Kitendo cha afisa habari wa simba na mjumbe wa kamati ya ushindi ya taifa stars haji manara kupost picha ya wachezaji wa simba peke yao wakifanya mazoezi mepesi kabla ya mechi na kuandika caption ya kinazi kimewauzi sana wapenzi wa yanga
Kitendo iki ni kibaya sana na kinatengeneza matabaka katika timu ya taifa na kilipaswa kikemewe na tff na pia mpk dakika hii msemaji uyu ilipaswa awe ameshaomba radhi kwa watanzania wote wapenda mpira
Ushabiki wa simba na yanga unapaswa ubakie kwenye vilabu na usiingie kwenye timu ya taifa.Na viongozi mbumbumbu kama haji manara wasiotambua na kuheshimu mipaka ya nyazifa zao na taaluma zao wanapaswa wawe makini sana kwa kauli zao na matendo yao mbele ya jamii ya wapenda soka
Wapenzi wa yanga hawapaswi kulaumiwa kwa lolote bali tff inapaswa kuwajibika katika hili na kubeba lawama zote
Tanzania kwanza! simba na yanga badae!
View attachment 1604415