Tanzania tunashindwa kuwapa miradi wazawa hadi tunawapa Wachina?

Tanzania tunashindwa kuwapa miradi wazawa hadi tunawapa Wachina?

Mechanic 97

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2021
Posts
854
Reaction score
1,296
Yaani uchimbaji na uhunzi wa madini ya chuma leo 2024 ambapo wenzetu wanafikiria akili mnemba(AI) umeshindikana Mpaka mmetafuta kampuni ya kichina. Kwamba mmeshindwa kuwapa motisha kampuni za wazawa na vijana wazawa na nyinyi wenyewe mkishiriki Kwa pamoja. Hafu utasikia mabeberu wanatunyonya hawapendi tuendelee looo!
Screenshot_20240804-191234.jpg
 
ILA CCM INATUFELISHA SANA.

Naandika Kwa masikitiko makubwa mno yaani vitu ambavyo vimefanywa miaka ya nyuma (1300) Huko China na (1650) na wenzetu wa ulaya. Kesho kutwa 2/8/2024 viongozi wa CCM. Wanaenda kusaini mikataba huko mundindi Ludewa Kwa ajili ya uchimbaji wa madini hayo na uchakataji na bila shaka ni kampuni ya kichina na Wamefanya hivyo Bila hata ya kuwapa nafasi wazawa Wenda wakapata kufunguka kwa kuwa njia ya uchukuzi/barabara inakwenda kukamilika na sijui wanafanya hivi kabla ya hata barabara kukamilika ili kuwawahi wa Tz au laaa sijui yaani.

Mimi navyo fahamu uchimbaji wa madini na uchakati wa madini ya chuma na makaa ya mawee huko liganga ulisubiri tuu barabara Kwasababu haitaji teknolojia ya hali juu sana. Kutokana teknolojia ya hali inatumika pale ambapo makaa ya mawee yanakua gharama ndio hapo utahitaji tanuli la upepo wa moto (blast furnace). Lakini Kwa upande wa ludewa makaa ya mawe yapo jirani hivyo unaweza anza hata Kwa tanuli ndogo kabisa na za kawaida na kuna mwenzetu huko ludewa Mzee Kisangani kasha jaribu na alitegemeea vijana wengine kama 200 waingie.


Mimi pia nilitegemea makundi ya vijana wadogo na wa makamo kutoka pande zote za nchi wakiwamo (wasomi, mafundi, wajasiriamali na etc) wataungana pamoja na Mzee Kisangani pindi tu barabara itakapo kamilika watakwenda kufanya Moja Kwa Moja shughuli zilipo kwenye makaa ya mawee na chuma sio kuwa manamba, sijui mama ntilie, kwenye eneo la mradi ambao ni wa mchina kwenye nchi Yao wenyewe.

Mm nilifikiri kuwa ludewa ndo itakua ndio sehemu sahihi. Ambapo vijana wa nchi hii watapatia mitaji na uzoefu katika sector ya viwanda Kwa kuwa ndio sehemu pekee ambapo makaa ya mawee na madini ya chuma vipo karibu. Hivyo itawarahishia vijana kuanza chini Kwa kuwa ndio sehemu pekee ambapo makaa ya mawee na madini ya chuma vipo karibu. Hivyo itawarahishia vijana kuanza chini Kwa teknolojia ya kawaida na kukua na kupata teknolojia kubwa ambayo itawasaidi kwenda kuwekeza kwenye maeneo ambayo yatahitaji teknolojia na mitaji Mikubwa. Swali Sasa CCM Leo hii mnaamua kuwapa wa wachina mali tuliyopewa na mwenyezi mungu ambayo ni rahisi hata kwetu sisi kudeal nazo ila man aka kumpa mchina tena Kwa mvutano sana ambapo mchina anataka faida kuliko uwekezaji. Je na hayo maeneo mengine ambako ni kugumu mtampa mchina mta yaacha alidhini.

Mm nilifikiri wachina wamepewa fursa kwenye uwekezaji wa viwanda lakini kwenye malighafi anapewa mtanzania. Kwa maana nimeona viwanda pale makambako vinajengwa na nimeambiwa Nivya vyuma mm nilijua labda mnasogeza wawekazaji ila kule ludewa vijana wa Tz waanze kazi.



