Tanzania tuna walimu wa kufundisha Kifaransa, Kiarabu na Kichina? Walisomea wapi haya masomo?

Tanzania tuna walimu wa kufundisha Kifaransa, Kiarabu na Kichina? Walisomea wapi haya masomo?

Wapo wengi sana.
Kuna walimu wa kichina, kiarabu, kifaransa, hata kihindi.......
Wabongo mmeanza kulalamika kama kawaida yenu.....uoga umewajaaaa... someni lugha zote wacheni ujinga.
 
Kwahiyo wote sasa tutaenda kurasini
alliance france na udsm wamejazana na kwakweli ni wazuri mno 🐒

kutokana na uhitaji kwa mazingira ya sasa, bila shaka vijana wengi watatumwa maeneo mbalimbali duniani kujifunza, na kwa muda mfup tutakua na wakufunzi wengi na wakutosha humu nchini🐒
 
Mbona UDSM, UDOM wanatoa hizo Kozi, nakumbuka Udom pale nilisoma kichina kidogo nikaacha, na wanafundisha wachina wenyewe.
 
kwahiyo nchi nzima wanafunzi tuwe tunaenda kurasini kuhudhuria vipindi cyo
hiyo ni sehemu moja tu,
udsm, alliance france & British council unapata huduma hiyo pia 🐒

hata hivyo,
kulingana na mahitaji kuongezeka bila shaka vijana wengi watatumwa maeneo mbalimbali duniani kujifunza mambo hayo ili kukidhi mahitaji 🐒
 
Nimeona taasusi mpya zilizotolewa na wizara ya elimu Tanzania. Naomba tusaidieni mawazo kama zinatekelezeka na zina tija kwa watoto wetu

1. Tuambieni waalimu wa lugha ya kiarabu, Kifaransa na Kichina tunao? Chuo gani cha ualimu kinafundisha haya masomo kwa ngazi ya degree? Nauliza degree kwa sababu mwalimu wa kidato cha tano lazima awe na degree.

2. Ni nani kati yetu amewahi kushirikishwa kutoa maoni kuhusu mabadiliko haya?

3. Je, wanaosoma dini watakwenda kusoma nini chuoni? Wataenda vyuo gani hapa nchni?

4. Dunia inakimbilia kwenye TEHAMA, kwanini mfumo huu umejikita zaidi nje ya TEHAMA?

5. Ni nchi gani Duniani ina Tahsusi za aina hii tulipokwenda kujifunza au tunarudia aliyoifanyia hii nchi Mungai wakati anapanga kuua elimu yetu huku elimu ya Kenya ikiwa inapanda?

6. Waalimu wa kufundisha dini tuliwaandaa katika vyuo gani?

Kwamba hizi tahasusi zimeridhiwa au zimeletwa kwa ajili ya maoni? Nchi ya viwanda, biashara na kilimo kweli itatoboa kwa mfumo wa elimu ambao hauungani kati ya primary, secondary na chuo?
umenena vyema yaani hadi hasira, hakika naona waarabu na islamic ndo kama walikalia kikao cha kupitisha hayo madubwana ya tahasusi ya hovyo,nilitegemea kuona electronics,telecom,coding,programing,syber security,IT,computer engineering,kama walivyo ichambua kiarabu kwa kila tahasusi badala yake wameweka tu kwenye kapu moja computer science yaani hii nchi kwenye teknoloji tutakwama sana,tutabakia tu kuongea kiarabu
 
Unasikitisha sana, Kuna wataalum wengi sana wa Lugha ya kiarabu nchini, Napia Lugha za kifaransa na kichina nazo wapo wataalamu wake, nahasa Zanzibar. Zanzibar mpaka watoto wadogo mitaani wanaongea Kitaliano
 
Tumeomba Walimu wa somo la Kiarabu kutoka makundi ya Al-Shaabab na ADF ya Congo. Nasikia wana Walimu wazuri sana kwa habari ya Kitabu kilichoandikwa Kiarabu.
 
umenena vyema yaani hadi hasira, hakika naona waarabu na islamic ndo kama walikalia kikao cha kupitisha hayo madubwana ya tahasusi ya hovyo,nilitegemea kuona electronics,telecom,coding,programing,syber security,IT,computer engineering,kama walivyo ichambua kiarabu kwa kila tahasusi badala yake wameweka tu kwenye kapu moja computer science yaani hii nchi kwenye teknoloji tutakwama sana,tutabakia tu kuongea kiarabu
Shida yako unawaza udini tu mdogo angu ila ukifikiria kwamba Arabic is the most spoken language in Africa, and comes in a list of twenty mostly spoken languages in the world huezi kutoa comment ya kijinga kama hii.
Honestly mimi nilikuwa nashangaa sana kwann hapa bongo watoto wanakomaa na lugha mbili tu Kiingereza na Kiswahili while kwa dunia ya sasa kujuwa zaidi ya lugha mbili ni fursa nzuri mno na ndio kwenda na wakati,
Shida wadogo zangu mnatumia hisia kuchambua mambo na sera za kibaguzi. I'm doing Electronics, communication and computing but it never stopped me from learning 3 languages apart from English in my extra time. Lugha ya kiarabu na warabu havina uhusiano na kuwa muislam nna marafiki wengi wakristo na wanajifunza lugha ya kiarabu, fungua ubongo ufikirie kma mtu aliyeelimika
 
Dunia ya sasa ni ya teckinolojia kunasoftware nyingi zinazotafsiri Lungha, na ikumbukwe lungha sio UJUZI, Ata mfaransa akija Tanzania ata hitaji IT,Food, Acc na wajuzi wengine. Tuna ndugu wengi wamesoma lungha hizo wapo hawazalishi na hawaajiriki zaidi parttime za ukarimani . Tungeanzisha tahasusi za ujuzi Wizara ya Kilimo na Ofisi ya Waziri Mkuu kila mwaka inapanga bajeti kusoma kilimo (BBT) na Ufundi Veta. Nadhani Combination zingeegemea kutoa ujuzi hii. Hiyo miaka miwili ya form 5 na 6 bora hao vijana tuwapele wakasome bure fani za kupaka rangi,ushonaji ,kufuga nyuki, kuchomerea,ujenzi,kilimo,kutengeneza simu ,kutengeneza pikipiki na Magari. Ingesaidia kujiajiri baada ya kuhitimu masomo yao.
Kaka umenitext wasap ila sijaweza kujib pm yako imefungwa
 
Back
Top Bottom