Tanzania tuna amani ila uhuru wetu umebagazwa na kubanangwa

Tanzania tuna amani ila uhuru wetu umebagazwa na kubanangwa

Na mtu yeyote anayeshabikia CCM eidha chawa ni agent wa terrorism kwa hiyo tuna mtambua kama terrorist
Tatizo la wengi wenu mnaichukia ccm kiasi kwamba kila yoyote mwenye kuwaza tofauti basi atakuwa ccm

Kwenu nyinyi mtu ambaye hayupo na nyie pamoja basi ni ccm,mnafeli sana mjue

Sisi wengine hatupo kichama hapa bali kwa maslahi ya wananchi wote
 
Ukiwa mwendawazimu siku zote utaongea kama mwendawazimu, wew upo kwa maslah ya mwananch yupi?
 
Tunataka haki ili tuone ni kwa namna gani itaondoa amani. Kama unaongelea amani kwa maana ya amani, huwezi kuonyesha haki ni hatari kwa amani. Ww unazungumzia madaraka bila kujali yanapatikana vipi, hivyo uko hapa kulinda madaraka ya viongozi majizi kwa kichaka cha amani. Ndio maana unasema wanaoikosoa serekali wanajiingiza matatizoni, maana unajua viongozi wa serekali hawatawali kwa haki, bali uoga, hivyo yoyote asiye muoga wanaweza kumpoteza.

Inshort hutetei amani kwa umuhimu wa amani, bali ni mtetea uovu unayepandikiza uoga. Zama zimebadilika mzee, na msipokubali kuwa zama zenu zimepita mtaaingiza nchi hii kwenye matatizo makubwa. Kama hamtakiwi si mkae pembeni, kwani lazima iwe nyie tu?
Sipo hapa kupandikiza uoga nipo hapa kuwaambia ukweli kwamba usipokaa mbali na matatizo utaliwa kichwa,je hili nalo ni geni hapa?

Kila siku mnalialia fulani katekwa sijui fulani kachukuliwa na wasiojulikana,kama nyie mnaweza pambana na hii hali kwa mabavu mbona hampambani na kuikomesha? Hamuwezi kwakuwa dola ina nguvu zaidi yenu

Narudia mara nyingi kusema
Hamtaweza kuiangusha serikali maadamu vyombo vya ulinzi na usalama vipo upande wa serikali,iwakae vichwani mwenu

Haki haiwezi kuitangulia amani,kwahiyo ni ndoto za Alinacha eti ujaribu kufanya kinyume chake
 
Kuna tofauti kati ya aman na utulivu.
Hii nchi ilitakiwa iwe bora zaidi ya hapa..
Ukikutana na waafrika takataka ambao wamewahi kuitembelea Tanzania wanaona tuna maisha bora sana. Pumbavu kabisa
 
Tatizo la wengi wenu mnaichukia ccm kiasi kwamba kila yoyote mwenye kuwaza tofauti basi atakuwa ccm

Kwenu nyinyi mtu ambaye hayupo na nyie pamoja basi ni ccm,mnafeli sana mjue

Sisi wengine hatupo kichama hapa bali kwa maslahi ya wananchi wote
Kwa fikra zako hizo upo kwa masirahi ya mwanachi wa nyumbani kwako,watoto wako,na sio Watanzania wanao tekwa na kuuawa kila uchwao,
 
View attachment 3521700

My people,​

Kumekuwa bado na mijadala ya hapa na pale kuhusiana na je Tanzania kuna amani? Na wengine wakisema hakuna haki au wanasema haki kwanza,au amani ni tunda la haki

Haki huja baada ya amani kuwepo sehemu yoyote ile duniani,kwani uwepo wa amani ndio hufungua kurasa nyingine za mazungumzo na maelewano,mfano kinachoendelea leo pale Ukraine na Urusi ni vita na hakuna amani,kwa mazingira yale hakutakuwa na haki kwasababu haki ni zao la amani,vita visimame ndio wazungumze,kuona je Ukraine ana haki kama nchi huru kujiunga na Umoja wa Nato au kujiunga kwake anahatarisha usalama wa Urusi

Wote ni mashahidi baada ya vita ya siku 12 kati ya Iran na Israel,ili amani ipatikane,ilibidi wasimamishe vita na kufanya mazungumzo ya kusitisha vita na kuleta amani ndio kisha mambo mengine yaendelee

