Tanzania Tupate Angalau Medali Moja Katika Michezo ya Paris Olympics 2024

Tanzania Tupate Angalau Medali Moja Katika Michezo ya Paris Olympics 2024

Tunaomba kama nchi iwekeze kwenye michezo mingi, kwani michezo pia ni ajira.
 
Saa sita mchana kijana wetu Saliboko anaingia mchezoni.
 
Michezo ni hamasa , vile vituo vya michezo viwekwe kila mkoa ...Michezo yote iwe sehemu ya ajira kama mpira , basketball, kuogelea , kuendesha baiskeli na pikipiki ,Sarakasi na mengine.

Serikali ikimaliza kujenga veta basi pia wajenge vituo vya michezo angalau kila mkoa halafu wilayani ....Michezo ni ajira kuacha vijana hawana kazi za kufanyia ndio mwishoe wanajiingiza kwenye uhalifu , uvutaji wa bangi na utumiaji wa vilevi .
 
Hiyo medali tunaipata kwa miujiza au maandalizi yapi. Mashindano kibao ya riadha Diamond League, marathon kubwa anashiriki Gabriel Geay tu, naye kakumbwa na kutomaliza mbio kibao, mashindano makubwa kabla ya olympic yanafanyika Tanzania hawashiriki wanaenda mbio za uchochoroni huko China,
 
HAPO MAGDALENA NA SIMBU NDIO WATU WA KUWAANGALIA WENGINE WASINDIKIZAJI....
 
Muipate wapi ? Sizipo hizo z marathon kila siku mnapata za sijui tulia, crdb, sijui nani nani za goba nk
 
Tanzania tuna wakimbiaji wa Marathon kwa wanaume

10 August 2024
Paris, France

TANZANIA INA TUPA KARATA YAKE YA MWISHO YA MATUMAINI YA MEDALI KTK MBIO ZA MARATHON PARIS OLYMPICS 2024

Leo asubuhi jijini Paris Ufaransa katika michezo ya Olympics Paris 2024 Tanzania itakuwa na wawakilishi wawili kuiweka katika ramani ya mbio za marathon. Huku Gabriel Geay akitumainiwa kunyakua medali ...kutokana na rekodi yake nzuri alizoweka ktk michuano mikubwa alitoshiriki akiwashinda wakimbiaji mahiri wa Kenya na Ethiopia...

Tanzania banks on marathoner Gabriel Geay for Paris medal​



View: https://m.youtube.com/watch?v=creOxJNqau4

Regarded as one of Tanzania’s most promising athletes, 27-year-old Gabriel Geay finished as runner-up at last year’s Boston Marathon, outpacing legends like Kenya’s Eliud Kipchoge. Geay is now gearing up for this weekend’s race in Paris, confident in his medal prospects.
 
09 August 2024
Paris, Ufaransa

Eliud Kipchoge wa Kenya atapata upinzani mkali kutoka kwa Gabriel Geay wa Tanzania katika mbio za marathon kwa wanaume leo asubuhi tarehe 10 August 2024.

View: https://m.youtube.com/watch?v=z38aXMlVfEc
Mkimbiaji huyo wa Kenya Eliud Kipchoge umri miaka 39, na anashiriki michuano ya Olympics kwa mara ya 5 anaelezea matumaini yake baada ya kufanya vibaya mbio za Marathon huko Boston akashindwa kumaliza ktk 3 bora. Huku Gabriel Geay waTanzania alimaliza mbio za Boston Marekani akiwa mshindi wa pili na kujiweka ktk nafasi ya kufanya vizuri marathon za Paris Olympics 2024
 
Tumejitahidi lakini Watanzania! Na supoort kubwa kutoka kwa Bongo Zozo! Nimemuoa leo akiwapatia support kina Simbu! Amemaliza nafasi ya 17 huku mwenzake akishindwa kumaliza. Kilomita 42 sio mchezo aisee. Jirani yeye kupitia kwa Benson Kipruto amepata nafasi ya tatu.
 
Tumejitahidi lakini Watanzania! Na supoort kubwa kutoka kwa Bongo Zozo! Nimemuoa leo akiwapatia support kina Simbu! Amemaliza nafasi ya 17 huku mwenzake akishindwa kumaliza. Kilomita 42 sio mchezo aisee. Jirani yeye kupitia kwa Benson Kipruto amepata nafasi ya tatu.

Maumivu ya mguu na vilima vya Paris vilileta changamoto si tu kwa majeruhi Gabriel Geay bali hata wakali kama kina Eliud Kipchego pia walichemsha, ila watarudi katika ubora wao ktk mashindano mengine makubwa ya marathon duniani
 
Dada yetu Magdalena Shauri analalamika kuwa halikosa maji katika moja ya kituo kimoja! Amemaliza nafasi ya 40 katika watu 90! Amejitahidi jamani! 😀
 
Back
Top Bottom