Tanzania tuna walimu wa kufundisha Kifaransa, Kiarabu na Kichina? Walisomea wapi haya masomo?

Typo ya kibabe sana hiyo mkuu 🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️🏃🏿‍♂️
 
Ukisoma vizuri maelekezo ya TAMISEMI inaonekana wamejiandaa vizuri maana tahasusi hizo zimeelekezwa katika shule maalum ambazo wao ndiyo wamezichagua kwa ajili hiyo.

Lakini pia haitashangaza kama mpaka masomo yanaanza hakuna cha mwalimu wala vitabu. Hatujawahi kuwa siriazi na cho chote; na uzoefu wetu unaonyesha hivyo!🚮
 
Yule waziri wa elimu yule ni Professor lakini kuna walakini mkubwa sana.
 
Hao walimu wakufundisha hizo shule wapo ?
 
Walimu watapatikana tu wa kuunga unga kama walivyo wa kiingereza.
 
Wanafunzi watakutana na mtihani wa taifa tu nchi la hovyo hili.
 
Wapo wa kutosha wala hakuhitaji mjadala maana Udom na udsm wamejaa
 
mimi naona msingi sio walimu wa kufundisha hizo kozi, msingi ni wadau wapi walishirikishwa mpaka kufikia uamuzi huo? maana waziri na mkwewe wanakaa tu wanaamua nini cha kufanya kwa nchi. Masomo ambayo dunia inayathamini na kuyafundisha sasahivi sisi tunahangaika na malugha ya watu , na tunapoelekea huko usishangae tahasusi ya lugha ya mama kizimkazi nayo inakuwa kwenye mitaala, wazungu wanasema wanyime elimu na maarifa upate kuwatawala vizuri. SHAME.
 
Ni kweli kwamba dunia ya sasa ni ya teknolojia na upo sahihi kwamba serikali ingeyatilia mkazo masomo ya teknolojia.. lakini kuuliza kwamba walimu wa lugha hizo tatu wapo au hawapo ni swala la kushangaza Sana watu wanasoma kifaransa,kichina na kiarabu toka shule ya msingi hata Mimi ni mmoja wapo nilisoma kifaransa toka shule ya msingi mpka kidato cha pili nikasoma masomo ya sayansi form 3 mpk six ... Na kuhusu dini kwani hakuna vyuo vinavyo toa elimu ya THEOLOGY ? [emoji848] mbn vingi Tu mkuu ... Kiufupi umekurupuka ni Mambo ambayo yapo miaka na miaka sio kama yameanzishwa juz juz kama usemavyo
 
Watasambazwa nchi nzima kwenda kufundisha hizo shule ?

Wako wangapi ?
siala la kitakwimu hatubuni majibu,

walimu wapo na wanendelea kufundishwa maeneo mabalimabali kutokana na umuhimu na mahitaji ya nchi na dunia nzima...
 
Watanzania mnapenda kulalamika sana haswa kwa vitu vidogo
Nina msululuu wa marafiki kutoka pande mbali mbali za dunia kutoka katika GROUP za FACEBOOK wanakuja ama wengine wanafikikia kuja TANZANIA kujifunza kiswahili haswa wachina
Hivi unafikili kila mtu afanye TEHAMA unadhani DUNIA itaendelea hvyo

Mimi nawashauri VIJANA wengi kwa sasa watumie FACEBOOK kupata maarifa na marafiki kuna GROUP tofauti tofauti ambazo zitaongeza KNOWLEDGE yako kulingana na wewe mwenyewe unataka nini ama kujifunza nini
mimi napenda sana mambo ya ANCIENT hvyo nipo kwenye GROUP amabazo nakutana na watu kitoka mataifa mbalimbali amabao mataifa yao yameendelea au mengine yanaendele sana lkn hawana interest kabisa na TEHAMA hvyo mambo mengine kila mtu afanye analopendelea ndio maana hizo tahasusi zikanyambuliwa tofauti tofauti
Kuhusu walimu ni vile wewe sio interest zako ila walimu wapo hata ukitaka kujifunza Ancient Greek language KOINE wapo walimu
 
Ni nature ya mwanadamu kutokukubaliana na mabadiliko ila nazan tuwape mdu wa kuzoea lkn pia tujipe mda wa kujielimisha juu ya jambo hili
Serikal inawasomi na wataalamu weng sana na ndo walotumika kuandaa mitahara hii ebu tuwaamin wataalamu wetu
 
Hizi tahasusi za dini zilitakiwa ziachwe kwa madhehebu ya Dini yenyewe. Sioni tahasusi inayohusu dini za asili za waafrika au dini za kihindi . Je hawa wamebaguliwa? Mambo ya dini yasihusishwe na mitahala ("syllabus ") ya Wizara ya Elimu. Wahitimu wa dini watapata ajira wapi?Serikali haina dini!.
Hizo tahasusi za lugha ni kitu kizuri kwanza Tanzania imechelewa sana. Afrika ya kusini ilianza kufundisha Kichina kama miaka 20 iliyopita. Wachina ndio wawekezaji wakubwa nchini, wakiongea tuwaelewe wanasema nini? Wachina walijifunza kiswahili miaka mingi iliyopita , sasa wanakuja kuwekeza hadi vijijini.
 
Pleasure,ikimpendeza anaamua tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…