Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
*1.Tanzania; Una mgonjwa mahututi ndani lakini unamuacha ili uwahi mazishi ya mtu aliekufa ambae hata sio ndugu yako!*
*2. Tanzania; Mgeni akija nyumbani anakula vyakula vizuri kuliko familia yako na anatumia vyombo vizuri kuliko familia yako.*
*3. Tanzania; Ukiugua Ukaomba michango utibiwe hakuna anaejitokeza, ila ukifa wanatoa mpaka offer za maji, chakula, usafiri na jeneza!*
4.Tanzania; Unamuomba mtu msaada wa sh 10,000 anakwambia sina ila anakwambia twende tukanywe bia anakununulia bia za 30,000.
*5. Tanzania; Watu wote mtaani wanajua mke wako au mme wako anachepuka lakini hakuna wa kukwambia, wanaogopa kusutwa!*
*6. Tanzania;Unavunjiwa nyumba usiku wezi wanaiba, hakuna jirani anaemuona mwizi, lakini usiku ingiza mchepuko, asubuhi wote wanajua!*
*7. Tanzania; Ukienda bar na mwanamke, wahudumu hawakuchangamkii na wanaweza hata kumpiga kikumbo usipokuwa makini.*
*8. Tanzania; Wenye vitambi wanaheshimiwa kuliko wasionavyo, ukienda kwenye harusi na kitambi hata kadi huulizwii, ngoja uende kibaumbau uone sura ya mtu wa getini!*
*9.Tanzania; Ukimkopesha mtu hela mnakuwa maadui, usipomkopesha mnaendelea kuwa marafiki.*
*10.Tanzania; watu wanafuatilia mambo ya wasanii na kujua mpaka siri za ndani, lakini muulize mtu, asili ya ukoo wao, akutajie babu wa babu yake anaitwa nani hajui!*
*11. Ukiwa na hela unaishi vizuri mtu anakuchukia tu bila sababu, na utaambiwa unaringa, unajisikia kumbe tu umepambana umetusua!*
*12. Tanzania; Mtu yuko kwenye magroup sita, la primary, secondary, chuo, kazini, manchester fans etc, kote huko kila siku mtu kafiwa uchangie, anaoa uchangie, anaolewa uchangie, anaumwa* *uchangie, ...wewe nani uwe na hela zote hizo?? Maisha yataacha kuwa Magumu?? Punguza* *network isiyo ya lazima!*
*Watanzania tubadilike.*[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
C&P
*6. Tanzania;Unavunjiwa nyumba usiku wezi wanaiba, hakuna jirani anaemuona mwizi, lakini usiku ingiza mchepuko, asubuhi wote wanajua!*Namba 6 imewahi nitokea I see. Usiku wa kitotolo nimevusha zigo, lakini cha ushangaza naamka asubuhi nakutana na gazeti. MAJIBU NIKAPATA KUWA WACHAWI NI WANOKO BALAA.