Hafu taarifa inasema product itakuwa chuma ghafi yaani naona watachimba tu bila kuprocess
Kuchimba tu si angechimba wazawa.
Hayo si kama mawe ya tu yanapatikaka layer ya juu kabisa wala hayahitaji mitambo inayoendeshwa na robort.
Lakini kwa nini wasiwalete Wachina na watu wengine hata kutoka Rwanda wakawekeza kwenye Viwanda vya Chuma kisha wazawa wakachimba hayo makaa ya mawe na madini ya chuma wakauza kiwandani. Ajira zibaki hapa Tanzania . Mnje tuuze Chuma. Afrika nzima na asia ndio kuna ujenzi mkubwa unaibuka na huko Uarabuni hivyo soko la chuma ni kubwa sana .
Rais Samia ameingia madarakani tu kitu cha kwanza ni kukimbilia Kenya kuweka mkataba wa kuwauzia Makaa ya mawe na sasa ni mwaka wa tatu melfu ya masemi trailer yanasomba makaa ya mawe usiku nachana. Tenda ya kusomba hayo makaa anajua mwenyewe nani mmiliki wa hayo masemi mana yalinunuliwa kwa fujo sana baada ya huo mkataba. Huyu atakua wapi na uzalendo na Tanganyika zaidi ya kuangalia maslahi yake . Hapo alichoangalia ni kupata tenda ya kusomba makaa ya mawe na kuingiza fedha kwenye familia lakini nchi itapata nini hayo mtayaangalia nyie wenyewe.
Miaka mitatu madini ya makaa ya mawe yanasombwa kwenda nchi za nje kwa mamilioni ya tani hata kama kila tani ni sh. 100K mpaka sasa yameenda kwa maelfu
Watanganyika hatujitambui kabisa. Hatuwezi kufanya utabiri wa miaka 50 ijayo mbele tutakua kama taifa moja au nchi yenye mappande ya ma setler wanaomiliki himaya kama ilivyo Loliondo kwa waarabu na wajukuu zetu kuwa watumwa wasioweza hata kuoa na kuzaa mana hawana hata ardhi ya kujenga na kulima au kufuga . Hawa mamilioni ya wafugaji wanaoporwa ardhi zao na Biteko na Bosi wake na kuwauzia wazungu na Waarabu ili wachimbe madini watakwenda wapi maana watoto wao elimu waliyo nayo ni kufuga. Na sasa kila sehemu nchi nzima inauzwa kwa wajanja wanaoitwa wawekezaji na hatuoni tija zaidi ya kukopa kopa tu na kununua magari ya kifahari na wao kumiliki mali zisizoelezeka.
Mbona Magufuli amekaa madarakani miaka 6 hatuoni mali zake alizojikusanyia zaidi pia alikaa miaka 20 kama waziri. Mbona hatuoni mali za Mh.Philipo Mpango wakati alikua waziri wa Fedha miaka 6 ya JPM na uchumi wa nchi ukapanda bila tozo umiza na mikopo na misaada lakini pia hakuuza ardhi yetu wala madini yetu.Mafuta yakashuka bei mpaka 1500 PL.
Tatizo ni pale juu hakuna uzalendo .Anawaza mitano tena tu na sio Taifa na watu mil.65 na vizazi vyao ndio maana anauza kila kitu apate pesa za haraka haraka na kukamilisha miradi katikati ya matumizi ya anasa na starehe kabla ya 2025 arudi tena kuweka mikakati ya kuweka mtu atakayelinda uovu wao. Wazalendo kama akina Mpina wasipopambana sasa 2026 vita yake itakua ni kati ya mabeberu wa ndani wakisaidiana na wa nje kuweka madarakani watu wao kwa gharama yoyote ili kazi iendele.