kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Kwa muda mrefu Tanzania tulijiweka katikati ya dunia kupitia siasa ya nje ya kutofungamana na upande wowote, sera hii imetuchelewesha sana kwakuwa hakuna anaetuamini kwa 100% badala yake tuko 50/50. Hii imesababisha kukosa fursa nyingi kutoka Magharibi na Mashariki na Asia (waisalamu).
Kenya yenyewe iko 100% magharibi tangu enzi hizo, hii iliwapatia fursa nyingi kutoka upande huo kuliko sisi. Rwanda hivyohivyo, na inaisumbua DR Congo pamoja na udogo wake.
Huu ni wakati wa kuacha kupepesa macho wakati mfumo mpya wa dunia BRICS unatengenezwa. Lazima tukae siti za mbelembele kwenye tukio hili kwakuwa kwavyovyote vile dunia sasa inaenda kuongozwa na China, India na Urusi kiuchumi, kiulinzi na kiteknolojia kwa pamoja na kuungwa mkono za Brazil na nchi za Kiarabu kama Saud Arabia, South Afrika na Iran.
Tuombe mapema kujiunga na BRICS ili tuwe miongoni mwa waanzilishi wa mfumo huu ambao hata Mwl. Nyerere kama angekuwa hai nadhani angekuwa miongoni mwa waanzilishi wake.
Magharibi wana mashariti mengi sana ya kikoloni ambayo lengo lake ni sisi kuendelea kuwa tegemezi kwao milele.