Tanzania tuna walimu wa kufundisha Kifaransa, Kiarabu na Kichina? Walisomea wapi haya masomo?

Well, una hoja nzuri sana Mkuu. Ingawa kwa maendeleo ya sayansi na teknolojia yaliyopo sasa kama vile Matumizi ya Walimu wa chache waliopo ikimuishwa na Matumizi ya IoT and Artificial Inteligence tunaweza kufundisha masomo hayo vizuri kabisa Mkuu. Shida itakuwa ni haya maumeme yetu yanayo katika kila dakika na hayajafika kila Kijiji.
 
Ndiyo maana Jeshi lilionya kuhusu hawa Watu wasio na Asili ya Tanzania. Huyu Mungai kwakweli hapaswi kuigwa kwa walichotufanyia kielimu kama Taifa kwa manufaa ya mataifa jirani.
 
Walimu wapo kuna course zipo udsm school of education ambapo chinese ni teaching subject, course za french zipo udom ila sijui kama ipo kwenye college yao ya education
Hizo computer science walimu wapo mashuleni ila tu hawafindishi hilo somo sababu ya miundombinu hairuhusu.
 
Hao walimu wakufundisha hizo shule wapo ?
Wanakosekana vipi na vyuo vipo. Wapo watu wako china kule wanafundisha hizo lugha. Wapo UK wapo South Africa. Na ni watanzania..
Nimetoa mfano posta pale wapo walimu wengi tu wa lugha wana degree kabisa.
 
Katika shule na vyuo vya watu waliopambazuka, lugha za kigeni zinasomwa kama minor. Yaani iwe ni interest yako tu kujifunza. Lakini huwezi kuwakuta wanacheza na ile elimu msingi inayoandaa nguvu kazi yenye ushindani
 
Kufundishwa vyuo vikuu shio shida. Haya masomo huwa yanakuwepo vyuo vikuu ili wale wenye kupenda waweze kusoma. Shida ni kuzifanya kuwa major courses. Yaani unaandaa hawa watu wamtumikie nani?

Nikupe mifano michache, ukiwa unatoka Mwenge kwenda Posta mita chache kabla ya kukaribia mataa ya Morroco kuna njia inaingia kushoto kabla ya jengo refu lililopakana na mataa yenyewe, pale vimewekwa vibao kadhaa vya kichina vikielekeza jambo fulani kwa lugha ya kichina. Sasa unajiuliza hivi vibao vilikusudia kumwelekeza nani? Vinaelekeza nini? Kwa nini asiweke kwa lugha mbili? Maswali ni mengi na hayakauki kichwani. Kwa hiyo usiyejua kichina imekula kwako. Vivyo hivyo hata kwenye hayo majengo ya msaada hapo chuo kikuu, ukifika pale school of confucius unaweza kudhani umeingia China, ni mwendo wa maandishi ya kichina tu kwenye kuta za majengo. Sasa unajiuliza wasomi waliotishwa na maandishi ya kichina chuo kikuu watatoka na ubongo wa kuweza kuwakabili wachina kwelikweli? Na pengine itakuja na misaada ya kufundisha tamaduni na lugha za kiarabu na kifaransa na majengo ya ufadhili yatajengwa tena kwenye vyuo vyetu hivi vikuu! Kwa mtindo huu tunaingiza uduni na ukoloni wenyewe kwenye vichwa vya watoto wetu.

Hatari kabisa.
 
Sijawahi kuona mwarabu au mchina amekuna kutalii, wafaransa sina tatizo wapo sn
Lugha hizo nilipokaa waarabu wapo wengii tu , wengine marafiki zangu .

Biashara za sasa unaweza kusoma china fresh maana sio wote wanajua kingereza, watanzania wanafanya biashara na wachina kuliko watu wengine
 
Lugha hizo nilipokaa waarabu wapo wengii tu , wengine marafiki zangu .

Biashara za sasa unaweza kusoma china fresh maana sio wote wanajua kingereza, watanzania wanafanya biashara na wachina kuliko watu wengine
Nimekuelewa
 
Kama nlivyosema wameamua kushusha chini ili knowledge waanze kuipata huku chini mkuu unavyosema kufundishwa chuoni sio issue kwani haya masomo mengine ya English n.k si wanafundishwa chuoni walimu then wanakuja kufundisha sekondari
 
Hayo makombi ni kupotezea tu isionekane dini imeingizwa, na ile dini ya pili imeingizwa kupoteza maboya tu. Ni abrakadabra tu imefanyika hapa wala hakuna tija. Mambo ya dini yana wenyewe wakafundishane huko. Nani anataka ajira ya kufundisha dini? Unaanzaje kuomba ajira msikitini/kanisani? Hii nchi si ya kidini katika mfumo wake wa serikali. Huko ni kumong'onyoa misingi imara iliyowekwa tangu kuasisiwa kwa taifa hili. Wakaona italalamikiwa sana wakachomeka divinity ili kubalansi mambo wakati ukweli ni kuingiza islamic knowledge huku ikishadidiwa na kiarabu kabisa ili dini hiyo itamalaki kwa mawanda katika taifa na mwisho wa siku itawale nyanja zote na iwe ndio mfumo wa taifa. Hakuna mwenye shida na abrakadabra na mambo ya dini nyakati hizi huko ni kuridhisha kundi fulani la wahafidhina wa dini ya kipuuzi ili tu waone wako kwenye hatamu nchini. Comb zingejikita kwenye masomo yenye tija, dini kila raia ana yake atafundishwa huko anakoabudu
 
Mama anaupiga mwingi! Nchi yaajabu hii
 
Nimegundua Watanzania wengi ni wagumu wa kutafuta Maarifa. Kwa maswali ulouliza inaonekana unaishi nyuma ya muda. Kifupi tu, Masomo yote hayo yanatoa walimu, na baadhi ya shule zina walimu, na baadhi ya walimu wa masomo hayo, hawana kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…