Inasikitisha sana ila ndo tukubali ukweli kuwa ile Tanzania ya watu wapole, wapenda amani wasiotaka fujo iliisha rasmi jana tarehe 29/10/2025. Hakutakuwa tena na kubembelezana kwenye mambo ya haki. Kila kitu kimeanza upya kuanzia jana.
Raia wamevumilia toka awamu ya kwanza hadi leo awamu ya 6 na wameona inatosha. Kuanzia Nyerere hadi huyu mama hakuna ambaye hakuwa kandamizi wa haki za watu. Kwa mfano hazina ya Tanzania hadi leo inalipa fidia watu walionyang'anywa mali zao na serikali ya awamu ya kwanza.
Uongozi wa mama ndo umevuka mipaka yote kwenye kuminya haki. Kupitia Mafwele na maafisa wengine wa vyombo vya usalama utawala huu umedhulumu haki ya kuishi kwa watu wengi. Binafsi Mdude na yule dogo aliyechana picha ya Rais bado wananiuma mno rohoni. Utekaji, uuaji na kuwatupa watu jela kiholela ndo mambo yamechangia leo vijana wapo barabarani.
Tumekuwa tukimtetea mama ila yeye mwenyewe anajiharibia. Imagine kwenye kampenzi za uchaguzi anajisifia kuwashughulikia wanaharakati wa Kenya!!.. kuna clip pia anaagiza watu waliokuwa wakisumbua kwenye mkutano wake washughulikiwe.
Kwa uzoefu wangu ni kuwa mama atakuwa rais hadi 2030 lakini kwenye kujisafisha lazima awatoe kafara Mafwele na genge lake. Tumuombee Mafwele naye asije dhulumiwa haki yake ya kuishi. Apelekwe mahakamani ili tujue kila kitu.
Kama hatua zisipochukuliwa huenda tukafika 2030 kwa taabu sana na huo uchaguzi utakuwa mgumu kuliko huu uliofanyika.