msomi duni
Member
- Apr 11, 2024
- 90
- 301
Nisikuchoshe usinichoshe, bila kumsifu mama wala chama hata kama una masters, degree au diploma of honor Yani GPA ya nne ma straight A's huku mtaani ni laana tu kwanza unakuwa case study pili hupati michongo maana kila mtu anaona unaenda kumuovertake kwenye ugali wake ukienda kujiajiri ndio balaa tupu maana mkononi mtaji una elfu hamsini, unabaki kubishana tu vijiweni kati ya chama na pacome nani mkali utaishia kujua ofisi zote za kubeti na kama haitoshi utamsifu mama utakuwa chawa utapauka kama viatu vya mwalimu wa shule ya msingi.
Ndio maana tunaanza kuoneana wivu hadi tunaanza kutamani uchawi... Na ndio sisi tunaunga mkono kila hoja ya wapinzani ila tunakula ChiChieM na kussuport kikokotoo, mwisho nawashauri wadogo zangu kama hauna ndugu maofisini tena wenye vyeo usiwasumbue wazazi kukulipia ada bora ufanye mtaji uanze kuuza hata viatu au mawigi utanishukuru baadae.