu hazifanyi kila kitu zenyewe jezi zinatengenezwa na Adidas, marketing inafanywa na digital companies, management inafanywa na Elliot companies sijui merchandise inafanywa na Spotify huko. Maana yake ni kwamba kila mtu aki specialise on what he does better ndio maendeleo yataonekana.
Otherwise serikali iendeshwe kwa mfumo wa Bodi yaani Rais anapewa KPI na kila mwaka inakua reviewed aki underperform shareholders wanamuondoa!! Hili haliwezekani hivyo basi hakuna haja ya serikali kuhodhi uchumi maana hakuna uwajibikaji kama uliopo private sector. Vodacom iliposhuka tu faida walipunguza wafanyakazi maelfu hakuna utani ila NIDA ina underperform ndio kwanza wanaongezewa mishahara na posho.
Nadhani sasa naelewa tofauti yetu hasa ipo wapi.
Wewe bado ukpo 'trapped' kwenye mifumo, kijamaa/socialist, communist versus capitalism. Mimi nilishaondoka huko siku nyingi sana.
Sijali sana nani analeta mapadiliko katika maisha ya wananchi wetu, ili mradi anafanya hivyo kwa haki na maslahi ya kila upande.
Serikali huwezi kusema ina 'limitations' za kufanya mambo, kwani serikali ni ya wananchi wenyewe.
Wewe bado unang'ang'ania nadharia za vitabuni, kama unavyo zieleza hapa, kuamini kwamba serikali haiwezi kufanya mambo kwa niaba ya wananchi na ikayafanya kwa ufanisi; kwa sababu tu ya nadharia unazosoma vitabuni, na kutoa mifano ambayo ni dhahiri kabisa ni utendaji mbovu na siyo kwa sababu za kukosa uwezo wa kufanya vizuri.
Wewe kila suluhisho la matatizo unaliona kwenye sekta binafsi, na huku ukisahau kabisa kwamba ufanisi kwenye sekta binafsi unatokana na yanayofanywa serikalini kwenyewe. Kama serikali inaamua kuharibu mashirika yake yenyewe au ishirikiane na sekta binasfi hiyo hiyo kuharibu mashirika yake, hilo linakuwa ni sababu ya kusema serikali haina uwezo wa kuendesha mashirika kwa ufanisi!
Hizi ni kasumba tu.
Hiyo mifano ya mashirika ya kimarekani yanayofanya biashara au kutengeneza silaha uliyoyatolea mfano hapo, utayatofautisha vipi na serikali za nchi hiyo? hawa ni sawasawa tu na kuwa waajiriwa wa serikali yenyewe, pamoja na kuwa na muundo wa kampuni.
Ninachosisitiza hapa, achana na ushabiki wa mifumo kinadharia. Tanzama mazingira ya nchi yako na amua kufanya yanayohitajika kwa manufaa ya nchi bila kujali hiyo mifumo unayojifunza vitabuni.