Tanzania: Wagonjwa wapya 53 wa COVID-19 wathibitika, idadi yafikia 147 (Aprili 17, 2020)

Tanzania: Wagonjwa wapya 53 wa COVID-19 wathibitika, idadi yafikia 147 (Aprili 17, 2020)

Hakimu Mfawidhi,
Kijana, Sio serikali haina hela. Lazima serikali itumie hekima kwasababu 75% ya watanzania lazima wafanye kazi ndio wapate kula in every single day.

Sasa serikali kama itakurupuka pasipo na kujipanga maanake tutapoteza ndugu zetu wengi kwa njaa kulikoni Korona. Na serikali hata iwe na hela, kuwalisha watanzania hao nusu na robo baada ya miezi kadhaa itaingia umasikini.
 
Baadae Ndugu Rais, nipo zangu nimepumzika baada ya fungulia nikaamua kuishika simu yangu ya mkononi ghafla ninaona clip ya mteule wako kutoka mkoani Dodoma kwa maana ya mkuu wa Wilaya ya Dodoma akiwa anawapaka SENITAIZA

walevi walio kusanyika Bar kibaya zaidi hata yeye ameonekana hata hajajikinga kwa kuvaa hata Mask kweli jaman ili TUKIO LIMENIKATISHA TAMAA, Yani watu wanakusanyika kipuuzi vile na mkuu wa wilaya anapita kati kati yao na wengine anakumbatiana nao kabisa?
 
Magufuli anajidanganya mwenyewe kuchanganya maombi na corona, Mambo ya mungu mpe mungu ya kaizali mpe kaizali, ana hamasisha watu wasongamane sehemu za ibada Waambukizane corona bila Kuchukua tahadhari , hii yote ni kwa sababu serikali yake haina options. Sehemu za misongamano ni za kuepuka na kuzuiliwa kwa kipindi hiki.
Lengo la Serikali ya CCM ni kutaka watu wafe kwa wingi wapate kisingizio cha kuahirisha uchaguzi mpaka 2025
 
Perfectz,
Uswahilini huko Dsm watoto wadogo licha ya kufunga shule bado wanacheza pamoja, wazee wao kutwa wamejikusanya vijiweni vibarazani hawaogopi corona
 
Wamasai walinzi wa mabar wanajikusanya pamoja wahudumu wa Bar wanalala chumba kimoja wakiwa wamebanana humo hakuna hamasa ya kutosha kuzuia misongamano huko jiji la Dsm, wenyeviti wa Serikali za mitaa hawamsaidii magufuli, vijiwe vya wavuta Bangi vijiwe vya wasela bado ni vingi wazurulaji idadi ni kubwa zaidi vita ni ngumu kupita Maelezo,
 
Kwa sasa maambukizi makubwa yapo kwenye guesthouse Gym za mazoezi kwani huko wanatoka jasho kukohoa virusi vinasambaa zaidi pindi mtu akiwa anapumua kwa kasi ya mazoezi
 
Sehemu zingine zenye maambukizi ni Hosptal hususani kwa wale wapima damu kwani huvaa gloves ambazo hutumika kuwashika watu mbalimbali pindi wakiwatoa damu hivyo kupelekea kusambaza maambukizi zaidi, ni bora wapima Damu wawe wanasafisha mikono kwa sabuni mbele ya mgonjwa anayepimwa kisha anajipaka dawa ya kuzuia bacteria virus vyote.
 
Maaayo wataogundulika tena watakuwa 120+
Mungu atusimamie.

Tuweni serious, ukitembea mjini unashangaa watu yaani hawako serious kabisa na hili swala.
Unapokuwa na afya njema,unaambiwa kwa mda wa siku 14 unakatiza mitaa bila dalili yoyote,lakini kwa kuambukiza wengine ni sekunde tu. Jiulize muathirika mmoja anaweza waachia ugonjwa watu wangapi kwa siku 1 tu!

Huyo huyo qliyeambukizwa,yeye pia ana uwezo wa kumuambukiza mtu mwingine. Waliochukua hatua kali wakaonekana wajinga,wengine wakaonekana hawana chakula. Hujihurumii mwenyewe,basi na wenzako?

Madaktari na manesi wakianza kuuguwa,wanaojiona wajanja ndo mtaisoma number. Wagonjwa wakiwazidi uwezo wahudumu,ndo mtakuja kukumbuka baadhi ya maada mlizoziona za kijinga.

Hakuna cha Mungu wala raisi, karantini ndo dawa. Wenye shida ya njaa,acheni kuishi kwa mazoea,hiki kipindi kigumu sana,mnapaswa kubadiri gia ya maisha. Bado hamjaanza kuona wenye hela wanajiona wako sawa nanmkulima wa mchicha. Bado yaja aise
 
Hii itakua unpopular opinion ila nitasema ninachofikiri.

Pasi na chembe ya shaka Covid-19 ni ugonjwa hatari ila, kwa mawazo yangu, dunia nzima ime overact na jinsi ya kukabiliana na huu mlipuko.

Kinachoendelea sasa ni mashindano ya kutoa takwimu za waathirika na kutishana. Bado death rate ya corona sio ya kutisha sana kiasi cha kufanya shughuli zingine zote zisimame. Ikumbukwe watu walikua wanakufa kabla ya corona na wataendelea hata baada ya corona, it's the circle of life. Sasa kila anayefariki ni corona magonjwa mengine yote yamepotea ghafla. Hata mimi nikifa kwa corona hakuna sababu ya maisha ya wengine kusimama.

Nadhani kuchukua tahadhari tu ingetosha ila sio kusimamisha maisha ya watu juhudi ambazo hazionekani kuzaa matunda yoyote, mwishoe watu watasema potelea mbali na kurudi makazini. Dawa au chanjo ya corona isipopatikana hadi mwakani watu wataendelea kukaa ndani mwaka mzima?

Sasa bongo nao watu wanataka kila kitu kisimame sababu corona imeua watu watano toka ianze, really? I can assure you malaria imeua wengi zaidi ya hao in the last 24hrs.

According to Wikipedia, Mortality rate - Wikipedia, inakadiriwa watu laki moja na nusu hufa kila siku kwa sababu mbali mbali duniani. Sasa iweje corona iliyoua watu karibu watu laki moja na nusu kwa miezi mitatu isimamishe dunia.

www.worldometers.info/coronavirus/
Confirmed
2,173,432
Recovered
554,786
Deaths
146,291

Media nyingi zinatoa idadi ya vifo na waathrika wapya tu hawasemi wangapi wamepona. Nia ni kujazana hofu.

Come June maisha yataendelea aidha chanjo imepatikana au lah, vinginevyo we're facing economy Crashdown beyond repair. Kilichofanyika so far ni kuua sisimizi kwa nyundo.
 
Kipindi cha matatizo hasa yanayohitaji nusra kila mtu hujitaidi kwa uwezo wake wa kimawazo,kiimani na uimara wa kulichukulia jambo kutafuta njia ambayo anaamini huenda ikawa ni suluhisho kwake.Jamga letu sote, akikosea wazo mmoja basi wewe mwingine boresha ilimradi tuishinde vita hii!! Kwa pamoja hakuna kisichowezekana.
 
Back
Top Bottom