Tanzania U17 (Serengeti Boys) Mabingwa wa kombe la CECAFA U17

Tanzania U17 (Serengeti Boys) Mabingwa wa kombe la CECAFA U17

SPINE

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2017
Posts
1,068
Reaction score
1,150
Serengeti boys leo ilikuwa inacheza mchezo wa fainali dhidi ya Somalia huko nchini Burundi katika mashindano ya CECAFA U17. Mchezo ambao umeisha kwa Serengeti boys kuifunga Somalia (Ocean Stars) magoli mawili kwa bila hivyo kutwaa kombe hilo la CECAFA U17.

Hongera Serengeti Boys, Hongera Tanzania.
 
ila fainali kuipeleka Gitega na hali ya hewa ikijulikana kabisa kule mvua ndio nyumbani ni kama kuwakomoa...Tunawaongeza kwa kweli wamepambana
 
Kwakweli
Hizi zote Ni juhudi za serikali yetu pendwa ya awamu ya 5

HIZI NI HABARI MBAYA SANA KWA CHADEMA, WEZI NA WALE WAPIGA DILi
 
Nini future ya wachezaji Hawa?

Hii ndio changamoto kubwa wachezaji hawa ambao bado umri wao ni mdogo wanaipata maana wengi hujikuta future yao inaishia Simba na Yanga. Inabidi wakaze msuli kwenye mashindano ya AFCON mwakani yanayoandaliwa na Tz ili wapate nafasi ya kuonekana kimataifa, inawezekana kupata timu kubwa zinazochukua vijana kwenye club zao then ikawa ndio pa kutokea.....tofauti na hapo ni kungoja baraka za muumba.
 
Nikiwakumbuka vijana hawa wala hata sishangilii ubingwa huu maana sioni future ya taifa stars.
1 Mohamed Hussein gk copa coca cola 2008
2 kabal faraj gk copa coca cola 2008
3 leodgar Ngonyani center back copa coca cola 2008
4 Lambele Jerome center back copa coca cola 2008
5 Dotto Wilson na pacha wake kulwa Wilson fullbacks copa coca cola 2008
Na wengine wengi walioipelekea Tanzania Brazil na kutwaa ubingwa
 
Ukisikia wali mlenda ndio huu sasa, mbona kle Uganda wachezaji wetu walienda kwa basi [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35]
Walienda kwa basi

kwa sababu Bombadia yetu ilkua bado imeshikiliwa kule kwa ulaya kwa wazungu.

Hiyo yote Ni kwa sababu ya Yale Majizi ya chadema
 
Nikiwakumbuka vijana hawa wala hata sishangilii ubingwa huu maana sioni future ya taifa stars.
1 Mohamed Hussein gk copa coca cola 2008
2 kabal faraj gk copa coca cola 2008
3 leodgar Ngonyani center back copa coca cola 2008
4 Lambele Jerome center back copa coca cola 2008
5 Dotto Wilson na pacha wake kulwa Wilson fullbacks copa coca cola 2008
Na wengine wengi walioipelekea Tanzania Brazil na kutwaa ubingwa
Inasikitisha sana
 
Kikosi hicho wamrbaki wachezaji watatu Lambele Jerome , Suleiman kassim selembe na kabal faraj wengine sijui wako wapi
 
Back
Top Bottom