Hapana haki inayoweza kupiganiwa au kudaiwa kwenye mazingira ya vita,hakuna haki inayoweza kudaiwa kwenye mazingira ya fujo na vurugu,lazima kwanza pawepo na Amani kisha mambo mengine ndio yafuatiye

Na amani ni moja ikiwepo utaona athari zake mara moja na amani isipokuwepo pia utaona athari mara moja,lakini haki ikiwepo au isipokuwepo huwezi ona athari yake mara moja kwasababu haki ni mjumuisho wa vipengele vingi au mambo mengi ambayo hayana athari ya moja kwa moja kama ambavyo amani ikiondoka utaona athari ya moja kwa moja

Mfano leo hii amani ya Tanzania ikiondoka mara moja,wote tutaathirika tupende tusipende,kwakuwa penye mazingira ya fujo na vurugu hakuna shughuli ambazo zitafanyika

Lakini inapokosekana haki ya kutoa maoni na mawazo ambayo hatuna sasa sio wote tunao athirika bali ni wale ambao wanadai haki hiyo tu ndio wanao athirika,mfano wanaotekwa wote ni wale ambao wanatoa mawazo yao na maoni yao dhidi ya Serikali, kwahiyo ukiwa mtulivu na kujua kujichunga na kujiweka mbali na matatizo utakuwa salama

Kwahiyo mpaka hapo tumeona kwamba Tanzania tuna amani na ndio maana shughuli zinaendelea kama kawaida,wanao lima wanalima,wanafabiashara wanafanya biashara zao na wanao beti wanabeti ingawa ni haramu,pamoja na kwamba kuna haki tunazikosa .

Tanzania hakuna uhuru wa kutoa maoni na mawazo,hakuna uhuru wa kuchagua viongozi tunao wataka,maana uhuru ni kujifanyia mambo yetu bila kubagazwa au kubanangwa

Na si kila haki yenye kugaiwa,mfano huwezi kudai haki ya kutambuliwa kwa mashoga hapa Tanzania,lakini bado utainjoy amani ya nchi hii,hakuna haki ya kutoa mawazo yako na maoni yako pasina kuchunga mipaka,kwasababu uhuru wako wa kutoa maoni na mawazo unaishia pale uhuru na haki ya wengine inapoanzia

Kwahiyo ndugu zangu watanzania, hapa Tanzania tuna amani na tuendelee kuilinda amani yetu kwani ni tunu kubwa sana basi tuilinde kwa wivu mkubwa sana

Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania

Ni hayo tu!
Amani inayohubiriwa na watawala na machawa Tanzania sio ya kweli, ni amani ya kukwepa uwajibikaji, ni amani ya vitisho, ni amani iliyojaa hofu ndani yake, ni amani ya kukaa kimya na kuacha mambo yaende tu. Watawala wanaogopa kuzungumzia haki kwa sababu hawako tayari kuitenda hiyo haki, haki ndo msingi wa amani, amani ni tunda la haki, haki inapokuwepo hakuna atakayeonewa, atakayedhulumiwa, nk, katika mazingira ya haki amani hutawala, katika mazingira ya amani hakuna guarantee ya haki kutawala, kama tulivyoona kwa miaka mingi iliyopita.
Na ukitaka kujua ni propaganda, waislamu siku zote wamekua wakisema uislamu ndo dini ya haki, sasa wameikana hiyo imani na kuanza kuimba uislamu dini ya amani.
Punguzeni uchawa kwenye mambo ya msingi yanayogusa maisha ya watu
 
Kuna tofauti kati ya aman na utulivu.
Hii nchi ilitakiwa iwe bora zaidi ya hapa..
Ukikutana na waafrika takataka ambao wamewahi kuitembelea Tanzania wanaona tuna maisha bora sana. Pumbavu kabisa
Nakubaliana na wewe kwamba hii nchi ingetakiwa iwe mfano wa kuigwa barani AFRKA kwa maendeleo

Mfano kama jiwe ndani ya miaka 5 tu aliweza kufanya mambo ambayo hayakufanywa kwa miaka 30 ya Marais waliopita,je hao watangulizi wake kama wangekuwa na kariba kama ya Jiwe,je nchi ingekuwa wapi?
 
