Matajiri wa Tanzania wezi - Ndesamburo
na Ratifa Baranyikwa, Dodoma
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
Alimshangaa Rais Jakaya Kikwete kutoa mikopo maarufu kama ya mabilioni ya JK kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania na kuonya kuwa hali hiyo ni hatari na itawalemaza wananchi.
Tunapochukua fedha tunasambaza kwenye Saccos na kwa machinga hii nchi tunaiharibu fedha za JK hazitarudi, yeye anasema zitarudi namshangaa Tanzania yenyewe ina madeni na serikali haina tabia ya kurudisha madeni. Je, kwa mtu mmoja mmoja itarudi? Wanasema ni zawadi za uchaguzi.
Hii tabia ya kugawa fedha kama karanga inadumaza watu, inalemaza badala ya kufanya uchumi ukue unalemaa
fedha ipo tunakosa Management, ni nini tunafikia huko tunakuwa taifa la kuomba omba. Kisaikolojia ukifikiri wewe ni maskini utakufa maskini, alisema.
Katika hilo, alisema kuna haja ya Tanzania kutafuta namna ya kuwatajirisha matajiri wachache, ili waweze kuendeleza wengine kuliko kutoa mikopo kwa kila mtu.
Aidha, alisema njia pekee ya kuondokana na utaratibu mbovu wa kutozingatia taratibu wa kibiashara ni kuwa na utaratibu wa kutumia mtaji wa kuanzia biashara.
Unapokuwa kwenye venture capital itakudhibiti ukikopa fedha kwa ajili ya kujenga shule utajenga shule kuliko ilivyo hivi sasa, unakopa fedha kwa ajili ya kujenga shule zikija unajenga kiwanda na ndiyo kitu kinachotushinda katika kuleta maendeleo na hili jambo tukianza kila mkoa tutaendelea, alisema.
Akizungumzia viwanda ambavyo vimekufa katika jimbo lake la Moshi, Ndesamburo alisema kama serikali imeshindwa kuendeleza viwanda katika jimbo hilo wampe, ili aweze kuvifufua na hatimaye wakazi wa Moshi waweze kufaidika.
Niliwaambia bungeni kama serikali imeshindwa kufufua viwanda wanipe nifufue
.narudia tena serikali nipeni viwanda Moshi nifufue niviendeleze nitafute wawekezaji, vurugu zitakuwa hakuna kama tunataka viwanda viendelee, serikali ifikiri upya kuwasaidia Watanzania, alisema.
Aidha, mbunge huyo amelalamikia njia ya reli inayopita Moshi kufungwa na kuhoji sababu ya kutoiendeleza njia hiyo.
Njia ya reli ya Moshi imefungwa na ni sehemu kubwa ya uchumi wa nchi yetu, ingekuwa inafanya kazi Burundi wangeitumia na nchi nyingine katika kusafirisha mizigo kutoka katika Bandari ya Mombasa hivi tumepungukiwa akili au maarifa? Mi nafikiri tumepungukiwa kiitikadi, alisema.