View:
View: https://youtu.be/MRGEoW9YI6U?si=QtIAEorUKSofnfNh
 
Mkuu, shida ni mitaji na technology,
Wew ulikuwa na hio dollar 77M tukupe ?
 
Yaani uchimbaji na uhunzi wa madini ya chuma leo 2024 ambapo wenzetu wanafikiria akili mnemba(AI) umeshindikana Mpaka mmetafuta kampuni ya kichina. Kwamba mmeshindwa kuwapa motisha kampuni za wazawa na vijana wazawa na nyinyi wenyewe mkishiriki Kwa pamoja. Hafu utasikia mabeberu wanatunyonya hawapendi tuendelee looo!View attachment 3061593
Wazawa gani hao?
ATCL imefanikiwa?
Mwendokasi una hali gali
TTCL inaishi?
Nitajie kitu kimoja tulichofanya wazawa kikafanikiwa
 
Yaani uchimbaji na uhunzi wa madini ya chuma leo 2024 ambapo wenzetu wanafikiria akili mnemba(AI) umeshindikana Mpaka mmetafuta kampuni ya kichina. Kwamba mmeshindwa kuwapa motisha kampuni za wazawa na vijana wazawa na nyinyi wenyewe mkishiriki Kwa pamoja. Hafu utasikia mabeberu wanatunyonya hawapendi tuendelee looo!View attachment 3061593
Kwani watanzania wanapatikana nchi gani?
 
Watanzania wengi kazi zao za kubabaisha sana wakipewa kazi waka haribu utalaumu tena labda waendelee kupewa uzoefu na hao wakandarasi wa kigeni hadi pale watakapo kua tayali na ujuzi wa kutosha
 
Wazawa gani hao?
ATCL imefanikiwa?
Mwendokasi una hali gali
TTCL inaishi?
Nitajie kitu kimoja tulichofanya wazawa kikafanikiwa
Asipokuelewa na hapa basi tena. Sisi hatuwezi cho chote mbali na kuiba. Wewe fikiria mwekezaji wa Kiarabu wanamnunulia mabasi mia ili aje kuendesha mradi wa mwendokasi ambao kimsingi una kila kitu. Unakuta abiria wamerundikana pale kisa eti mkatisha tiketi hana chenji. Just imagine!

We are hopelessly incompetent. Hata uongozi wa nchi wakipewa wawekezaji kwangu ni sawa tu 🚮
 
Yaani uchimbaji na uhunzi wa madini ya chuma leo 2024 ambapo wenzetu wanafikiria akili mnemba(AI) umeshindikana Mpaka mmetafuta kampuni ya kichina. Kwamba mmeshindwa kuwapa motisha kampuni za wazawa na vijana wazawa na nyinyi wenyewe mkishiriki Kwa pamoja. Hafu utasikia mabeberu wanatunyonya hawapendi tuendelee looo!View attachment 3061593
Halafu tunalia ajira hakuna, sijui think tank ya huyu mama iko wapi
 
Wazawa Gani sasa hivi wote tunawaza loophole tule. Angalia tu vijana kwenye nyuzi za ajira kila mtu ana mindset ya sehemu nzuri ya mawindo😂😂. Kwa ubatizo wa jina la asali. Hata kazi hajajua Anawaza asali
 
Tof
Wazawa gani hao?
ATCL imefanikiwa?
Mwendokasi una hali gali
TTCL inaishi?
Nitajie kitu kimoja tulichofanya wazawa kikafanikiwa
Tofautisha watu binafsi na mashirika ya CCM .
Wapo wazawa wengi sana wenye uwezo wa kuendesha makampuni yao tatizo ni Nchi kuvaliiwa na wageni kuanzia kwenye siasa .

Miaka miwili mama ameshirikiana na Doto Biteku waleuza maeneo yote yenye madini ya Tanganyika.
Kongo ina wadekezaji wengi kuliko Tanzania lakini nchi haina amani kutokana na uwekezaji wa kijambazi unaofanywa watawala wanaowaza kwenda kuishi Ufaransa kula bata. Tanzania tumepata watawala wanaowaza kwenda kuishi Dubai tutakoma na kukomaga.
 
Back
Top Bottom