Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Tumeishi miaka hii ambayo mengi yanayotokea mbele ya macho yetu yanatoa fundisho kubwa sana kwetu na vizazi vijavyo.
Nimesikia na hata nimeshiriki kampeni za kutaka tuwe na TUME HURU ya Uchaguzi. Sambamba na hilo tumebananishana na chama letu la ajabu ajabu (CCM) likubali mchakato wa katiba mpya kwa afya na ustawi wa Tanzania
Mambo hayo yaani Tume Huru na Katiba yanaweza kuonekana ndiyo mwarobaini jadidifu wa ustawi wa siasa zenye tija kwa nchi. Lakini mimi ninaona ipo ofisi moja ya umma ambayo haipaswi kuwa affiliated na uzayuni wa CCM na wstawala wake. Ofisi hiyo ni ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
CCM imekuwa ikiitumia ofisi na mamlaka ya msajili kudhoofisha ustawi wa siasa zenye tija. Ofisi ya Msajili imeshiriki moja kwa moja na hata kwa hila kuanzisha migogoro ndani ya vyama vya siasa. Tukiangalia hiki kinachoendelea sasa ndani ya NCCR Mageuzi, tunaiona ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ikimwagia petroli mgogoro ambao imeuasisi yenyewe. Hakuna chama cha siasa za upinzani nchini ambacho hakijapitia mbinumbinu za msajili kwenye kukidhoofisha.
Tufike mahala tuweke pembeni uoga na tupaze ssuti kutaka mabadiliko yenye tija kwa Taifa.
Katiba mpya inaweza kupatikana lakini tukijisahau inaweza kurudi na uzwazwa wa taasisi zinazoikaba koo demokrasia kwa mlango wa nyuma
Uzi tayari