Tanzania ya mitandaoni

Tanzania ya mitandaoni

Ni Tz ambaye huwezi kutofoutisha alie komea darasa la saba wa kidato cha nne wa cha sita na wa degree, wote niwataalamu wa kuchambua masuala ya taifa
 
Situmii WhatsApp zaidi ya miezi sita sasa,na maisha yangu hayajaharibika.

Napata muda mwingi zaidi kusoma na kusikiliza mambo ya kiimani na kujielimisha,na Nina raha sana tu.
 
*1.Tanzania; Una mgonjwa mahututi ndani lakini unamuacha ili uwahi mazishi ya mtu aliekufa ambae hata sio ndugu yako!*

*2. Tanzania; Mgeni akija nyumbani anakula vyakula vizuri kuliko familia yako na anatumia vyombo vizuri kuliko familia yako.*

*3. Tanzania; Ukiugua Ukaomba michango utibiwe hakuna anaejitokeza, ila ukifa wanatoa mpaka offer za maji, chakula, usafiri na jeneza!*

4.Tanzania; Unamuomba mtu msaada wa sh 10,000 anakwambia sina ila anakwambia twende tukanywe bia anakununulia bia za 30,000.

*5. Tanzania; Watu wote mtaani wanajua mke wako au mme wako anachepuka lakini hakuna wa kukwambia, wanaogopa kusutwa!*

*6. Tanzania;Unavunjiwa nyumba usiku wezi wanaiba, hakuna jirani anaemuona mwizi, lakini usiku ingiza mchepuko, asubuhi wote wanajua!*

*7. Tanzania; Ukienda bar na mwanamke, wahudumu hawakuchangamkii na wanaweza hata kumpiga kikumbo usipokuwa makini.*

*8. Tanzania; Wenye vitambi wanaheshimiwa kuliko wasionavyo, ukienda kwenye harusi na kitambi hata kadi huulizwii, ngoja uende kibaumbau uone sura ya mtu wa getini!*

*9.Tanzania; Ukimkopesha mtu hela mnakuwa maadui, usipomkopesha mnaendelea kuwa marafiki.*

*10.Tanzania; watu wanafuatilia mambo ya wasanii na kujua mpaka siri za ndani, lakini muulize mtu, asili ya ukoo wao, akutajie babu wa babu yake anaitwa nani hajui!*

*11. Ukiwa na hela unaishi vizuri mtu anakuchukia tu bila sababu, na utaambiwa unaringa, unajisikia kumbe tu umepambana umetusua!*

*12. Tanzania; Mtu yuko kwenye magroup sita, la primary, secondary, chuo, kazini, manchester fans etc, kote huko kila siku mtu kafiwa uchangie, anaoa uchangie, anaolewa uchangie, anaumwa* *uchangie, ...wewe nani uwe na hela zote hizo?? Maisha yataacha kuwa Magumu?? Punguza* *network isiyo ya lazima!*
*Watanzania tubadilike.*[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
C&P

Wewe unataka kutukanwa tu, tetesi zinasema kwamba kuna watu wamekupania kutaka kukudhuru kisa umesema ukweli.
 
Wewe unataka kutukanwa tu, tetesi zinasema kwamba kuna watu wamekupania kutaka kukudhuru kisa umesema ukweli.
[emoji34][emoji35][emoji35][emoji35]nitawaroga wote [emoji34][emoji35][emoji35][emoji34][emoji12][emoji86]
 
Kwenye magroup ya watsapp ndo umeniacha hoi, kuna jamaa kwenye daladala nlipata kuchungulia simu yake alipoitoa, dah si kwa magroup ile jamani
 
Tanzania nchi pekee ambayo mganga anaweza kutumia smartphone na kuvaa pensi.

C&P.
 
Huu uzi inatakiwa usomeke ujinga wa watanzania
 
Kwenye magroup ya watsapp ndo umeniacha hoi, kuna jamaa kwenye daladala nlipata kuchungulia simu yake alipoitoa, dah si kwa magroup ile jamani
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Namba 6 ndio imenichekesha zaidi
 
Namba 6 imewahi nitokea I see. Usiku wa kitotolo nimevusha zigo, lakini cha ushangaza naamka asubuhi nakutana na gazeti. MAJIBU NIKAPATA KUWA WACHAWI NI WANOKO BALAA.
 
Back
Top Bottom