Kwa fikra zako hizo upo kwa masirahi ya mwanachi wa nyumbani kwako,watoto wako,na sio Watanzania wanao tekwa na kuuawa kila uchwao,
Hahaha very funny, kwahiyo ili nionekane nina maslahi ya watanzania niwahamasishe kuandamana
 
Kwa fikra zako hizo upo kwa masirahi ya mwanachi wa nyumbani kwako,watoto wako,na sio Watanzania wanao tekwa na kuuawa kila uchwao,
Hahaha very funny, kwahiyo ili nionekane nina maslahi ya watanzania niwahamasishe kuandamama
Amani inayohubiriwa na watawala na machawa Tanzania sio ya kweli, ni amani ya kukwepa uwajibikaji, ni amani ya vitisho, ni amani iliyojaa hofu ndani yake, ni amani ya kukaa kimya na kuacha mambo yaende tu. Watawala wanaogopa kuzungumzia haki kwa sababu hawako tayari kuitenda hiyo haki, haki ndo msingi wa amani, amani ni tunda la haki, haki inapokuwepo hakuna atakayeonewa, atakayedhulumiwa, nk, katika mazingira ya haki amani hutawala, katika mazingira ya amani hakuna guarantee ya haki kutawala, kama tulivyoona kwa miaka mingi iliyopita.
Na ukitaka kujua ni propaganda, waislamu siku zote wamekua wakisema uislamu ndo dini ya haki, sasa wameikana hiyo imani na kuanza kuimba uislamu dini ya amani.
Punguzeni uchawa kwenye mambo ya msingi yanayogusa maisha ya watu
Sijui huwa mnaizungumzia amani katika muktadha gani?

Amani tunayo izungumzia kama nchi ni kutokuwepo kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe,uwepo wa fujo na vurugu na nchi kutotawalika

Sasa niambie je ikifikia hatua hii kuna haki unaweza kuipata au kuidai?

Uislamu ni dini ya amani,ndio maana salamu yake ni "AMANI IWE JUU YENU" Na hii ni salamu iliyotumiwa na manabii na mitume,hata Yesu aliitumia pia

Uislamu ni dini ya haki kwasababu kila haki ya mwanajamii inazingatiwa,hata kafiri ,jirani wote hao wana haki zako

Lakini kwanza ili jamii ikae kwa kuelewana n kusikilizana pmoja na kutambu haki ya kila mmoja wao kwanza AMANI IWEPO
 
Hahaha very funny, kwahiyo ili nionekane nina maslahi ya watanzania niwahamasishe kuandamama

Sijui huwa mnaizungumzia amani katika muktadha gani?

Amani tunayo izungumzia kama nchi ni kutokuwepo kwa vita ya wenyewe kwa wenyewe,uwepo wa fujo na vurugu na nchi kutotawalika

Sasa niambie je ikifikia hatua hii kuna haki unaweza kuipata au kuidai?

Uislamu ni dini ya amani,ndio maana salamu yake ni "AMANI IWE JUU YENU" Na hii ni salamu iliyotumiwa na manabii na mitume,hata Yesu aliitumia pia

Uislamu ni dini ya haki kwasababu kila haki ya mwanajamii inazingatiwa,hata kafiri ,jirani wote hao wana haki zako

Lakini kwanza ili jamii ikae kwa kuelewana n kusikilizana pmoja na kutambu haki ya kila mmoja wao kwanza AMANI IWEPO
Nchi hii haina amani kwa sababu hakuna haki. Huo ndo ukweli mchungu.
 
Inaonekana somo la history ulikuwa una dodge au tu ukiazi wako tu

Hivi mpaka leo hujui ni serikali ngapi duniani zenye dola kamili zimeangushwa na wananchi wake?!

Pimbi ni pimbi tu!
Hizo dola unazo sema zilianguka baada ya vyombo vya ulinzi na usalama kuwa upande wa wananchi

Baada ya vugu vugu la Arabian spring, yale maandamano mwanzoni yalipata upinzani kutoka vyombo ulinzi na usalama lakini wajeda wakaona hawana haja ya kuzidi kuua raia bure wakawa upande wa wananchi

Libya wananchi walikabiliwa Vikali na vyombo vya ulinzi na usalama mpaka pale jeshi la Nato lilipo ungana na wananchi kupiga jeshi la Gaddafi

Idd amini dada aliondolewa madarakani baada ya kupigwa na jeshi la Tanzania,kwahiyo msaada wa vyombo vya ulinzi na usalama vina mchango mkubwa sana

Naona serikali ikimaliza muda wake 2030 unless vyombo vya usalama viamue vinginevyo
 
Back
Top Bottom