Tanzania ya Samia bado ni ya Magufuli: Acheni Kujitoa Ufahamu Ndugu zetu

Hakika ajenda ni yake Mwenzake Msiri na Mshirika wake hayati JPM [R.I.P] waliekuwa karibu na walitangaza ilani ya CCM pamoja na kuanza utekelezaji wake wakiwa pamoja.
 
Bado namkumbuka yule jamaa aliyeambiwa na Rais hadharani "baki na m.av.i yako nyumbani"

.....simuoni huyu mama akidhalilisha watu kwa namna hivyo! Unless tunasema hizo ndizo "agenda" za CCM ambazo mama lazima azitekeleze!
Kuna mada nilianzisha ya ‘Umagufuli bila Magufuli’.

Nimezungumzia jambo kama hilo.

Ila wengi wa waliochangia naona hata hawakunielewa!

Agenda ya Magufuli inaweza kutekelezwa bila lugha za namna hiyo.

Uongo?
 
Reactions: SMU
Yani kumpongeza mtu within 3days tayari wapinzan wamepoteza agenda? Kwamba kwa hizo siku 3 upinzan umeacha kazi zake? Inamaana wapinzani wakiona jambo zuri wakasifia tayari wanakuwa wamepoteza agenda, mbona by then mlikuwa mnalaum kwa nini hawaungi mkono lolote. Halafu ulitakiwa ujifunze kwamba, kumbe wapinzani walikuwa against na model za Magufuli kufikia dhamira yake! Upinzan utaendelea kuji adjust ili ufit in kulingana na mazingir, atapongezwa akifanya vizur na akizungua atachachafya tu.
 
Bendera fuata upepo,au?
 
Mwaga raia mwaga..
 
Jaffo hata magu alishaanza kumsema. Mtashangazwa
 
Aliumiaje? makamu wa rais?

JPM was firm hakutaka kuleana, na hamkumpenda maana aliburuza vitu na we needed him sana
Hayo ni maswali gani unauliza sasa. Kwahiyo nyie mlipenda alivyoburuza vitu. And you needed him? Go get him....
 
Ikulu Chamwino
Dodoma, Tanzania

Muonekano mpya wa Rais wa Jamhuri ya Muungano akiingia ktk Ikulu ya Chamwino

Mh. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiingia bila mbwembwe za ulinzi mkali kujikinga dhidi ya njama za "mabeberu na vikaragosi wao waliopo Tanzania wasio wazalendo".
 
Kama kuna viongozi wengi wazuri,kwa nini CCM ilitumia fedha nyingi kuwanunua wapinzani,na kisha kuwapa uongozi?.
 
Waulize wakina sabaya na heri James watakufafanulia vizuri, naona somo hujalipata bado.
 
Ni kama watu wanajitahidi kuukataa ukweli. Wanaombea usiwe ukweli...Mama Samia hana ajenda yake Wala ahadi zake... Ameingia kumalizia ngwe ya pili Rais Magufuli. Sasa ataimalizaje bila kuangalia ahadi zao jwa wananchi?
 
Mtoa mada you are very bright agree with you buddy.. hakika wapinzani ni vigeu geu kupitia mada hii uliyopost , mwenye macho haambiwi tazama that is the fact na ukweli utabaki pale pale hahahha asante kwa kudadavua kwa kina..BIG UP
 
Bahati mbaya uelewa wa "Nyumbu wa Ufipa" ni mdogo sana!
 
Nilidhani Tanzania ni ya Watanzania..., kumbe ni ya mtu (aliyepo madarakani) Kwahio bado tupo kwenye enzi za utawala wa Kifalme ? Kwahio Rais ni Dictator anayefanya anayvotaka ? Kwahio kama Magufuli alijikwaa na kukosea na huyu mama aendelee kujikwaa ili tu kufuata nyayo ?

By the way niambie ni muongozo upi either wa CCM au popote pale uliosema kutofuata protokali na kuminya uhuru wa kujieleza, kuleta ubaguzi, dhiaka as well as kutochukua ushauri (Nadhani wengi wanaomlaumu Magufuli ilikuwa ni kwenye hizi issue)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…